read

19. Mambo Muhimu Ya Kuzingatia

1. Si haramu kusuhubiana na mke anapokuwa na mimba lakini iwapo kutakuwa na hatari kwake yeye au mtoto aliye tumboni, basi katika hali hii itakuwa ni haraam kusuhubiana. Hata hivyo wataalamu wanapinga kusuhubiana wakati mwanamke anapokuwa na mimba.

2. Wazee waliwauliza Maulamaa iwapo watoto watazaliwa vile yalivyoelezwa hapo awali, lakini walijibu kuwa hayo yote yapo mikononi mwa Allah swt.

3. Maelezo yote yalivyoelezwa kama ni makruh (karaha) basi yachukuliwe ni karaha na kama yameelezwa kuwa ni haramu basi yachukuliwe vile vile ilivyo hukumu za haramu. Ni mwiko kubadilisha haram kuwa makruh!

4. Iwapo mwanamke alikuwa katika hali ya janaba na hakuwahi kuoga ghusl-i-janaba na akaingia katika haidh, au baada ya kutoka haidh lakini kabla ya kufanya ghusli Haidh akaingia janaba (akatakiwa kufanya ghusli janaba) yaani anatakiwa kufanya ghusli zote mbili: Janaba na Haidh. Katika swala hili hatakiwi kufanya ghusli mbili mbalimbali isipokuwa atafanya nia moja tu ambayo itafaa kwa ghusli zote mbili.

5. Kutoa manii kwa mkono ni haraam na vile vile madaktari pia wanapinga mno kwani kunadhoofisha uwezo wa mtu na hatimaye kupoteza nguvu za kiume.

6. Kuingilia kwa njia ya nyuma ni haramu na ni yenye madhara makubwa sana.

7. Kutalazimika kufanya ghusl-i-janaba iwapo kutatokwa na manii kwa njia yoyote ile ya kutumia mkono, kusuhubiana au kuingilia kwa sehemu ya nyuma au katika usingizi.

8. Iwapo mtu ataota ndoto ya kusuhubiana na mwanamke lakini hakutokwa na manii, basi halazimiki kufanya ghusl-i-janaba.

9. Ni lazima kusuhubiana mara moja katika miezi minne lakini ni sharti kuwa kusiwepo na udhri wowote wa kisheria wala asiwe amekwenda safarini.

10. Ni swala mashuhuri miongoni mwa Maulamaa kuwa usiku saba ni makhsusi kwa ajili ya mwanamke aliyeolewa bikira na usiku tatu kwa mwanamke asiye bikira.

11. Ni hukumu kwa ajili ya wanaume kutoziweka nywele za sehemu zao za siri kwa zaidi ya siku arobaini (na wazikate kabla ya siku hizo) na wanawake wasiziweke zaidi ya siku ishirini (na wazikate kabla ya siku hizo). Ipo riwaya ya Imam Ja’afer Sadiq a.s. isemayo: "Msiziweke nywele zenu za sehemu zenu za mwili zinazotakiwa kukatwa i.e.mashurubu, kwapani na sehemu za siri na muziondoe kwa kutumia nurah.

12. Kuna faida mno kusuhubiana na mwanamke ambaye ametoka katika haidh na ameoga ghusl-i-haidh.

13. Wapinzani wa swala hilo juu wanasema ni vyema kujiepusha na mwanamke ambaye ametoka haidh kwa siku kumi ambavyo hatapata udhaifu na siku ishirini zilizobakia ni nzuri ambamo siku kumi za katikati ndizo nzuri mno.

14. Imeruhusiwa kumwoa msichana mdogo, lakini iwapo hatakuwa ametimiza umri wa miaka tisa au kuzidi basi ni haraam kusuhubiana naye.

15. Iwapo mwanamme atamwoa msichana asiyefikia au kutimiza umri wa miaka tisa na akasuhubiana naye basi atambue kuwa ametenda tendo la dhambi na iwapo amemjeruhi katika sehemu zake za siri yaani iwapo sehemu ya kike kuungana na sehemu ya haja ndogo au sehemu ya kike kuungana na sehemu ya choo (njia ya nyuma) basi atambue kuwa huyo mwanamke atakuwa haraam kwake yeye kwa umri mzima. Lakini Maulamaa wanasema kuwa nikah (ndoa) haivunjiki kwa hivyo kamwe hataweza kusuhubiana naye kwani atakuwa haraam kwake kusuhubiana naye. Na iwapo hali kama hiyo itatokea kwa mke wake ambaye amekwisha timiza umri wa miaka tisa au zaidi basi hatakuwa haraam kusuhubiana naye.

16. Mtu hawezi kumwoa dada wa mke wake aliye bado hai na iwapo atathubutu kufanya hivyo (yaani kuwaoa dada wawili wakiwa ni wake zake wawili) basi ni dhambi na nikah hiyo itakuwa batil na watoto watakaozaliwa watakuwa ni waladuz-zinaa.

17. Iwapo mwanamme atasuhubiana na mwanamke aliye na bwana ambaye yu hai au mwanamke ambaye hakumaliza kipindi chake cha Iddah basi kamwe hataweza kumwoa huyo mwanamke mbeleni.

18.Iwapo mtu alisuhubiana na mwanamke asiye na bwana (ingawaje ni dhambi la zinaa aliyojipatia) lakini iwapo atataka kumwoa,basi anaweza.

19.Iwapo mwanamke (mwenye bwana) atafanya zinaa na bwana mwingine nje ya ndoa yake au mwanamme (mwenye mke) atafanya zinaa na mwanamke mwingine nje ya ndoa yake basi wote wanakabiliwa na adhabau ya kukalishwa shimoni na kupigwa mawe hadi kufa. Na iwapo ni mwanamke asiye na bwana au mwanamme asiye na mke basi watachapwa viboko mia moja.
20.Iwapo ni mwanamke aliyepewa talaqa basi hakuna mtu atakayeruhusiwa kumwoa kabla hajamaliza kipindi chake cha Iddah na iwapo mtu yeyote atathubutu kufanya hivyo, basi mwenye kuoa, kuolewa na wote walioshiriki katika kufanikisha hivyo wanalaaniwa na Allah swt na wanajitafutia adhabu zake. Na iwapo watasuhubiana basi hiyo ni zinaa na mtoto akizaliwa atakuwa waladuz-zinaa na atambue waziwazi kuwa kamwe hawezi kumwoa hata kama atataka hivyo.

21.Iwapo mwanamme atafanya tendo la kubaka (atamwingilia kwa nguvu) mwanamke basi atambue waziwazi kuwa kamwe hawezi kumwoa (aliyebaka) huyo mwanamke wala hawezi kumwoa mama,dada na binti yake.

22.Mwanamme atakaye kuwa amempa mke wake talaqa tisa kwa mujibu wa Shariah, basi atakuwa haraam kwake daima.

23.Iwapo mwanamme atakuwa amesuhubiana na wifi au shanghazi yake, basi hawezi kuwaoa mabinti wao (watoto wa shanghazi na watoto wa wifi) .

24.Iwapo kutakuwa na mume ambaye ameishi na mwanamke kwa kipindi cha miaka thelathini au hamsini au hata zaidi ya hayo lakini kwa ndoa ya muda (muta') na atakapokufa mmoja wao basi hakuna atakayemrithi mwenzake.

25.Haki ya urithi wa kutoka mali ya baba kwa ajili ya watoto itakuwa sawa kabisa kwa mujibu wa Shariah za Dini iwapo watakuwa wamezaliwa na mama aliyeolewa kwa ndoa kamili au ndoa ya muda au amezaliwa na kijakazi wa baba yake.

26.Iwapo mwanamme atampa mke wake talaqa, basi itabidi ishuhudiwe na waadilifu wawili ndipo hapo sigha hiyo itakaposomwa na nikah ya mwanamke haivunjiki hapo hadi mwanamke huyo kutimiza kipindi cha Iddah yake (ndipo hapo atakapokuwa huru kuolewa) na iwapo ataolewa kabla ya kutimiza Iddah, basi ndoa hiyo itakuwa haraam na iwapo watasuhubiana basi hilo ni tendo la zinaa. Hata hivyo siku hizi kuna mtindo wa kupeana talaqa za haraka haraka ilimradi mmojawapo anataka kuoa mwingine basi atafanya kila aina ya hila ya kujifanyia njia sahili ili mradi afanikiwe katika adhma yake lakini ikumbukwe wazi kuwa iwapo Shariah za dini ya Islam kama hazikufuatwa na kutimizwa basi mambo yote yatakuwa ni haraam. Kutoa na kupewa talaqa kuna masharti maalum na yenye msimamo na mipangilio yake.

27.Iwapo bibi na bwana walikuwa mushrik na wote kwa pamoja wakawa Waislaam, basi ndoa yao itahala­lika na kuwa ya daima; lakini iwapo mmoja wao atakuwa Mwislaam na baada ya kupita kipindi cha Iddah hawi Mwislaam basi nikah inavunjika na haitawezekana kamwe hadi awe Mwislam.

28.Iwapo bwana atakuwa Mumini na mke akiwa mushrik na iwapo mke hatabadilisha imani yake (akawa Mwislam) basi itakuwa ni swala kama la hapo juu kwani huyo bibi hatakuwa mke halali wala bwana hatakuwa halali kishariah. Kwa kifupi wote wanakuwa wametoka katika nikah.

29. Iwapo mke atakuwa Mumini na bwana atakuwa mushrik, basi hukumu yake ni kama ilivyozungumzwa hapo juu katika na.28, yaani uhusiano wao unakuwa umevunjika kindoa.
30.Bwana Mushrik anapokubalia Islam na akawa Mwislaam lakini mke akabakia mushrik, na baada ya kupita kipindi mke akawa Mwislaam, basi katika hali kama hii kwa mujibu wa Shariah, ndoa yao ilikuwa imekwishavunjika (hawakuwa na ndoa) na bwana haelewi masuala haya na anamchukulia mke wake kama yu halaali kwake na siku atakapokuja kujua masuala haya kishariah basi itambidi afanye nikah haraka.

31.Watu wengi sana wanadai kuwa wao wamekuwa Waislaam lakini wake zao wanakataa kata kata kuwa Waislaam na ilhali wameshazaa nao watoto hivyo hawawezi kuwapa talaqa wake zao kwa sababu kama hizo na lawama na aibu kutoka kwa jamaa zao. Kwa hivyo "Mungu atatusamehe tu, sisi tufanyeje?".

Sisi tujiulize kuwa hapo kosa ni la nani na anayetakiwa kulaumiwa ni nani. Hivyo itawabidi wasiwachukulie wake kama hao kama ni wake zao na wala wasi suhubiane nao na hivyo tu ndivyo watakavyoweza kujiepusha na madhambi.

Sasa tuzungumzie swala la toharah kwani chakula anachokipika ni najis na nguo na vyombo anavyoviosha pia ni najis kwa hivyo ni haraam na sala zitakuwa batil hivyo itambidi kuchukua hatua za kujitoharisha kishariah na kuchukua hatua zote za tahadhari ili aweze kusali na kufunga saumu bila ya kuhatarisha amali zake za ibadah.

Iwapo hatafanya hivyo na kuishi na mke wake mushrik na vyote atakavyopatiwa na mke wake kwa ajili ya wudhuu, ghusli, sala na saumu basi vyote vitakuwa ni batil. Hivyo mwenye kujitakia hayo, itambidi atafute ufumbuzi wake. Ama sivyo matokeo yake yapo bayana.

Watu wengi wanasema "Je! mwenye kukubali matendo yetu ni Allah swt au ni Mashekhe wetu?" Kwa kweli huku ndiko kujidanganya nafsi zetu na kujihadaa kwani Shariah kuhusu sala,saumu na mengineyo ni ya Allah swt na wala si yetu hivyo ni kwa mujibu wa hayo tu, hakuna Shariah ya aina yoyote ile ambayo mtu anayo ruhusa kuibadilisha kwa mujibu wa matakwa yake. Je! ni Sheikh yupi ambaye anataka kujitumbukiza bure katika moto wa Jahannam kwa kumsingizia Allah swt, Mitume a.s. na Maimamu a.s? Hivyo sisi pia inatubidi kufanya utafiti zaidi juu ya masuala ya Dini kwani ni fardhi yetu kujua masuala yote ya Dini.

32.Ingawaje Islam imeruhusu kuoa wake wanne kwa wakati mmoja lakini imeweka Shariah kali mno ya kutimiza na kuhakikisha uadilifu miongoni mwao. Itambidi mtu atafiti zaidi juu ya masuala haya katika fiqhi.

33.Mke hawi haraam baada ya kumpatia talaqa, illa baada ya kupita kipindi cha Iddah. Iwapo mume atataka kumrejea mke wake kabla ya kipindi cha Iddah kuisha, na iwapo atakuwa na uhusiano wa mume na mke, basi talaqa itavunjika na hakuna haja ya kusoma nikah tena.

34.Iwapo mume atampa talaqa mke wake na baada ya kupita kipindi cha Iddah atataka kumrejea tena mke wake basi itambidi kusomewa nikah tena.

Si lazima kuwa mwanamke huyo aolewe na kusuhubiana na mwanamme mwingine na kupewa talaqa ndipo bwana wa kwanza aweze kumrejea.

35.Mwanamme hawezi kumpa talaqa ovyo mwanamke kwa sababu zisizo na msingi kishariah. Hivyo itambidi mtu kutafiti vyema masuala ya talaqa katika Shariah kwa pande zote mbili kwani kuna mambo mengi ya kuzingatia na kuyatekeleza yakiwemo pamoja na haki ya mke na watoto. Hivyo tusidhani kuwa tutakapomwambia mke "nimekupa talaqa" basi siyo kwamba amepata talaqa bado anakuwa amebakia katika nikah au kwa kupewa talaqa mahakamani, kwani haki zake zote bado zipo juu ya bwana wake.Shariah za Kiislamu ni Shariah halali hivyo Shariah za nje ya Islam hazitabadilisha msimamo wa Islam.