Table of Contents

Sura Ya 15: Utulivu Wa Hasan Na Shughuli Za Husein.

Swali, ambalo wakati mwingine hujadiliwa, ni kwa nini Husein hakuchagua kukubaliana na Yazid kama vile ndugu yake mkubwa al-Hasan, alivyofanya huko nyuma wakati akishughulika na Mu’awiyah. Swali hili hal- izingatii tofauti katika hali ya ndugu wawili hawa ambayo hukua katika umuhimu pamoja na uzito ulioambatana na hali za nje.

Kwani kwa mujibu wa imani ya Shi’a Hasan alimrithi Ali kama Imam, na Husein alimrithi Hasan katika wadhifa huo huo kama ilivyoamriwa na Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, ndugu wawili hawa, walikuwa na hadhi moja hiyo hiyo mbele ya macho ya Mtume na mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini Hasan alikuwa amewekwa pia kama khalifa.

Alipoona kwamba Mu’awiyah amefaulu katika kupanda kwa siri mbegu za kutofuatiana na kufarakana miongoni mwa Waislamu, na alikuwa ameingiza hisia za ukosefu mkubwa wa usalama kwa kudhoofisha utaratibu wa udumishaji wa amani, sheria na taratibu, Hasan aliona inafaa kuingia katika mkataba wa amani naye ambao chini yake huo alijiuzulu kwa manufaa ya mpinzani wake kwenye zile nyongeza tu, za mamlaka ya kidunia.

Hakujitenga kabisa kutoka kwenye ubora wa kiroho hata kidogo, na akaendelea kuwa kiongozi wa kiroho wa Waslamu. Mu’awiyah aliyavunja masharti ya mkataba wakati wa uhai wa Hasan, na ulipunguzwa kuwa makubaliano tu ya Hasan kutomwingilia Mu’awiyah.

Baada ya hitimisho la mkataba, Mu’awiyah alijaribu kwa uwezo wake wote kutaka kumvua Hasan ule ubora wa kiroho, na kwa kipindi cha miaka ishirini Husein alibakia amefungwa na masharti ya mkataba uliofanywa na ndugu yake. Baada ya watia sahihi kwenye mkataba walipokuwa wamekwishakufa, Husein hakufungua mazungumzo yoyote yale kwa ajili ya amani, akijua vyema kwamba sera kama ilivyodhihirishwa na mkataba na Hasan wa kumnyima uongozi wa kiroho wa mamlaka ya kidunia umebadilishwa na ule wa kuteka au utwaaji wa uongozi wa kiroho na mtawala mwenyewe.

Viunganisho katika nyororo hii ya utekelezaji wa sera hii vilikuwa ni uvunjaji wa dhahiri wa masharti ya mkataba na Hasan, na mauaji ya Hasan yaliyifanywa na mmoja wa wake zake, aliyeitwa Ju’da, ambaye alimtilia sumu kwa maelekezo ya siri ya Mu’awiyah.

Kielekezo kingine katika welekeo uliotajwa katika ibara iliyotangulia kimetolewa na khitilafu au tofauti katika namna na taratibu ambamo Yazid aliwafanya watu watoe kiapo cha utii kwake kutokana na njia na mitindo ambayo ilikuwepo na kutumika katika siku za Makhalifa waliotangulia. Katika matukio kama hayo walikuwa wakiahidi kuzitetea amri za Qur’an na Sunna za Mtume.

Ufidhuli wa Yazid na kiburi ulikifanya kiapo kuwa ni utambuzi wa unyonge kwa mwenye kuapa kwamba alikuwa ni mtumwa wa Khalifa ambaye angeweza kuangamiza maisha yake, mali yake na kizazi chake katika namna yoyote ile aionayo inafaa. Yazid ibn Abdallah ibn Rabia alikuwa tayari kutoa kiapo cha utii kwa mujibu wa taratibu ya zamani lakini alisita kuapa kumtii Yazid kwa mtindo uliopendekezwa. Akauawa. Haya yalifanyika Madina.

Wapi, basi palipokuwa na haja yoyote ile kwa Husein kujaribu kujipendekeza kwa Yazid? Husein alikuwa akishirikiana kwa ukaribu mno na Hasan wakati wa miaka yote iliyopitiwa na mkataba wa Hasan na Mu’awiyah, na alikuwa ameona upotofu uliokuwa umejitokeza wa mielekeo iliyoenea inayoelekezwa kwenye dini (imani) na kukosekana majibu ya malalamiko yake ya mdomo na maandishi dhidi ya kile kilichokuwa kinatokea katika nchi za Kiislamu.

Lazima atakuwa ameona ya mbele kwamba upinzani wa namna ya mfano, kama ni lazima, mpaka mwisho mchungu, ulikuwa utolewe ili kuuokoa Uislam. Hata hivyo, hakufanya haraka katika kulifanya hilo. Alipochukua madaraka, hatua ya kwanza ya kisiasa ambayo Yazid aliichukua ilikuwa ni kutaka kiapo cha utii cha Husein cha kumtii yeye chini ya vitisho vya kutumia nguvu.

Hapa ndipo ambapo Husein alipojiona amewekwa katika mazingira ambayo yalikuwa kwa dhahiri kabisa tofauti na yale ambayo yalimkabili Hasan ambaye aliachia madaraka yake ya kidunia tu kwa manufaa ya Mu’awiyah kwa ajili ya kuiweka amani na utulivu katika milki yake.

Alikuwa, hata hivyo, ameshikilia ubora wake wa kiroho na uongozi wa Waislamu. Husein alishurutishwa siyo tu kujivua ubora wa kiroho, bali pia kutoa kiapo cha utii kwa Yazid ambaye alichukua amri za Qur’an na Sunna za Mtume kwa thamani ndogo sana. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba hakuna hata mmoja wa marafiki na ndugu zake Husein, hali wakiwa wanamshawishi asiondoke kwenda Kufa, na wakimshauri kubakia Madina, au kukaa Makka au kwenda Ta’if au Yemen, aliyependekeza kwake kukubaliana na kuchukua kiapo cha utii kwa Yazid.

Ilikuwa inafahamika kwao wote kwamba aina hii ya kiapo cha utii ilikuwa nje kabisa ya suala hili kwa kiasi ambacho Husein alikuwa anahusika, ikiwa yenye kubomoa yale yote yaliyokuwa matukufu na ya hali ya fikira za kiungwana, na kufikia kubadilishana haki mbalimbali za Waislamu, na madai yake mwenyewe ya haki.