read

99 - Miongoni Mwa Khutba Zake (A. S)

Miongoni Mwa Khutba Zake (a. s) - an-Nuuriy ameieleza katika al-Mustadrak Jz. 1, uk. 411, na as-Saduq katika Man la Yahdhurul-Faqih, Jz. 1, uk. 270.

Katika Kujiepusha Na Dunia

“Tunamhimidi kwa yaliyotokea, na tunamuomba msaada kwa ajili ya mambo yetu yatakayokuwa, tunamuomba usalama katika dini, kama tunavyomuomba usalama kuihusu miili.1

“Nakuusieni kujiweka mbali na dunia hii ambayo ni yenye kukuacheni japo muwe hampendi kuiacha, na ni yenye kuichakaza miili yenu japo mupende kuifanya upya. Kwa kuwa mfano wake na ninyi ni kama wasafiri,2 wamesafiri waliokwenda kiasi fulani cha masafa kisha wakawa kana kwamba wao haraka wameikata safari, wameikusudia alama, na mara moja kana kwamba wameifikia. Ukaribu ulioje wa masafa kwenye lengo endapo mtu atalielekea na kulifikia! Ukaribu wa masafa ulioje wa kwenye lengo ikiwa mtu yualielekea na kulifikia!
Hatua fupi ilioje ya mtu aliye na siku moja tu ambayo hawezi kuizidisha, hali ikiwa amtakaye mwenye haraka yaani mauti amfuata, anasumbua duniani mpaka aitoke apende asipende! Hivyo basi msihusudiane kugombania utukufu wa dunia na fahari yake, na wala msifurahiye mapambo na neema zake, na wala msiyahuzunikie madhara yake na shida ya madhara yake.

“Kwa hakika utukufu wake na fahari yake vinaelekea kukatika, mapambo yake na neema zake vitatoweka, madhara yake na shida zake zinakwisha, na kila muda humo waelekea mwisho, na kila aliye hai humo aelekea mwisho.

Je ninyi kutokana na athari za waliokuwa mwanzo hamuonyeki! Na katika babu zenu wa mwanzo kuna ufunguzi wa macho na zingatio, endapo mtakuwa mnatia akilini! Je hamuoni kuwa waliopita miongoni mwenu hawarejei, na walioendelea kuishi hawatobaki milele! Si mwaona wana wadunia wanaingiwa na jioni na wanaingiwa na asubuhi wakiwa katika hali nyingi mtawanyiko: Kuna aliyekwisha kuwa mauti analiliwa, na mwingine ahaniwa, na aliyetupika chini amekumbwa na balaa, na mwenye kumtembelea mgonjwa, na mwingine anatapia nafsi yake, na ambaye aitafuta dunia na mauti yamtafuta yeye, na kuna aliyeghafilika wala haghafilikiwi, na katika athari za waliopita hupita waliobakia! Lo! Mkumbukeni mbomoa raha, na anayeyatia uchungu matamanio, na mkata matumaini, pindi yavamiwapo matendo mabaya, na muombeni msaada Allah (swt) ili kutekeleza wajibu wa haki Yake, na neema Zake na hisani Zake zisizo na idadi.”

  • 1. Amefanya vyema na kubuni (a.s) katika usemi wake huu, na hivyo ni kwa sababu dini au itikadi pia zina ugonjwa, tiba na kupona kama ambavyo miili ilivyo.
  • 2. Yaani wasafiri: Kwamba ninyi mpo katika masafa ya umri ni kama walivyo wasafiri katika masafa ya njia, hawabakii ila watafikia mwisho kwa kuwa (dunia) ina kikomo.