read

81- Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Na Miongoni Mwa Maneno Yake (a.s) - Saduq ameieleza katika Ma’anil-Akhbar, uk. 251, na katika al-Khisal, Jz. 1, uk. 11, na al- Barkiy katika al-Mahasin, uk. 234.

Kuhusu Zuhudi (Kutotilia Manani Raha Ya Dunia)

“Enyi watu! Zuhudi ni kupunguza matumaini,1na kushukuru neema,2 na kuogopa kujiingiza kwenye haramu,3 na endapo hilo likiwa mbali kwenu basi haramu isiishinde subira zenu,4wala msisahau shukrani kwenye neema, Mungu amemaliza udhuru kwenu,5 kwa hoja zilizo wazi, na vitabu vilivyo na udhuru wa wazi.”

  • 1. Kupunguza matumaini: Kuchelea mauti na kujiandaa nayo kwa matendo, na wala mradi wake sio kuungojea umauti bila ya kazi.
  • 2. Kushukuru neema: Ni kutambua kuwa yatoka kwa Mungu na kuitumia kulingana na sharia.
  • 3. Sheikh Muhammad Abduh amethibitisha katika matni kuwa kuogopa maana yake ni kujizuia na jambo lisilo wazi ukweli wake, ili kuchelea kuingia ndani ya matendo ya haramu. Yaani endapo la haramu likijitokeza itakuwa ni katika zuhudi kujizuia na linalofanana nalo sembuse la haramu.
  • 4. Hilo likiwa mbali kwenu basi ni mambo mawili katika matatu ambayo hapana budi na mawili hayo; mambo hayo ni: woga na kushukuru neema, ameyafanya kuwa na nguvu zaidi na ni muhimu sana kuliko kufupisha matumaini, na endapo ikiwawia vigumu kufupisha matumaini yenu na kuwa katika ukamilifu wa zuhudi itakiwayo kwenu, basi haramu isi-ishinde subira yenu, yaani hizi nguzo mbili nyingine zisikupiteni, nazo ni: Kushukuru neema, na kujiepusha na haramu; kwa sababu kusahau shukrani kwavuta kujidai, na kutenda ya haramu kunaharibu nidhamu ya maisha haya na ya marejeo. Na kujidai na ufisadi vyaleta malipizi duniani, na maisha ya mashaka na majuto akhera.
  • 5. Mungu amemaliza udhuru kwenu yaani ametimiliza, anakusudia kuwa yeye ameweka wazi kwenu kwa hoja zenye mwanga zinazowajibisha kujiuepusha, na zinazowajibisha kutenda, endapo mtafanya kinyume adhabu itakuwa wajibu juu yenu, hivyo Yeye katika kuwaadhibu anao udhuru. Na yaani amefanya insafu, na hamza hapa wanasema yamaanisha kuondoa, yaani usemapo yaani nimempa fulani udhuru yamaanisha nimeondoa udhuru wake sikumwachia nafasi ya kutoa udhuru endapo atahalifu niliyomnasihi. Na pia husemwa yaani nimejisimamishia binafsi kwake udhuru uliowazi kuhusu adhabu nitoayo kwake kwa kuwa nimemhadharisha na nimempa nasaha.Na inafaa ibara iwe katika kitabu kwa maana hii pia, bali yenyewe ndio iliyo karibu na tamko Ilaykum. Na maneno yanakuwa majazi na kutimia kwa hoja upande wake ni kukam lika kwa udhuru kwetu.