read

98 - Na Miongoni Mwa Maneno Yake (A.S)

Na Miongoni Mwa Maneno Yake (a.s) - Ibn Qutaybah ameeleza katika al-Imama was-Siyasah, jalada la kwanza, uk. 151.

Kuhusu Dhulma Ya Bani Umayyah

“Wallahi wataendelea hivi (Ufafanuzi: Usemi hapa ukadiriwe hivi: Wangali bado ni madhalimu) mpaka wafikie kiasi cha kuwa hawatoacha alichokiharamisha Mungu ila watakihalalisha, wala ahadi ila wataitangua na hata haitobakia nyumba ya matofali wala ya manyoya ila dhulma yao itaingia, na ubaya wa matendo yao utawafanya duni.

Mpaka watakuja kusi-mama waliaji wawili walie: Mliaji analia kwa ajili ya dini yake, na mliaji alia kwa ajili ya dunia yake, mpaka iwe nusura ya mmoja wenu kwa mwingine mfano wa nusura ya mtumwa kwa bwana wake, akiwa yupo anamtii, na anapoghibu humsengenya.

Mpaka itakuwa mwenye shida kubwa mno kati yenu ni yule mwenye kuwa na dhana njema mno kwa Mungu miongoni mwenu.

Mungu akikutunukieni amani na salama ikubali- ni, na akikupeni mtihani vuteni subira, “..... Na kwa hakika mwisho mwema ni wa wachamungu.”(7:128)