read

Kiyama

“Mpaka Kitabu kifikie muda wake, na amri makadirio yake, na kukutan- ishwa viumbe wa mwisho na wa mwanzo, na itakuja amri ya Mungu apendavyo katika kuwafanya upya viumbe Wake, ataiyumbisha mbingu na kuichana, na ataitikisa ardhi na kuitetemesha, na kuin’goa milima yake na kuivunja vunja, na kwa haiba ya utukufu Wake itagongana yenyewe kwa yenyewe, na kwa hofu ya ukali wake, na atawatoa nje walio ndani yake (ya makaburi), na atawafanya upya baada ya kwisha kwao (kuchakaa kwao).

Na kuwakusanya baada ya kutawanyika kwao, kisha atawapambanua1kwa ajili ya kutaka kuwauliza kuhusu amali zilizojficha, na matendo yaliyofichikana, na amewafanya makundi mawili: Hili moja alineemesha na hili la pili analiadhibu.

Ama watiifu atawalipa thawabu ya kuwa karibu Yake, na kuwafanya wa kudumu ndani ya nyumba yake, kiasi kwamba wafikao humo hawatotoka, wala hali haitowabadilisha, wala hawatofikiwa na hofu, wala hawatopatwa na magonjwa, wala hawatopatwa na hatari, wala kusumbuliwa na safari kwa kuwatowa sehemu hadi nyingine.

Ama watenda maasi atawakaribisha kwenye nyumba ya shari mno, na kuwafunga mikono shingoni, na kuzifunga nywele za utosi na nyayo za miguu, na kuwavisha kanzu za lami na vazi la moto, watakuwa katika adhabu ya moto uliokolea, na mlango uliowagubika wahusika wake, katika moto wenye ukali na sauti, na mwale umulikao, na wenye ukelele wa nguvu na wa kutisha, wakaao humo hawatoki, mateka wake hawakom- bolewi kwa fidia, pingu zake hazikatwi. Ile nyumba haina muda kiasi cha kuwa muda ukifika itakwisha, wala muda uliopangwa kwa wale watu hata ufikie mwisho.”

Sehemu Ya Khutba Imuelezayo Nabii (S.A.W.W.)

“Aliidharau dunia na kuiona duni na kuidogesha, aliona dunia haina thamani na akaidharau, na alijua kuwa Mungu (swt) amemuepusha nayo kwa hiyari yake (s.a.w.w.) na ameikunjua kwa wengine ili kuwadharau. Hivyo basi alijiepusha nayo kwa moyo wake, na kufisha utajo wake katika nafsi yake, na alipenda mapambo yake yatoweke mbali na macho yake, ili asichukue kutoka humo vazi la fakhari, au awe anatarajia humo nafasi, amefikisha kwa niaba ya Mola wake Mlezi akitoa udhuru,2 na alitoa nasaha kwa umma wake akionya, na alilingania pepo akibashiri, na alihofisha moto kwa kuhadharisha.”

Ahlul-Bayt

“Sisi ni mti wa unabii, na mashukio ya risala, na mapishano ya malaika,3 na chimbuko la elimu,4 na chemchemu za hukumu, mwenye kutunusuru na kutupenda atakuwa anangoja rehema, na adui yetu mwenye kutuchukia anangojea adhabu.5

  • 1. Atawapambanua: Yaani atawatenga na kuwafanya makundi mawili: 1. Wenye furaha na 2. Wenye shida.
  • 2. Yaani mfikisha hoja itakayochukua nafasi ya udhuru katika kuwaadhibu endapo watakhalifu amri yake.
  • 3. Yaani ni mahali pa kupishana kwa maana ya: Akiingia huyu miongoni mwao huyu mwingine anatoka, kwa hiyo anakuwa huyu wa pili kama ni khalifa wa yule wa kwanza, wanapokezana.
  • 4. Kauli yake; ‘na chimbuko la elimu’: Anakusudia hekima au hukumu ya kisharia. Amesema Mtume wa Mungu (s.a.w.w.):”Mimi ni jiji la elimu na Ali ni mlango wake, hivyo basi autakaye mji huo na auendee mlango.”
  • 5. Kwa sababu adhabu itawafika kwa yakini kabisa, wamekuwa kama wanaoingojea, na pia wao wanatazamia mauti, ambayo ni utangulizi wa adhabu, ndio maana amejaalia kuun- gojea kwake ni kungojea litakalofuata baada ya mauti (nalo ni adhabu).