read

95 - Na Miongoni Mwa Khutba Zake (A.S)

Anaelezea Katika Khutba Hii Hali Ya Watu Ilivyokuwa Wakati Wa Bi’tha

Allah swt. alimtuma (Muhammad) hali watu wakiwa wapotevu katika mkanganyiko, na wakikusanya fitna,1 utashi wa nafsi umewaghilibu, na kibri kimewafanya wateleze,2 na jaahiliya iliyoshona imewahafifisha,3wameduwazwa na myumbo wa mambo, na balaa la ujinga.

Hivyo basi Mtume (s.a.w.w.) alikithirisha katika kutoa nasaha nyofu, naye alipita njia ya sawa, na aliwaita kwenye hikima na mawaidha mema.”

  • 1. Wanao kusanya fitna: Ni wanaokusanya kuni: Na Waarabu humwita anayechanganya kati ya maneno mazima na mabovu au asemaye kati ya maneno ya sawa na yaliyopotoka: Haatibul’layli: Mkusanya kuni usiku, kwa kuwa hajui kinachokusanywa na kamba yake.
  • 2. Kiburi kimewatelezesha: Yaani kimewafanya wateleze na wawe kwenye makosa, kikawapeleka kwenye mtelezo na kuanguka kwenye madhara. Na katika riwaya nyingine, Istazahum (al-kubarau) yaani wakubwa wao na mabwana zao wamewapoteza.
  • 3. Jahiliyah ni hali waliokuwa nayo Waarabu kabla ya nuru ya elimu ya Uislamu: ikawafanya wawe na akili hafifu.