read

71 - Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Na Miongoni Mwa Khutba Zake (a.s) - Al-Mufid ameielezea katika al-Irshad uk. 61, na ibn Da’abiy katika al-Ikhtiswas uk. 155, na Tabrasiy katika al-Ihtijaj Juz.1, uk. 254.

Katika Kuwalaumu Wa-Iraqi:

“Ama baada! Enyi watu wa Iraqi, mko kama mwanamke mwenye mimba, ameshika mimba na alipotimiza upevu wa mimba akaporomosha mimba, na mumewe akafariki, kwa hiyo muda wake wa ujane ukawa mrefu, na akarithiwa na wa mbali kabisa.1 Wallahi sijakujieni kwa hiyari; isipokuwa nilikujieni katika hali ya kusukumwa.2

Nimepata habari kuwa ninyi mwasema: ‘Ali anasema uwongo, Mungu (swt) akuangamizeni! Nani nimsemee uwongo? Nimuongopee Mungu? Mimi ni wa kwanza kumwamini! Au nimsemee uwongo nabii wake? Mimi ni wa kwanza kumsadiki yeye!

Hapana wallahi, lakini hiyo ni ibara ambayo mmeshindwa kuitambua maana yake,3 hamkuwa wenye kustahiki nayo, Waylumah, ninakupimieni vipimo vya kiilimu na hikma, upimaji usio na thamani,4 lau angekuwa na chombo apime humo.” “Na bila shaka mtajuwa habari zake baada ya muda,” (38:88)

  • 1. Anakusudia kuwa wao walipoona kuwa watu wa Sham wanakaribia kuangamizwa, na kujitokeza alama za kuwashinda, walielemea kwenye (wazo la suluhu) mapatano ya kusimamisha vita, ili kuwaitikia walioomba kufanya tah’kiimu, hivyo basi mfano wao ukawa sawa na mwanamke mwenye mimba, alipotimiza miezi ya mimba yake, akamporomosha mwanawe bila ya kutokea sababu ya kimaumbile, bali kwa sababu tu ya tukio lililojitokeza, kama kipigo na kuanguka, na halifanyi hilo ila ataangamia. Na wala hakutosheka katika kuifanyia mfano hofu yao katika hilo, bali alifikia kusema: ‘Na akafa mumewe akiwa katika hali hii, na udhalili wake ulichukua muda mrefu, kwa sababu ya kumkosa kwake wa kumsimamia, mpaka akifa bila ya mtoto, watamrithi wa mbali walio duni katika daraja kinasaba, miongoni mwa ambao nasaba yake haitiliwi manani.’
  • 2. Anaapa kuwa yeye hakuja Iraqi akiwaomba nusra watu wake kwa hiyari kwa kuwaboresha wao juu ya wengine, isipokuwa alisukumwa kwao na msukumo wa dharura, kwani lau si tukio la Jamal (ngamia) asingefarikiana na Madinatul’Munawarah. Na maneno haya pia huelezwa kwa njia nyingine, nayo: Sikuja kwenu kwa hiyari, wala sikuja kwenu kwa shauku na ninyi.
  • 3. Lahaja: Ni kiungo cha mwili cha kutamkia, husemwa: ana lahaja fasaha. Na inawezekana anakusudia hapa lahaja ya Rasuli (s.a.w.w.), na inawezekana anaikusudia lahaja yake yeye mwenyewe; anasema kwamba hiyo ni lahaja ambayo mko mbali na man- ufaa yake, yaani aina ya maneno ambayo ninyi mko mbali na maana yake, hivyo hamyafahamu, kwa ajili hiyo ndio mnayakadhibisha.
  • 4. Neno: husemwa kuonesha kustaajabishwa na kutukuza; huandikwa lime- unganishwa na asili yake: na mradi wao ni kuadhimisha, hivyo basi lasemwa mahali pa kusifu japokuwa asili ya madhumuni yake ni kinyume chake. Na mifano kama hiyo ni maarufu katika lugha yao (watu wa Basra) kwani wao humwambia mtu wanayemheshimu na kumtukuza: na Hasan Al’Basriy alisema hali yu amtaja Ali (a.s) akimueleza kuwa yeye yuko na haki katika mambo yake yote: lau ningepata chombo nipime humo, yaani lau ningezipata nyoyo zenye kupokea na akili tambuzi.