read

13. Utiifu Kwa Misingi Ya Mapenzi

Itatubidi lazima tukumbuke kuwa sheria iliyo ya uchokozi na udhalimu, kamwe haiwezi kuwa sahihi. Hivyo misingi ya mamlaka ya bwana yamewekwa kwa mapenzi na wala sio kwa vitisho na uonevu. Allah swt anatuambia katika Quranii Tukufu sura Ar-Rum 30:21

"..... naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu..."

Katika Aya hii tunaona maneno mawili, ‘mapenzi’ na ‘huruma’ yametumika katika mapenzi ya unyumba. Kwa kawaida mwanamke tukiongelea ukweli anampenda bwana wake zaidi mno. Yeye yuko tayari kujitolea nafsi yake na mwili wake kwa ajili ya mume wake. Hivyo ‘mapenzi’ ndivyo yanavyo tuelezea hali hiyo.

Kwa upande mwingine mapenzi ya mwanamme kwa mke wake yana sura tofauti kimaumbile - hapo hakuna swala la kujitolea. Na hivyo ndivyo ‘huruma’ inavyotumika.

Vyovyote vile mapenzi, utiifu na huruma ndio mambo ya kutimiza katika maisha ya mwanadamu: Kuzatiti mambo ya nyumbani na uzazi.