read

73 - Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Na Miongoni Mwa Maneno Yake (a.s) - Ibn Sa’ad ameieleza sehemu ya maneno haya katika Tabaqat, Jz. 1, na al-Baladhuliy kati- ka al-Ansab, uk. 361.

Alimwambia Marwan Bin Al-Hakam Huko Basra

“Walisema: Marwan bin Al-Hakamu alitekwa siku ya Jamal na aliwasihi Hasan na Husain wamuombee kwa Amirul-Mu’minina (a.s). Nao walisema naye kuhusu suala lake, naye (Amirul’Mu’minina) alimwacha huru. Walimwambia (wasemaji ni Hasan na Huseni): Akuba’i ewe Amirul- Mu’minina.Akasema (a.s.):

“Kwani hakunifanyia bai’a baada ya kuuliwa Uthman? Sina haja ya bai’a yake! Kwa kuwa huo ni mkono wa kiyahudi,1 lau anifanyie bai’a kwa mkono wake angenisaliti kwa tako lake.2 Ila tu yeye Marwan atakuwa na uamiri wa muda mfupi kama vile mbwa anavyoramba pua yake. 3 Na yeye ni baba wa maraisi wanne wa kaumu.4
Umma utapata siku nyekundu kutoka kwake na kwa wanawe.”5

  • 1. Mkono wa kiyahudi yaani: wakisaliti wenye vitimbi, na uyahudi hunasibishwa na vitimbi na udanganyifu.
  • 2. Tako ni kitu mtu huwa na pupa ya kukisitiri, na amelitumia hapo likiwa jina mbadala la vitimbi vya chini kwa chini, na amelichagua kwa ajili ya kumdunisha mwanavitimbi.
  • 3. Uamiri: Ni utawala, na usemi wake: ‘kama mbwa anavyoramba pua yake’ anakusudia muda wa utawala wake utakuwa mfupi, na ndivyo ulivyokuwa muda wa ukhalifa wa Marwani, kwa kuwa alitawala miezi tisa. Na riwaya husika ya Amirul-Mu’minin kuhusu Marwan: “atabeba bendera ya upotovu baada ya panja zake mbili kuwa na mvi”. Kwa kuwa yeye alishika uongozi wa ukhalifa akiwa na miaka 56 katika riwaya ya wastani.
  • 4. Al-Akbush: ni wingi wa Kabshu, nayo katika kaumu ya watu ni raisi wao. Na wamefasiri al-Akbushu kuwa ni Abdul-Malik bin Marwan huyu, nao ni al-Walid, Sulayman, Yazid na Hisham. Na wamesema: Hawakuutawalia ukhalifa ndugu wanne isipokuwa hawa. Na inajuzu iwe wamekusudiwa wana wa Marwan mwenyewe, nao ni Abdul-Malik, Abdul-Aziz, Bashar na Muhammad, na walikuwa kundi shujaa: Ama Abdul-Malik alitawalia ukhalifa, na Muhammad alitawala Jaziira, na Abdul-Aziz Misri, na Bashar Iraqi. Na tafsiri hii ni bora; kwa sababu al-Walid na ndugu zake ni watoto wa mwanawe, na hao ni watoto wa mgongo wake.
  • 5. . Siku nyekundu: Ni siku ya shida, waarabu husema mwaka wa ukame mwaka mwekundu.