read

14. Adabu Za Kusuhubiana

1.Mtume s.a.w.w. amesema: "Msisuhubiane na wake zenu kama kuku. Fanyeni mapenzi ya kutosha mubusu na hatimaye munapojawa na raha ndipo musuhubiane”.

2.Watu wengi wanachukulia mambo ya kishetani katika kusuhubiana huku wakipuuza njia aliyoihalalisha Allah swt. Wao wanaingilia njia ya nyuma i.e. panapopitia choo kwa kisingizio cha kupata raha zaidi kumbe kunakujitumbukiza katika hatari ya kuweza kuambukizwa magonjwa hatari kabisa kwa sababu hiyo ni nafasi ya kupitia uchafu mtupu uliojaa magonjwa ya kila aina. Kwa msomaji ni ushauri wangu kuwa aonane na mganga ili aweze kupata ukweli na uhakika wa swala hili ili aweze kuelewa vyema falsafa ya Islam katika swala hili.

3.Manukato ya maua na mafuta mazuri yanaweza kuwafanya kustarehe zaidi katika kusuhubiana.

4.Kwa kubaki mbali na mke kwa kipindi kirefu bila ya kusuhubiana naye au kwa udhuru mwingine wa kisheria haifai kumtukana au kumuudhi kwani kunaweza kwa urahisi kumfanya mke aende nje kwa waume wengine na hapa bwana ndiye atakaye wajibika.

5.Wataalamu wanasema kuwa bibi na bwana wanaposuhubiana,inawabidi wasiingiliane tena illa baada ya siku tatu au hata zaidi. Ingawaje hakuna ushahidi wa kuleta madhara.

6. Haifai kusuhubiana wakati tumbo likiwa limejaa (ameshiba) au likiwa tupu (njaa) bali baada ya kula iwapo utakuwa umepita muda wakutosha, basi hakuna madhara.

7. Baada ya kusuhubiana kwa bibi na bwana,wasioshe sehemu zao za siri kwa maji baridi wala wasioge kwa maji baridi kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kuwaingiza katika magonjwa mengi mno na kuna uwezekano mkubwa wa mishipa kulegea.Lakini kusafisha kwa kitambaa chenye maji si vibaya.Bibi na bwana hawatakiwi kusafisha sehemu zao za siri kwa kutumia kitambaa kimoja tu kwani kunapunguza mapenzi baina yao.

8.Baada ya kusuhubiana wote wawili wanashauriwa kujisaidia haja ndogo (kukojoa mkojo) na kwa kufanya hivyo mishipa haitalegea.

9.Kusuhubiana kwa kijana mwenye umri mdogo na mwanamke mwenye umri mkubwa ni hatari sana kwa siha ya mwanamme kwani ni sawa na sumu kali sana.

10.Umri wa mwanamke: kuanzia miaka kumi na miwili hadi ishirini ni kama bibi harusi na katika umri huu anaweza kutoa uridhisho mzuri kabisa katika kusuhubiana.Vile vile kuanzia umri wa miaka ishirini hadi thelathini anaweza kutoa uridhiano mzuri na bwana pia anaweza kuridhika. Na mwanamke kuanzia thelathini hadi arobaini si mbaya. Kuanzia arobaini hadi hamsini huwa hisia zimekuwa sugu, hata hivyo hana madhara.

11.Mtume s.a.w.w. alimwambia Imam Ali a.s. "Ewe Ali! Unapomleta mke wako nyumbani mwako, ondoa viatu vyake ili aweze kuketi vyema na uoshe vikanyagio vya miguu yake na kumwagilia maji hayo mlangoni na kona zote na kuta za nje ya ya nyumba; kwa kufanya hivyo kutaondoa mawazo na shida sabini elfu na kutakuletea baraka na rehema sabini elfu za Allah swt. Na vile vile kila kona ya nyumba itakuwa imebarikiwa na bibi harusi atakuwa amehifadhika na ugonjwa wa kichaa, kubabuka ngozi kichwani na ukoma. Usimpatie kwa siku saba za kwanza maziwa, siki, giligilani na tufaha chachu". Alipouliza Imam Ali a.s. sababu yake, alijibiwa: "kwa kula vitu hivyo, mfuko wa uzazi ya mwanamke inapoa na inapoteza nguvu za kushika mimba na hawezi kuzaa mtoto..."