read

77- Na Miongoni Mwa Semi Zake (A.S)

Na Miongoni Mwa Semi Zake (a.s) - Al’Isfahaniy ameielzea usemi huu ndani ya ‘Al-Aghaaniy’ Juz. 11, uk. 29, na Al-Azhariy ndani ya ‘Tah’dhiibi-lughah’ Juz. 15, uk. 27.

Kuwahusu Bani Umayyah

“Kwa kweli Bani Umayyah wananiruhusu kiasi kidogo cha mirathi ya Muhammad (s.a.w.w.). Wallahi endapo nitabaki nitawapuliza mpulizo wa muuza nyama apulizapo mnofu wa nyama ulioenea mchanga!”

Maelezo

Ar-Radhiy (r.a) amesema: Na yaelezwa kwa tamko nayo iko katika hali ya kugeuza, kwa sababu ukweli ni kama ilivyokuwa katika riwaya ya kwanza, sio kwa kuwa hilo halina maana, kwa hiyo hii yakusudiwa riwaya iliyogeuzwa.

Na kauli yake (a.s) (Layufawiqunaniy) yaani wananipa kutoka mali ya (Muhammad) kitu kidogo sawa na mkamo mmoja wa maziwa ya ngamia. Na wid-hamu at-taribatu: ni udongo, ni wingi wa neno wadhamatu, nacho ni kipande cha tumbo au cha ini kilichoanguka na kutapakaa vumbi hupulizwa.