Husaini Mwana wa Ali

Naanziliza kwa jina
Lake yeye Subhana
Mola asiye kijana
Wala mke asiliye

Ndie watangu natangu
Kabula ya ulimwengu
Muumba nchi na mbingu
Milele Atabakiya

Asie na mshirika
Na wala hakuzalika
Ameketi pasi shaka
Enzie imetimiya

Sasa penda kuweleza
Kisa chenye kuchukiza
Na moyo nitaukaza
Hadi mwisho kufikiya

Ni rafiki wa Rasuli
Muhammadi mur sali
Husaini mwana wa Ali
Na Fatima Hashimiya

Swahili

Kwa Mwezi wa Muharram

Naanziliza kauli
Kwa jina lake Jalali
Na Swalawati Rasuli
Na-ali zake pamoja

Mswiba ulo adhimu
Kwa mwezi wa Muharramu
Dhuriya zake Hashimu
Karbala wakingiya

Hadithi imetuwambiya
Rasuli ameuswiya
Wapendwa wake dhuriya
Kinyume wakatumiya

Umati walibadili
Mahabba yao kwa Ali
Ikawa ni kuwadhili
Na maji kuwaziwiya

Yasitoshe walofanya
Ya Mtume kuyakanya
Dhuluma wakamuonya
Vijana kumuuliya

Swahili

Husain Amefariki

Hakika ni ujahili
Uovu na ukatili
Kuuwa pasi kujali
Bila ya kuzingatia

Asikiyae Hakika
Moyo utasikitika
Ma machozi yatatoka
Bila yakufikiria

Kwa huyu mtoto wake
Husain kina chake
Muda kiu imshike
Maji akihitajia

Kufika kwa makafiri
Husain alopojiri
Na mwana huyu saghiri
Maji alimuombea

Maadui wasijibu
Kwa kuwazidi ghadhabu
Mmoja wao kajibu
Mshale kuutumia

Jibu lake ni mshale
Kumchoma mwana yule
Akafia pale pale
Kifo cha kukusudia

Swahili

Machozi yamiminika

Kwa Jina la Rahmani
Na Muhammad Amini
Naanza kwa madhumuni
Kwa machungu na kuliya

Siku hizi za Ashura
Twazitaja kila mara
Kwa kubwa mno hasara
Maadui walotiya

Kiswache cha tuumiza
Na roho kutuunguza
Hatuwezi kunyamaza
Mashingo kuvumiliya

Twadhihirisha majonzi
Kwa Imamu na kipenzi
Na nyoyo zina simanzi
Kwa haya yalotokea

Twakumbuka siku hizi
Za vilio na huzuni
Ya kuuwawa Husaini
Mjukuu wa Nabiya

Swahili

Ya Aliy ya Aliy ya Abal-Husaina

Vikali mmeteswa na pepo mtaingia
Na waliowatesa motoni wataingia

Aliy Bunal Husaini kauwawa Karbala
Mishale pia vyuma vyote kuwa juuye

Aliomba ruhusa kwenda kupigania
Akapigwa mshale na lbn Fadhili
Kichwani mwake huyo Aliy Ibunil Husaini

Ashahidul Abasi kauwawa vibaya
Mikono ilikatwa yote miwili pia

Imam wetu Husain kauwawa Karbala
Mikuki na mishale vyote kuwa juuye

Kadhulumiwa Husaini huo mji Karbala
Humo usoni mwake mawe alirushiwa

Vitoto vililalama midomo ilikauka
Maji wahitajia adui wamezuiwia

Swahili

Ya Husaini Bin Ali

Kwa jina lako Jalali nasema yenye ukweli
Ya Husaini Bin Ali niwe nikihadithia

Mama yake ni Fatima, na babu yake Hashima
Na Madina mji mwema, ndiko alikozaliwa

Na Sayidina Husain, kaka yake ni Hasan
Akiwapenda amini, kisha akiwa sifia

Mtume amebaini, ya kama huyu Husaini
Na mwingine ni Hasani, Peponi wataingia

Yaani wao ni mabwana, wa peponi vijana
Subhana maulana, wote amewaridhia

Ni mwezi wa Shaabani, alozaliwa Husain
Na siku yake yakini, ni jumanne sikia

Swahili

Husain Akafahamu

Husain akafahamu, Ikawa hakuna budi
Mauti yake metimu, Dhiki imeshawazidi
Na kweli yake damu, Wazee kwa auladi
Adui watachezea, Roho zikiteketea

Adui pasi kuchoka, Kiu ilo kubwa mno
Waka mwandama mpaka, Joto lisilo kifano
Karbala wakafika, Vijana wazi midomo
Kusudi la mwandama ,Maji wanahitajia

Furati wakaushika, maji wanywayo wanyama
Pasi nafasi kutoka punda, farasi na kima
Mto wakauzunguka, Mjukuu wa Hashima
Na maji wakijinywea, Adui wakazuja

Swahili

Mzuri sana Husaina

Kiitikio

Mzuri sana Husaina, Wallahi na kuapia
Giza ilituenea,hapo ulipouliwa

Ee mwema mwana amani, umekufa kishahidi
Kunusuru hasa dini, ya wetu Mola wadudi

Umejitolea muhanga, ewe mwana wa Hashima
Ili kuhifadhi mwanga, Nuru kubwa ya Karima

Kila lote la azizi, kwa Rabuna umetoa
Bila kujali ajizi, hadi kufa kuokoa

Wanao wenye tohara, Nduguzo waso kifani
Masahaba we imara, umetoa uwanjani

Kunusuru haki kweli, mfano wako kuiga
Ujabali wenye dhili, kupambana bila woga

Swahili

Ya Shahida Karbala

Tunasikitika sana kwa kifo chako Husain
Ewe Husain ya shahida Karbala x 2

Mal-uni alofika kukuua ya Husain
Na Mungu atayaweka makazi yake motoni
Ewe Husain ya shahida Karbala x 2

Mbingu zilitikisika kwa kifo chako Husain
Majabali kupasuka kwa khofu na kwa huzuni
Ewe Husaini ya shahida Karbala x 2

Upanga uliushika ili kutetea dini
Kuchezewa yetu dini Husain hukuridhika
Ewe Husain ya shahida Karbala x 2

Swahili

Yaa Lailatal Ashri Tuul

Yaa Lailatal-ashri tuul
Qad zaada fiiki nnuhuul
Wadidtu min Qibali kuumi
Yaa hunu waq rrahiil

Bikarbalaa mudh-nazalnaa
Alimtu inda nnuzuul
Biannana sawfa nabqaa
Bila hami wwakafiil

Wadhaaka aadhamu thatwabi
Min zamani jaliil
Yumsil Husain Qatiilaa
Wa Yaalahu mun katiil

Fayaa dumuiya siilii
Alayhi kulla masiil
Thumma nthanat bintu twaha
Bi-Ibrati wa awiil

Tukhatibu-llayla laakim
Khitwabuha an dhuhuul
Taqulu la tubdi subhaa
Wadha minal mustahiil

Swahili