read

15. Uzazi

Uendelezaji wa binadamu na asili ya kuwapo kwake na kwa ujumla ni wajibu wa kila aina, vyote viko pamoja na mwanamke. Kwa hakika mwanamke amebarikiwa jambo hilo, yeye anatimiza wajibu wake kwa binadamu kwa ujumla.

Uislamu haujapitiwa (hauja acha kujaali) vile mwanamke anavyobeba mzigo huu na maswala kama hayo katika jambo hili. Uislamu umemuahidi thawabu kubwa kabisa na rehema na baraka za kila aina katika jambo hili gumu mno. Mwanamke inambidi apitie hatua nne katika swala hili, kwanza kushika mimba; pili kuzaa; tatu kunyonyesha na nne uleaji malezi bora ya watoto.

Mwanamke anapata thawabu za kudumu katika kila hatua hizi, na kwa mujibu wa Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:

Hatua ya kwanza:
"Wakati mwanamke anaposhika mimba, katika kipindi hicho ni sawa na yule anayefunga saumu daima, anayesali na anayepigana Jihad kwa nafsi na kwa mali yake katika njia ya Allah swt."

Hatua ya pili:
"Wakati mwanamke anapozaa, anapata thawabu kupita kiasi kwamba hatuwezi kuzielezea kwa sababu ya tendo hili jema."

Hatua ya tatu:
"Wakati mwanamke anapomnyonyesha mtoto wake maziwa, Allah swt anamjalia thawabu sawa na kumfanya huru mtumwa (kutoka kizazi cha Mtume Ismail a.s. ) kwa kila mara anaponyonyesha."

Hatua ya nne:
"Uleaji wa watoto - swala hili linazungumziwa zaidi katika maswala ya haki za watoto."

Taarifa ifuatayo kutoka Hadithi tukufu lazima isomwe kwa uangalifu sana: "Mtume Mtukufu s.a.w.w. alimwambia binti yake, Bi. Fatima a.s.:-

"Ewe Fatima mwanamke asimletee chochote kile mbele ya bwana wake asichokipenda; daima awe mtunzi muhifadhi wake; lazima awe mkweli na mtiifu mbele na anapokuwa hayupo; aukate (ukali na majeraha) ya ulimi wake (dhidi ya bwana wake); amtazame vyema pale anapohitajika bwana wake kutazamwa na kutunzwa; amtimizie mahitaji yake yote na daima aangalie ahali yake; kwa sababu kumtazama bwana wake ni ibada; na kamwe asimkaribishe mtu katika chakula isipokuwa ameruhusiwa na bwana wake; na daima mwanamke awe akiridhika na kile alichojaaliwa na Allah swt; na kamwe asimwache bwana wake, na kama atamwachia, basi sala zake, saum na zaka hazitakubaliwa na Allah swt hadi hapo bwana wake atakapokuwa amemridhia."