read

76 - Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Na Miongoni Mwa Khutba Zake (a.s) - Ameyaeleza hayo al-Haraniy katika at-Tuhaf, uk. 150, na ibn Shakir katika Uyunul- Hikami wal mawa’idh, na Zamakhshari katika Rabiul-Abrar Jz. 1, uk. 231, na al-Hisriy katika Zuhurul-Adabi, Jz. 1, uk. 42.

Kuhusu Zuhudi

“Mungu amrehemu mtu aliyeisikia hukumu akaihifadhi na kuielewa, na aitwapo kwenye mwongozo akausogelea,1 na amfuata kiongozi (kwa kushika mkanda wake wa kiunoni) na akaokoka, akajihadhari na Mola wake Mlezi, na kuhofia dhambi zake, akatanguliza ikhlas na kutenda mema, akachuma na kupata hazina, na akajiepusha na yaliyohadharishwa. Na akalenga lengo, na kufanikiwa kupata kitu mbadala, akaukabili utashi wake, na kuyakadhibisha matumaini yake (bandia), na akaifanya subira kuwa ndio njia yake ya uwokovu, na taqwa kuwa ndio masurufu ya kifo chake. Akapita njia ya haki, kwa mwenendo wa kiadilifu, na akijiambatanisha na njia ya hali ya juu ya ukweli, na kuutumia vyema wakati wake, na kuuharakia mwisho (wake), na akaenda na akiba ya matendo mema.”

  • 1. Hukumu hapa: Ni hekima, Mungu (swt) amesema: “Nasi tulimpa hekima angali mtoto;” (19:12).