read

16. Haki Za Mke

Qurani Tukufu inafafanua misemo ya kuwazulia Waislamu juu ya utumwa wa wanawake katika Islam, swala ambalo wanamagharibi waliomajahili ndio wanaotumia kama silaha dhidi ya Waislamu. Ilikuwa ni dharura katika kuimarisha na kudhibiti hali bora ya nyumbani ili kumzatiti mwanamme katika mamlaka sawa sawa juu ya wanawake. Na Aya hiyo ya Qurani ndivyo inavyofanyia ishara juu yake. Mbali na haya sehemu zote mbili yaani bibi na bwana wamepewa haki zilizo sawia. Kila sehemu wamepata nusu sawa sawa.

Kama iliyoelezwa hapo awali kwa mujibu wa akili na kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, mwanamme ndiye anayewajibika kwa ajili ya kumgharimia na kumtafutia mahitaji yote ya mke wake, na katika mtazamo huu wa uwajibikaji ambao upo katika mapenzi.

Inaonekana kutoka juu kuwa chochote kile anachotaka mwanamke kwa ajili ya utulivu wa akili yake kuwa bora kiroho, na kuridhika na mahitajio yake, vinaweza kutenganishwa katika makundi mawili:

1. Mapenzi halisi

2. Kutizamwa vyema

Lau mtu atakaa kupitia orodha ya madai ya wale wenye kutetea ukombozi wa wanawake, basi utagundua kuwa haki hizo zote ambazo zinakubaliana kiakili utaona yako katika makundi haya mawili.

Islam imewaamrisha kwa kuwasisitiza wanaume kuwapa uhuru wake zao kufurahi haki zao bila ya kubugudhiwa vyovyote vile. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:

"Mwanamke yeyote atakayembughudhi mume wake kwa ulimi wake....atakuwa ni wa kwanza kuingizwa Jahannam. Na, vivyo hivyo, iwapo bwana wake hatamfanyia haki."

Mapenzi na baraka

Imam Ja’afer Sadiq a.s. amesema:
"Mimi nina uhakika kuwa mtu anapokuwa bora zaidi katika imani na Islam basi vivyo hivyo mapenzi ya wake zake inavyozidi.

Aya isemayo: Allah swt ameweka mapenzi na huruma baina yenu, inaonyesha kuwa mapenzi ya kindoa ni baraka za Allah swt; na vile mtu atakavyokuwa na imani zaidi katika Allah swt, ndivyo vivyo rehema na baraka zaidi za Allah swt zitakuwa juu ya jozi hiyo (yaani bibi na bwana ).

Na kwa sababu hii Imam Ja’afer Sadiq a.s. amesema:”Miongoni mwa desturi za Mitume ni mapenzi ya wanawake."

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema, "Ijulikane mtu bora miongoni mwenu ni yule ambaye ni bora kwa wake zake na mimi ni bora kwa wake zangu."

Vivyo hivyo ameendelea kusema: "Rehema na baraka za Allah swt ziwe juu ya mtumwa wake ambaye anawafanyia wema baina yake na mke wake kwa hakika, Allah swt amempa mamlaka zaidi juu ya mke wake na kwamba amemfanya awe ni mtu mwenye kumhifadhi mke wake."

Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, imesisitizwa kuwa mwanamme anapokuja nyumbani aje na uso wenye bashasha, mchangamfu. Nyumba hiyo itakuwa ni Jannah iwapo sheria kama hizi zitafuatwa kwa makini.

Haki za kutimiza

Katika aya za Qurani, Allah swt anawaambia wanaume kuwatendea wema wake zao. Mbali na aya hiyo ya hapo juu ipo aya nyingine inayosema: sura An-Nisaa, 4: 19 "...Na kaeni nao kwa wema ..."

Kuwatendea wema kwa mujibu wa Hadithi inamaanisha kuwa kile ambacho atapatiwa mwanamke, kwa kiasi kinachowezekana, hali na desturi alivyokuwa akiishi katika majumba ya wazazi wake; ili kwamba asipate kukabiliana na hali ya kutoishi kwa raha na vile vile asipate ugumu wa kupata magonjwa ya akili kwa sababu ya kukosa raha katika majumba ya mabwana zao.

Na iwapo bwana, kwa sababu za uchumi wake kuwa kiasi,anashindwa kumpatia hali hiyo bora basi hawezi kulaumiwa.

Qurani Tukufu inatuambia katika sura Al-Baqarah 2: 236

"... Mwenye wasa’a kadiri awezavyo,na mwenye dhiki kadiri awezavyo..."

Imam Ja’afer Sadiq a.s. anatuambia: "Wale wote wanaomtegemea bwana ni wafungwa wake, na mtumwa wa Allah swt aliyebora kuliko wote mbele ya macho ya Allah swt ni yule ambaye anawatendea wema wafungwa wake."

Vivyo hivyo Imam Musa al-Kadhim a.s amesema: "Wale wote wanaomtegemea mwanamme ni watumwa wake. Kwa hivyo iwapo Allah swt anamjalia baraka zake mtu yeyote, basi itambidi na yeye aitumie zaidi kwa ajili ya wafungwa wake; na lau hatafanya hivyo, basi neema na baraka hiyo itatoweka”.

Kwa mujibu wa Shariah za Kiislamu, malipo, matumizi au posho ya mwanamke ni malipo ya utiifu wake. Iwapo huyu mwanamke hamkatalii mume wake haki zake, basi ana haki zake zote za kuruzukiwa. Iwapo bwana, kwa sababu ya matatizo yake ya kiuchumi, anashindwa kumtimizia posho na ruzuku za mke wake, basi atabakia na deni hilo akidaiwa na mke wake; na hivyo itambidi kumlipa mara moja pale apatapo mapesa n.k. Kwa kifupi kumtimizia mwanamke haja zake ni juu ya misingi nipe na nikupe, na mwanamme itambidi alipe kwa hali yoyote ile. Imam Ja’afer Sadiq a.s. amesema: "Amelaaniwa yule mwanamme ambaye hawajali wale wanaomtegemea."