Utangulizi
Sheikh Umar Jumaa Mayunga alikwenda Kenya ambako baada ya mazungumzo ya kidini, alishauriwa na Sheikh Abdallah Nasser (wa Nairobi) na Haji Ali Muhammad Ja'afer (wa Mombasa) kuwa atakaporudi Dar es Salaam aonane nami kwa maelezo zaidi.
Alikuja kuonana nami, na swali lake la kwanza lilikuwa juu ya Taqiyah. Nilimpa jibu lililomtosheleza kutoka kwenye Qur'an Tukufu na Ahadithi.
Baada ya hapo alikuwa akinitembelea mara kwa mara na mambo yote aliyokuwa akiyaelewa vibaya (kutokana na propaganda za kiovu za Wahabiyyah) aliyaelewa vipasikavyo.