4. Waliyodai "Ahlu - Tawheed" Na Majibu Yetu

Katika makaratasi yao hayo, ndugu zetu hao wamenukuu baadhi ya maneno yaliyomo katika Barzanji na Burdah (vitabu viwili vinavyoeleza sifa za Mtume Muhammad s.a.w.w.) na kujaribu, kadri ya ujuzi na uweza wao, kuonyesha kwamba kusema maneno hayo ni shirki. Lakini, kabla ya kutoa majibu yetu, tuanze kwa kuyanukuu maneno yenyewe. Nayo ni mane yaliyotolewa katika Barzanji, na mawili katika Burdah.

Swahili

3. Maulidi Katika Qur'ani Na Hadithi

Japokuwa -- kama tulivyoeleza katika sura iliyopita -- maulidi hayakutajwa kwa jina katika Qur'ani wala Hadithi, lakini yamekusanya mengi yaliyoamrishwa au yaliyopendekezwa na Qur'ani na / au Hadithi. Hapa chini tutayataja baadhi yake tu:

1. Kusoma na kusikiliza Qur'ani: Tunaposoma Qur'ani (k.m. Sura 73:4 na 20), tunaona jinsi Mwenyezi Mungu anavyotuamrisha tuisome. Na tunapokuja kwenye Hadithi zake, tunaelezwa kwamba Bwana Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipenda sana mtu amsomee yeye Qur'ani, na yeye akisikiliza.

Swahili

2. Hujja Za Wapinzani Na Majibu Yetu

Hujja yao ya kwanza ni kwamba: maulidi hayakuwako zama za Mtume Muhammad (s.a.w.w.) Kwa hivyo, kuyaleta baada ya yeye kufariki dunia, ni bid'a (uzushi). Na kila bid'a, kwa maneno yake mwenyewe Bwana Mtume (s.a.w.w.), ni upotevu. Kwa hivyo, kila anayesoma maulidi amepotea!

Swahili

1. Sherehe Za Maulidi

Maulidi ni Kiswahili cha neno la Kiarabu, mawlid. Neno hili lina maana ya "mazazi" au "kuzaliwa kwa…" (birthday). Kwa kawaida, linapotumiwa na Waislamu, huwa na maana ya siku aliyozaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), au hafla ya kuisherehekea siku hiyo.

Swahili

Utangulizi

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Bwana wa viumbe vyote. Na swala na salamu zimshukie Hashimu, Mtume Wake muadhamu (s.a.w.w.), na aali zake kiramu, na wote wenye kufuata nyayo zao.

Baina ya tarehe 4 Rabiiul Awwal, 1423 / 17 Mei, 2002 na 7 Jamaadath Thaani, 1423 / 16 Agosti, 2002 nilitoa mfululizo wa makala kumi na tatu juu ya maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Katika makala hayo, kwa kujibu hujja zinazotolewa na wale wanaopinga maulidi, nilijaribu kuonyesha kuwa maulidi si bid'a (uzushi) wala si haramu.

Swahili

Toleo Maalumu

… basi wale waliomwamini yeye
(Mtume Muhammad)
na kumhishimu na kumsaidia,
na kuifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye;
hao ndio wenye kufaulu.

(Surah 7:157)

*******************

Swahili

Ya Sayyidna Husaini

Kukuomba sina budi
Ya Razaku ya Wadudi
Ili utimu mradi
Yote nalo kusudia

Sikutaka kusimama
Mengi mno kuyasema
Ni mambo kunisukuma
Ni lazima kuelezea

Natokeza hadharani
Kwa ufupi nibaini
Yalomfika Husaini
Ya Rabbi niafikia

Yale ni mambo adhimu
Yalomfika Imamu
Sina shaka mwafahamu
Nami tawahadithia

Ule mwaka wa sitini
Wahijira sikieni
Kaondoka duniani
Muawiya kajifiya

Yazidi alitangaza
Nchi zote kaeneza
Dini ataiongoza
Ili watu kum-baiya

Swahili

Mtoto wake Husaini

Jambo jengine ni hili
La majonzi ikhiwani
Hiki si kisa cha pili
Ambacho ni cha huzuni
Ni cha kijana rijali
Mtoto wake Husaini

Kadhulumiwa Husaini
Na wake mwana mchanga

Naye kafa madhulumu
Kijana wa mikononi
Muovu huyo Khasimu
Adui aso imani
Bure kaimwaga damu
Ya kijana maskini

Kadhulumiwa Husaini
Na wake mwana mchanga

Kifo chake ni dhuluma
Kijana huyu yakini
Adui aso huruma
Aso Imani moyoni
Kwa mshale kamfuma
Ukamwingia mwilini

Swahili

Sifa Za Imam Hasan Na Imam Husain (a.s.)

Nawapa na taarifa
Japo kuwa walikufa
Walikuwa wana sifa
Njema zilotimilia

Walikuwa watukufu
Tena ni waaminifu
Walo na njema sharafu
Alowajazi Jalia

Walikuwa Maimamu
Kuongoza Isilamu
Mashujaa walotimu
Dini kuipigania

Walikuwa watu wema
Vijana wenye heshima
Akiwapenda Hashima
Wajukuu wa Nabiya

Walikuwa wenye dini
Maovu hawathamini
Na nyingi mno imani
Nyoyoni ilowangia

Walikuwa na huruma
Isilamu wenye hima
Toka kwa watu wazima
Na vijana wote pia

Swahili

Yapasa Tuyalilie Mauti Yake Husain

Na: Masoud Abdallali Muh'd,
Mombasa - Kenya

Imam Shafii Asema:

Husain! aliuliwa shahidi pasi na makosa yoyote
na kanzu yake ikatapakazwa wekundu.

Ikiwa dhambi zangu ni kuwapenda
Watoto wa Mtume Mohammad (s.a.w.w)
basi ni dhambi ambazo sitatubia.

Kwa sababu ya Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w)
Ulimwengu mzima ulitetema
na majabali na milima ilikaribia kuyeyuka.

Ni nani atakayemfikishia Husain ujumbe wangu na hata kama nyoyo zatukia?

Swahili