read

75 - Na Miongoni Mwa Semi Zake (A.S)

Na Miongoni Mwa Semi Zake (a.s) - Ibn al-Athir ameieleza katika an-Nihayah katika mada ya Qirzu.

Alipopata Habari Kuwa Bani Umayyah Wanamtuhumu Kushiriki Damu Ya Uthman

“Je Bani Umayyah kunijua kwao hakujawazuia kuniaibisha? Je kutangulia kwangu (kuukubali uislamu) hakujawaweka mbali wajinga na kunituhumu? Kwa kweli aliyowaonya Mungu amewaonya kwa ufasaha zaidi kuliko ulimi wangu, mimi ni mtoa hoja dhidi ya watokao nje ya dini, na ni hasimu wa wavunjao ahadi na wenye shaka,1 na kwenye Kitabu cha Mungu.

Kwa Kitabu cha Mungu hupimwa yasiyo wazi.2 Kulingana na yaliyo mioyoni waja watalipwa.” Anaikusudia kauli yake (swt) “Hadhani khasmani ikh’taswamu fii Rabbihim” (22:19)

  • 1. Anakusudia Siku ya Kiyama, imeelezwa kutokana naye (a.s.) usemi: “Anaa awwalu man yaj’thu lilhukuumati bayna yaday llahi taala” - Mimi ni wa kwanza miongoni mwa watakaopiga magoti mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • 2. Aikusudia kauli yake (swt): “Hawa wagomvi wawili waliogombana kwa ajili ya Mola wao Mlezi” (22:19), hivyo basi mambo yanayotatanisha hupimwa na Qur’ani, linaloafikiana nayo ndio haki kisharia, na litakalokwenda kinyume nayo ndio batili linakatazwa kisharia. Na yeye, Karrama-llahu waj’hahu amekwenda kwa mujibu wa hukumu ya Kitabu cha Mungu (swt) katika matendo yake, hana haki mwenye kukifumbia macho amnyooshee kidole cha kebehi hali yeye (a.s) akiwa yu ajiambatanisha na hukumu ya Kitabu.