read

5. Uhakika Anaotakiwa Mume Kuzingatia

(a) Je! unajua na kutambua kuwa wewe umechukua kitu bora kabisa kilichoumbwa na Allah swt? Roho, maisha ya mwanamke na mapenzi ya kiajabu kabisa !.

(b) Tumewafaradhishia wanaume kuwafanyia wema wazazi wao. Mama yake alimhimili katika maumivu na kumzaa katika maumivu.

(c) Macho yoyote yanayomwangalia mwanamke kwa nia mbaya ni sawa na kufanya zinaa.

(d) Bora miongoni mwenu kuliko wote ni yule mtu ambaye ni mwenye huruma na mwenye ukarimu kwa familia yake, na mimi niko vivyo hivyo kwa familia yangu.....Mtume Mtukufu s.a.w.w.

(e) Wanawake wanaheshimiwa na wale watu tu ambao ni wanaume wenye huruma na wenye fahamu zao timamu na hakuna anayewakashifu na kuwatukana isipokuwa wale ambao ni waovu na wapotofu.

1. Mwanamke anahitaji kuhifadhiwa

Daima ukumbuke kuwa mwanamke ni mdhaifu kuliko mwanamme hivyo inabidi ahifadhiwe katika kila hali ya maisha na apewe yale anayoyahitaji. Mume bora ni yule ambaye anathamini mahitajio ya mke wake na iwapo mke wake atamuomba bwana wake kitu chochote basi bwana afikirie kuwa amepewa heshima hiyo ya kumpatia mke wake alichoombwa.

2. Muwajie kwa maongezi mema

Daima mfanye mke wako awe na hisia kuwa yeye ni mtu muhimu kabisa katika maisha yako na kamwe usiache kudhihirisha hivyo. Kwa kutoa lawama na kutumia lugha chafu na kuhamaki kila hapa na pale yaongezea katika uelewano mbaya baina ya bibi na bwana, na haisaidii chochote katika kuleta unyumba wenye raha na starehe.

3. Kupeana zawadi

Zawadi, lau ikiwa ndogo kiasi gani, atakayopewa mke kutoka kwa bwana wake kwa hakika itaongezea mapenzi na uvutano baina yao na kwa hakika hili jambo ndilo linaleta raha zaidi kimapenzi.

4. Umchukulie vyema

Mwanamke ni kiumbe kilicho nyororo na hivyo ndivyo inavyobidi kumchukulia. Kwa kumdharau au kutumia maneno maovu, kwa kumchukua vibaya kutasababisha uharibifu wa akili yake hapo mbeleni ingawaje kwa wakati huo haitajulikana hivyo.

Mwanamke ni kiumbe cha ajabu kwa hiyo kila utakavyomuwia vyema ndivyo atakavyokuwa na akili timamu siku za mbeleni na ukianza kuchafua akili zake, siku za mbeleni hiyo akili itaharibika na unyumba wako utaanza kuwa katika matatizo.

5. Usimtatanishe katika matendo yake

Usijaribu kumfaidi mwanamke kwa sababu ya udhaifu wake na maumbile yake. Kimaumbile mwanamke ni mama na daima anapenda kuhifadhiwa na kutumika kama mama. Mara nyingi utaona tabia yake ikibadilika ikawa ya kiwakati, anatakiwa awe kama mke, hivyo usijali mambo kama hayo kwa sababu ni maumbile yake yalivyo. Kwa hakika hana nia mbaya hivyo hakuna ubaya wowote.

6. Usishangae juu ya furaha zake

Maisha mazima ya mwanamke yanategemea juu ya bwana wake yaani maendeleo, afya, furaha ya mume wake n.k. Mara nyingi utaona mke akivutiwa na mambo mengi kama vile bwana anavyokua naye kuhusu kazi yake. Katika hali hii mambo yanatakiwa yawe ya kuzingatia vyema.

7. Mapenzi ya mama na mtoto yasilete husuda

Mama kwa mtoto ni muhimu sana na vile vile tutambue kuwa mtoto ni wa baba pia. Kwa hivyo angalia kusitokee husuda baina yako na watoto wako kwa mama wa nyumba.

8. Mawazo ya ofisini uyaachilie mbali

Itakubidi lazima ujifunze namna ya kuacha mawazo ya ofisini mwako wakati una rudi nyumbani ili uweze kukutana na familia yako kwa uso wenye bashasha na wenye furaha.

9. Kwenda matembezi

mmoja katika vitu muhimu ni kuwa wakati fulani wewe na mke wako muwe mkienda kutembea mkiwa peke yenu. Kwa mwanamke ni muhimu sana kwenda nje ya mazingira ya nyumba na jiko kwa sababu vitamletea siha nzuri na ile waka na wasiwasi vitamtoka. Kwa wanaume wanaokaa nje ya nyumba kwa siku nzima hawawezi kutambua vile mwanamke anavyokuwa amefungiwa nyumbani kwa siku nzima kwa sababu mwanamme anapokuwa nje anaona vitu vingi tofauti tofauti, anakutana na watu wengi anafanya kazi nyingi mbalimbali kwa hiyo hahisi kama yeye yuko kama mfungwa lakini mwanamke mwenye mbio zake chumbani, sebuleni, jikoni, kwa siku nzima anahisi kuwa yeye yuko katika kifungo na kwa kumchukua nje kwa ajili ya matembezi kutaleta siha nzuri ya afya yake ya mwili na kiakili.