read

97 - Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S.)

Kuwakemea Sahaba Zake

Japo Mwenyezi Mungu amwachie muda dhalimu mshiko wake hautomkosa, naye yuamchunga kwenye mapito ya njia zake, na mahali pa mkwamo wa koo mapitio ya mate yake,1 naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hawa watu (Mu’awiya na kundi lake) watapata ushindi dhidi yenu,2
si kwa sababu wana haki zaidi kuliko mliyonayo bali ni kwa sababu ya haraka yao ya kutekeleza batili yao na ugoigoi wenu mbali na haki yangu (kuifuata). Umma huwa waogopa dhulma ya niliwaiteni kwa siri na kwa wazi hamkuitika, nilikunasihini hamkukubali.

“Mkiwa mpo kama hampo, mko watumwa kama mabwana!3 Ninakusomeeni nukta za hekima mnazikwepa, na ninakuonyeni kwa mawaidha yafikayo (masikioni) mnafarakana mbali nayo, nawahimizeni kwenda jihadi dhidi ya watu waovu, wala sijafikia mwisho wa kauli yangu nawaona mnatawanyika mfano wa mikono ya Sabaa - Ayaadiy sab’a. 4 “Munarejea kwenye makazi yenu mkiwa hamuwaidhiki. Nakunyoosheni asubuhi, mwarejea kwangu jioni mkiwa mmepindama kama upinde, mnyooshaji amehemewa na mnyoshwaji amekuwa mgumu.

“Enyi kaumu ambao miili yao ipo hadhiri hali akili zao zimeghibu, na ambao utashi wao uko tofauti. Watawala wao wamepatwa na balaa. Sahibu yenu yuamtii Mungu, na ninyi mnamuasi, na sahibu wa watu wa Sham yuamuasi Mungu na hali wao wanamtii! Ningependa, wallahi lau Muawiya hangenibadilishia ninyi ubadilishaji wa dinari na dirham, angewachukua kutoka kwangu kumi kati yenu na angenipa mimi mtu mmoja kutoka wao!

“Enyi Watu wa Kufa! nimepata uzoefu kwenu wa matatu na mawili mengine: Mko viziwi hali mkiwa na masikio, na mko mabubu hali mkiwa mwasema, vipofu mlio na macho. Sio wasaidizi wa kweli wakati wa mapambano wala sio ndugu wa kuaminika kwenye balaa! Mikono yenu iingie mchanga!( – yaani mikono yenu isiwe na kheri! - hili ni neno la kumlaani mtu). Enyi mlio mfano wa ngamia ambao mchungaji wake ameghibu! Kila wakusanywapo upande mmoja wanatawanyika upande mwingine.

Wallahi nawaona kwa maoni yangu, endapo vita vitakuwa vikali na hali ya mambo ikiwa inayumba mtamkimbia mwana wa Abi Talib ukimbiaji wa mwanamke akiwa uchi mbele, kwa hakika mimi nipo katika mwongozo wa wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, na (niko) katika njia ya Nabii wangu, na niko katika njia ya wazi nikiokota cha kuokota.5

“Waangalieni Ahlul-bayt wa Nabii wenu, na jiambatisheni na mwendo wao, na fuateni nyayo zao, hawatokutoweni nje ya mwongozo, na hawato kutumbukizeni kwenye maangamizi, wakikaa kaeni wakiinuka inukeni, msiwatanguliye mtapotea, wala msibaki nyuma yao mtaangamia.
Kwa kweli nimewaona sahaba za Muhammad (s.a.w.w.) simuoni yeyote kati yenu anashabihiana nao, kwa kweli walikuwa wanaianza asubuhi wakiwa na nywele timtim na wakiwa wamejaa vumbi kichwani (na mwilini).6

Wamepitisha usiku katika hali sijda na qiamu, wakibadili kati ya paji zao za uso na mashavu yao ( yaani mara wakisujudu kwa paji la uso na mara nyingine kwa mashavu yao). Na walikuwa wanasimama mfano wa aliyesimama juu ya kaa la moto kwa ajili ya kukumbuka marejeo yao, kana kwamba kati ya macho yao kuna goti la mguu wa mbuzi kutokana na sijda zao ndefu. Atajwapo Mungu macho yao hutiririsha machozi mpaka yalowesha kosi (kola zao), walikuwa wana yumba kama uyumbavyo mti siku ya upepo mkali, wakiogopa adhabu, na wakiwa na matarajio ya thawabu.”

 • 1. Mahali pa mkwamo wa koo (ambapo hukwama mfupa au mwiba), mapitio ya mate: maneno hapa yametumika kimfano kwa ukaribu wa ukali wa ki-ungu dhidi ya madhalimu.
 • 2. Kisha (a.s) aliapa kuwa hapana budi watu wa Sham - Syria - watapata ushindi dhidi ya watu wa Irak, na hiyo si kwa kuwa ndio wenye haki na kwamba watu wa Iraki (watu wa Iraki hapa ni jeshi la Amirul-Mu’minina Ali bin Abi Talib) wako katika batili; bali ni kwa kuwa wao (watu wa Sham ambao ni watu wa jeshi la Muawiyah bin Abi Sufian) ni watii mno kwa amiri-jeshi wao, yaani kamanda wao wa vita; na kigezo cha ushindi vitani ni utii wa jeshi kwa kiongozi wao na kutengenea kwa mambo yake, si katika kuwa waamini itikadi ya haki ndio lazima ushinde! Kwa kuwa vitani haitoshi kuwa jeshi lipo kwenye haki hata rai zitafautiane, na liwe halitii amri ya mnadhimu wake, kwa ajili hiyo waona mara nyingi washirikina wanashinda dhidi ya watu wenye itikadi ya tawhidi. (Kwa mantiki hiyo usemi ulio zoeleka: “Mungu mwenyewe atainusuru dini yake,” hauna maana yoyote, bali ni dalili ya kutoelewa mambo yapasavyo kuwa.
  watawala wake,* hali ikiwa mimi nimekuwa nahofia dhulma ya raia wangu. Niliwaita kwa ajili ya vita hamkuja, niliwaonyeni hamkunisikiliza, (*) Kisha (a.s) alikumbusha nukta nzuri kuhusiana na maana hii, akasema: “Kwa kawaida raia ndiye aogopaye dhulma ya mtawala, lakini mimi naogopa dhulma ya raia wangu.” Na mwenye kuzingatia hali yake (a.s) zama za ukhalifa wake, atatambua kuwa alikuwa mfano wa mtu aliyewekewa vikwazo; alikuwa hawezi kuyafikia ayakusudiayo nafsini mwake. Hiyo ni kwa sababu wamjuao ukweli wa hali yake ni kidogo mno; na kundi kubwa la watu lilikuwa haliamini kumhusu Amirul-Mu’minina ambavyo ipasavyo kuamini, na walikuwa kwa maoni ya waliomtangulia katika makhalifa ni bora kuliko yeye, na wengi wanadhania kuwa ubora upo katika kushika ukhalifa kwa hali yoyote ile, hata kwa nguvu, kama vile mfano wa Muawiyah, kundi kubwa la waislamu wanaona kuwa yeye ni khalifa yapaswa aitwe Amirul-Mu’minina, hali yaendelea hivyo, wafuatao wanawakalidi waliotangulia; na wanasema: ‘Lau waliotangulia wangejua kuwa yuko bora kuliko wao wasingewatanguliza waliotangulia.’ Na hawamzingatii ila ni mfuasi wa waliomtangulia kwa ubora. Na kwamba yeye alikuwa raia wao, na wengi wao walikuwa wanapigana katika kundi lake kwa ushabi- ki tu na kwa fahari ya ushujaa wa kiarabu, sio kwa ajili ya dini na itikadi. Na yeye (a.s) alikuwa analazimika kwenda nao kwa upole na kuwakurubia; alikuwa hawezi kudhihirisha aliyonayo; angalia barua zake kwa watendaji wake kwenye mikoa! Kama usemi wake: “Hukumu ni kama mlivyokuwa mnahukumu ili ipatikane jamaa kwa watu, na nife kama walivyo kufa swahibu zangu”. Maneno haya hayahitaji ufafanuzi zaidi, maana yake iko wazi, nayo ni kuwa yeye aliwaambia: “Fuateni kawaida yenu kwa hivi sasa katika haki hii ya haraka kuhusu hukumu na maamuzi ambayo mlikuwa mnahukumu mpaka watu wawe na umoja; yaani mpaka mambo haya yafikie mtangamano na kutoweka mfarakano, na kutu- lia kwa fitna. Hapo nitawatambulisha niliyonayo kuhusiana na mambo haya na hukumu ambazo mlikuwa mmeendelea nazo.

  Kisha alisema: “Au nife kama walivyokufa sahibu zangu.” Kuna anayesema: ‘Sahibu zake hapa; alikuwa anakusudia makhalifa waliomtangulia.’ Na kuna anayesema: ‘Sahibu zake alikuwa anakusudia Shi’a wake mfano wa Salman, Abu Dhar, Miq’dad, Ammar na wengine mfano wao.’ Huzingatii kauli yake akiwa juu ya mimbari kuhusu mamawatoto: “Rai yangu na rai ya Umar ni kwamba wasiuzwe, na mimi sasa naona wauzwe”.
  Inaendelea uk.81
  Basi Ubaida Assalmaniy, akamwambia: ‘Rai yako ukiwa pamwe na jamaa yapendeza mno kwetu kuliko rai yako peke yako.’ Hakurudia kusema lolote. Je hili lajulisha nguvu na kuyadhibiti mambo; au udhaifu katika mamlaka na unyonge?! Je hekima na maslahi katika wakati ule ilikuwa sio kunyamaza na kujizuia?! Huzingatii (tukio moja) alikuwa akisoma katika sala ya asubuhi nyuma yake kukiwa na jamaa katika sahibu zake; mmoja wao aka- soma hali amepaaza sauti yake, akiwa anakinza usomaji wa Amirul-Mu’minina (a.s): “inil’hukmu illa lillahi yaq’dhwii bilhaqi wahuwa khayrul’faasiliina.” (Hapana huku- mu ila ni ya Mungu, anahukumu naye akiwa mfanya maamuzi bora). Hakubabaika alay his-salaam, na wala hakuvunja sala yake na wala hakugeuka nyuma, lakini yeye alisoma hali akimpinga: “fasbir inna wa’ada llahi haqun wala yastakh’lifannaka lladhiyna la yuuqinuuna.” Na hii ni subira kubwa na utulivu wa ajabu na ni tawfiiq iliyo bayana. Kwa haya na mengine mfano wake sahibu zetu miongoni mwa mutakalimiina wameyatolea dalili juu ya uzuri wa siasa yake na usahihi wa uratibu wake, kwa kuwa mwenye kupatwa na ria kama hawa wenye utashi unaopingana, na jeshi kama hili linalomuasi na linalompinga, kisha kwalo akavunja maadui, na viongozi, hafiki yeyote alipofika kwa uzuri wa siasa na uzuri wa mpango. Mwisho wa Tanbihi *

 • 3. Watumwa kama mabwana: anawasifu kiburi na upotovu.
 • 4. Ayaadiy Sabaa: Mikono Sabaa, mithali hupigwa kwa kiarabu kwa wenye kufarakana. Yasemekana: Kuwa Sabaa ni Abu Arab Al-Yamani, alikuwa na watoto kumi, akawaweka sita kuliani na wanne kushotoni; akiwafananisha na mikono miwili, baadae watoto hao walitawanyika vibaya sana, ndio maana waarabu huupigia mfano mfarakano wowote na mfarakano wa ayaadiy sab’a - mikono Saba.
 • 5. Naokota chakuokota: Anamaanisha kuwa upotovu umefikia kiasi cha kuushinda mwongozo, kwa hiyo mimi naiokota njia ya mwongozo kati ya njia za upotovu nikiokota huku na kule. Na kuokota ni namna ya uchukuaji kitu kutoka ardhini, na kuitwa kwa wafuasi wake kuihusu njia ya haki kuokota ni kwa sababu haki ni moja na batili ziko rangi tafauti, hivyo basi yeye huiokota haki kati ya aina kadhaa za batili.
 • 6. Wanaianza asubuhi wamejaa vumbi: Ni ibara ya kuelezea maisha yao ya kujinyima na kujibidisha sana kiibada, kwa mfano, kusali sala za usiku, kufunga saumu za sunna mchana, kujiweka mbali na raha. Kwa hivyo makusudi ni kuwa wao walikuwa wanaishi maisha ya kujinyima kwa ajili ya Mungu (swt).