read

18. Kutokuelewana Na Magomvi

Uislamu unatambua waziwazi kuwa hii njia ya kubuni mambo tu haisaidii kuwa mema. Isipokuwa kanuni zinazotumika na desturi miongoni mwa bibi na bwana ndizo zinazoleta amani katika nyumba.Hotuba kubwa kubwa hazitamsaidia mtu wa kawaida iwapo hayatakuwa kwa mujibu wa akili na vile vile lau hazitakuwa katika uwezo wake.

Ndoa bora za Kiislamu ni zile ambazo bibi na bwana wanapendana na wanaheshimiana na kila mmoja kuheshimu haki za mwenzake.

Lakini dunia hii haipo ya watu wachamungu na wenye kufahamu tu bali imejaa zaidi kwa watu wenye mioyo migumu na wanawake wa aina hizo; wao hawajali uharibifu wanaouleta katika jamii ya Kiislamu kwa sababu ya matendo yao na kuchezea maamrisho ya Shariah za Kiislamu. Hivyo ilikuwa ni lazima kutengenezwa Shariah ili kurekebisha desturi zao.

Kwa nini ugomvi

Chanzo kikuu cha magomvi ni kupuuzia kwa wajibu wa mtu mmoja kwa ajili ya mwenzake. Dharau hiyo inawezekana ni upande wa bwana au upande wa mke, au pande zote mbili. Islam kwa kuzingatia maswala nyeti kama hayo imeweka Shariah kwa kila hali itakavyotokezea.

Wakati mke anapokuwa na hatia

Iwapo mke ataacha wajibu wake na kumsumbua bwana wake, basi Allah swt anaelezea laana za aina tatu kwa ajili yake, katika sura An-Nisaa 4: 34

"... Na wanawake ambao mnaona uasi wao kwenu waonyeni na waacheni peke yao katika vitanda na wapigeni"

Hatua ya kwanza:
"Itambidi kwanza bwana ajaribu kumuelimisha mke wake na kumshauri abadilishe desturi ya tabia zake. Mwanzoni nasiha na majadiliano baina yao inaweza kuleta matunda mazuri,wakati ambapo hatua kali zikichukuliwa zinaweza kuleta mwelekeo ulio mgumu zaidi."

Hatua ya pili:
"Iwapo hilo litashindikana, inamaanisha kuwa ugonjwa huo umechukua mizizi ndani zaidi. Hivyo itambidi bwana amwache mwanamke huyo kitandani mwake. Inawezekana mgomo huu baridi ukamrudishia mwanamke huyo akili zake; na akajirudia na ugomvi ukaisha."

Hatua ya tatu:
"Lakini, iwapo upuuzaji wake huo umezidi, na mawaidha, nasiha na mgomo wako huo haukumuathiri, basi matibabu madogo hayawezi kuwa na faida yoyote. Katika hali ya kuzidi kabisa kama hii, bwana ana ruhusa ya kumpiga mke wake. Kuna msemo usemao iwapo hatua nzuri zitashindwa kuamsha hisia nzuri za mwanamke, kinachobakia ni kumwijia kwa mabavu."

Lakini kumwijia kwa mabavu huko lazima kuwe ni kwenye hali nzuri na nidhamu bora. Imam Muhammad Baqir a.s. amesema:

"Kwa hakika, mjeledi kwa mswaki wa meno. Shariah inasema kuwa isiwe unampiga ngumi kiasi cha kuvunja mfupa au kuacha doa jekundu au michubuko, na kamwe mwanamme haruhusiwi kumpiga usoni mwanamke, na wala mahala pamoja kupigwa mara nyingi."

Iwapo matibabu haya yataondoa sababu za ugomvi, basi inambidi mwanamme (bwana) amwache kwa wema na atimize haki zake zote kwa mara moja. Lau katika hali hii ya ugomvi na kujaribu kumrudisha mke katika hali yake akaomba msamaha na akatubu kosa lake basi inambidi mwanamme na hasira zake na ugomvi uishie pale pale, na mrudishie haki zote za mwanamke anazostahili yaani mapenzi, haki na mambo mengine yote kama tulivyokwisha kuelezwa hapo nyuma. Sentensi ya mwisho ya Aya ya hapo juu inatuambia hivi: ( baadaye, wanaporudi katika utiifu, basi usiwatendee tena hasira).

"... Na kama wanakutiini msiwatafutie njia ( ya kuwaudhi bure)."

Wakati mwanamme anapokuwa katika hatia

Na iwapo kwa upande mwingine bwana ndiye yuko katika makosa na amepuuzia wajibu wake kwa mke wake, basi mwanamke itambidi kwanza ajaribu kuleta uelewano baina yao.

Allah swt anatuambia katika Qurani tukufu katika sura An-Nisaa 4:128

"... Na kama mke akiona kwa mume wake kugombanagombana na kutenganatengana, basi si vibaya kwao wakitengeneze baina yao sulhu...."

Na iwapo njia hii haitawezekana kuleta matunda mazuri basi mwanamke ana haki ya kuchukua mashitaka yake mbele ya Hakim-i-Shariah (kadhi au mujtahid ) ambaye ana mamlaka ya kila aina katika usuluhishi wa mfarakano kwa mujibu wa Shariah na maadili.

Bibi na bwana wanapokuwa na hatia

Iwapo bibi na bwana watapuuzia haki zao, basi hapo kwa kweli kuna haja ya msaada wa mtu mwingine ili kumaliza mzozo wao. Hivyo Allah swt ametuamrisha katika Qurani tukufu sura An-Nisaa 4:35

"... Na kama mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume basi pelekeni, mwamuzi mmoja katika jamaa za mwanamme, mmoja katika jamaa za mwanamke."

Uadilifu na maamuzi kama haya yanaweza kufikiwa katika hali mbili zilizotangulia pia, wakati mmoja tu anapokuwa katika hatia.