Table of Contents

Sura Ya 16: Msimamo Wa Husein - Fasiri

Suluhu na Yazid ikiwa haiwezekani kabisa, njia mbadala pekee iliyo ya wazi kwa Husein ilikuwa ni kumpinga Yazid ili kuyaokoa maadili mema ya Uislam kutokana na kushuka zaidi chini na kuilinda dini yenyewe kutokana na mashambulio yenye kuangamiza ya uhuishaji wa hali ya kabla ya Uislam.

Asingeweza, hata hivyo, kulea ndoto au fikra za uwongo kuhusu aina ya msaada ambao angeweza kuutumainia kujiorodheshea katika mzozo wowote ule na Yazid.

Hali iliyokithiri ya kutofurahisha ambamo ndugu yake, Hasan, alijikuta nayo mwenyewe, kupitia kule kuondoshwa kisaliti kwa msaada aliokuwa amepewa katika kukabiliana kwake na Mu’awiyah, na vile alivyoacha Hasan, chini ya vikwazo, yale madaraka ya kidunia kwa manufaa ya Mu’awiyah, na uvunjaji wa Mu’awiyah wa masharti yote ya mkataba wake na Hasan bila kupata adhabu yoyote juu ya hilo, yote haya yalikuwa ni historia tu ya siku za karibuni, na umuhimu wake usingeweza kupotea (akilini) kwa Hasan.

Kwa hiyo, yeye alifikiria mkakati mpya kabisa wa vita na Yazid, kwani, kwa hali yoyote ile, vita ilikuwa lazima iwepo. Hakufanya jaribio la kukutana na nguvu za kijeshi za Yazid kwa uwezo wake mwenyewe wa kijeshi. Hakujenga matumaini juu ya nguvu za idadi (kubwa ya watu) kwa mafanikio ya jambo lake (la haki) au juu ya njia zozote zile za kimaada. Husein aliamua kupigana vita na Yazid kwenye uwanja wa kiroho, kupinga maguvu ya Yazid kwa nji ya utukufu wa tabia yake, kuikabili nguvu kwa kutokuwa na maguvu, kukutana na makundi pamoja na ukosefu wa msaada wa nyenzo na kupinga dhulma kwa (kukubali) kuteseka na kufa kishahidi.

Utajiri mkubwa ambao ulimiminika katika nchi za Waislamu ukiwa kama matokeo ya kutekwa nchi kulikofanywa na Waislamu na namna za maisha ya anasa ya watawala na matajiri, ziliwafanya wapuuze wajibu wao kwa Mwenyezi Mungu na wanadamu wenzao. Ilikuwa ni hatua fupi, rahisi tu kwa watu kwa kawaida kutwaa mielekeo ya wakubwa wao wa kijamii.

Mbali na kutoa huduma za maneno matupu kwenye itikadi fulani fulani za kiislamu, na utekelezaji wa kijuujuu tu wa baadhi ya matendo ya Kiislamu, ule moyo wa Kiislam kwa kweli ulikuwa umelala bwete katika jamii ya Waislamu.

Ili kuendeleza mamlaka yao, watawala wa Bani Umayyah walitafuta kuto- ka kwa Waislamu utii mkubwa kwa watawala wao. Hili lingeweza kufanikishwa kimya kimya bila kujitokeza kwa kuingiza ugoigoi katika welekevu wa akili na kuwanyima watu hamu na ujasiri wa kuzungumza.

Baadhi ya watu maarufu ambao hawakujitolea kuusaidia utaratibu uliowekwa katika kuendeleza njama hii ya ukimya, huu ufishaji wa uwezo wa kuhisi wa umma na huku kusimamishwa kwa muda kwa uhuru na ukweli wa kuelezea maoni, walipatikana wakifanya hivyo kwa kupewa misaada au kwa vitisho vya matokeo ya kuuawa kwao, na kampeni za kitaifa za kuwaondolea watu uwezo wa kufikiri kwa uhuru kabisa na ujasiri wa kuongea zilishamiri.

Mbinu kubwa ya al-Huseun ya kupinga utawala wa Yazid ilikuwa ni kuhuisha uwezo wa watu wa kuhisi, kuamsha ndani yao uwezo wa kujifikiria wenyewe kwa hali ya kuwa huru kabisa, na kuwarudishia ujasiri wa kutoa maoni kwa uhuru kwa uamuzi wa dhamira zao.

Bani Umayyah ambao kwa nje waliukubali Uislam, walijaribu kuuangamiza Uislam kutokea ndani kwa kupotosha mafundisho yake, na kuwanyima Waislamu uwezo wao wa kuhisi, na ujasiri wa kuongea. Husein, kwa hiyo alikusudia kuipasua barakoa ya Uislamu kutoka kwenye uso wa watawala wa Bani Umayyah ili kudhihirishia ulimwengu walikuwa mbali kiasi gani kutokana na kuzionyesha alama halisi za Uislam, na kuwatenganisha Waislamu kutokana na washauri wao waliopotoka ili kuviokoa vizazi vijavyo vya Kiislamu kutokana na kuitukuza mifano iliyowekwa na wao kwa jina la Uislam ili kwamba wakati wowote njia mbaya au ovu za Bani Umayyah zilipotajwa kwa kuushushia hadhi Uislam, tabia yake mwenyewe (Husein) na mwenendo vingeweza kutajwa mara moja kwa kuwaokoa Waislamu kutokana na fedheha.

Malengo ya Husein aliyokuwa nayo katika fikra yasingeweza kupatikana kama angepigana kwa msaada wa nyenzo. Vita vya namna hiyo hus- ababisha vifo vya watu na uharibifu wa mali, lakini siyo kuangamia kwa itikadi. Kuchinjwa kwa watu na kuangamizwa kwa mali vilikuwa siyo sehemu ya lengo la Husein, na kuangamia kwa itikadi ambako kulikuwa kunadhoofisha dini kusingeweza kupatikana kwa vita katika uwanda wa nyenzo na zana.

Aidha, vita inayopiganwa kwa msingi wa nguvu za kijeshi vingeweza pia kuchanganywa, kwa kufananishwa na vita kati ya washindani wawili wanaogombea madaraka ambavyo vilikuwa mbali na ukweli kulingana na Husein alivyokuwa amehusika. Vita kama hivyo, kwa hali yoyote ile, vingekomea katika mafanikio kwa Yazid na huenda vingemwacha Yazid akiwa bado amefunikwa katika vazi la Kiislam, wakati vita vya Husein vilivyopiganwa katika uwanda wa kiroho, kwa kiasi vilimfedhehesha mtawala kiasi kwamba alipoteza huruma zote juu yake kutoka kwa wanadamu.