Table of Contents

Sura Ya 20: Majeshi Yakusanyika Dhidi Ya Husein.

Baada ya mauaji ya Muslim bin Aqil kule Kufa, Ubaydullah bin Ziyad alichukua hatua za ukali usio na ukomo kuondoa kutoka kwenye mawazo ya watu zile fikra zote za uaminifu na utii kwa Husein ambaye kwake yeye idadi kubwa ya wao wametoa kiapo cha utii mikononi mwa Muslim. Wale ambao dhidi yao hata shaka ndogo sana kiasi gani waliyoweza kuwa nayo ya uaminifu na utiifu kwa Husein waliuawa au walitupwa gerezani bila ya kufanyiwa uchunguzi wowote.

Mitham, ambaye alikuwa akiuza tende na Rashid al-Hajri waliuawa wakati wa utawala huu wa hofu. Al-Mukhtar bin Abi Ubayd al-Thaqaf pia alifungwa, ingawa alikuwa hayupo mjini Kufa wakati Muslim alipouawa, na alikuwa, kama suala la uangalifu, alikubali hifadhi ya maisha na mali iliyotangazwa hapo Kufa kwa wale ambao wali- itafuta chini ya bendera iliyopandishwa na Amr bin Hurayth.

Baada ya kwisha kutokomeza upinzani wote kwa mtawala, Yazid, hapo mjini, Ubaydullah bin Ziyad alichukua hatua za kuzuia hatari kwa serikali iliyoanzishwa iliyokuwa ikiibuka kutokea katika maeneo yapakanayo na Kufa, ambayo alipanga iweze kulindwa kwa ulinzi mkali sana. Kamanda wa shurta, Husein bin Tamim, alitolewa akiwaongoza watu 4000 kwenda Qadisiyya ambako njia kuu kutoka Hijaz, Iraq na Syria zilikutana. Vikosi vilisambazwa katika pande zote za njia kuu zinazokuja kutokea Basra na Syria na katika vituo vingine nyeti na dhaifu ili kuwazuia wale wote wenye kumwonea huruma Husein na kuwazuia wasiingie Kufa kusababisha matatizo hapo.

Basi wakati huo huo kabila la Dailam liliasi na kuushika mji wa Dastaba, ambao ulikuwa nje ya eneo la Kiarabu. Umar bin Sa’ad alipelekwa na watu 4000 kwenda kuwazimisha waasi, na malipo kwa huduma hizo, alipewa hati ya maandishi akiteuliwa kuwa mtawala wa Rayy, Dastaba na Dailam.
Jeshi hilo lilikuwa limeondoka kuelekea Iran, na yeye mwenyewe alikuwa katika hatua za kuondoka wakati suala la kumshughulikia Husein lilipochukua umuhimu tena. Ubaydallah bin Ziyad alimtaka Umar bin Sa’d kuzifikisha kampeni dhidi ya Husein kwenye mwisho wenye kufuzu, na kisha ndiyo aende Iran.1

Umar bin Sa’d alizaliwa ile siku ambayo Umar, khalifa wa pili aliyokufa. Kwa hiyo, ni lazima atakuwa amewaona masahaba wengi wa Mtume, na kuzisikia kutoka kwao zile hadith za Mtume ambazo zilionyesha upendo mwingi aliokuwa nao kwa wajukuu zake, Hasan na Husein. Atakuwa pia amemuona binafsi yeye Husein, na kumwona ni mtu mwenye tabia tukufu. Akihusishwa kwa kulinganisha ukaaji wake wa hivi karibuni mjini Makkah, maelezo kuhusu kujinyima kwa Husein, ucha-Mungu wake na utukufu wa tabia yake lazima hayo nayo pia atakuwa ameyasikia.

Kwa sababu zilizotajwa katika ibara ilitoyangulia Umar bin Sa’d hakupenda kupigana dhidi ya Husein akiona kwamba ni dhambi kufanya hivyo. Alipendelea kuachwa huru kutokana na kuchukua jukumu la kufanya kam- peni dhidi ya Husein. Ubaydullah bin Ziyad hapo hapo akataka irudishwe kwake ile amri ya kuteuliwa yeye kuwa mtawala wa Rayy, na hili lilimkabili Umar bin Sa’d kwa mgongano katika mapendeleo yake. Aliomba apewe siku moja ili afikirie na kutafakari juu ya jambo hili. Rafiki zake walimshauri asipigane dhidi ya Husein.
Mmoja wao alisema, “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kama utajiri wote na serikali zote vingekuwa katika milki yako, na ungekuwa upotee kwako ingekuwa ni vizuri zaidi kuliko kujichukulia jukumu la kumwaga damu ya Husein.2Tamaa ya kuwa na cheo kikubwa ilimvuta kuelekea upande tofauti na kiakili akawa katika huzuni na fadhaa kubwa.

Mwishowe hata hivyo aliruhusu mvuto (ubembe) unaopita wa madaraka ya kilimwengu kupotosha uamuzi wake, na akakubali kupigana dhidi ya Husein; na akaondoka kwenda Karbala na jeshi lake. Alifika Karbala mnamo mwezi 3 Muharram.3Pamoja na askari elfu moja chini ya Hurr, nguvu ya jeshi la Umar bin Sa’d ilipanda na kufikia watu elfu tano (5000), lakini Ubaydullah bin Ziyad, akielewa vyema ushujaa wa asili wa familia ya Husein aliwapeleka askari 3000 waliobakia wa ngome ya al-Qadisiyya kwenda Karbala pia.

Uandikishaji wa jumla wa askari kwa ajili ya jeshi ulitangazwa hapo Kufa, na Ubaydullah bin Ziyad alikwenda Nukhayla ambao uko katika njia iendayo Karbala kwenda kuyakagua majeshi na kuyapeleka Karbala bila mkatizo wowote ule. Viongozi muhimu wa Kufa walielekezwa kwenda Karbala na wafuasi wao. Kila mmoja katika wao ilibidi aondoke na jeshi kubwa, na kutokukubaliana na amri hii ilikuwa haisameheki kwa sababu yoyote ile. Hofu kuu iliingia katika nyoyo za wale ambao walirudi Kufa mara moja tu baada ya kutokea mbele ya Ubaydullah bin Ziyad.

Alipojua jambo hili, alimpeleka Suwayd bin Abd al-Rahman Minqar na kiasi cha askari wapanda farasi kwenda Kufa kumkamata kila mtu pale ambaye hajaondoka bado mpaka wakati huo hapo mjini kwenda kuungana na wenzie katika vita dhidi ya Husein. Suwayd alimkuta Msyria mmoja ambaye alikuwa katika ziara mjini Kufa kwa jambo lenye kuhusiana na mgogoro wa urithi wa mali. Mtu huyo alipelekwa kwa Ubaydullah bin Ziyad alihukumiwa akatwe kichwa chake mara moja. Kisha kila mtu alikwenda Karbala kupigana dhidi ya Husein.

Kwa hiyo, ilikuwa siyo muhimu kuzithibitisha takwimu zilizotolewa na wanahistoria mbali mbali- 20,000 za Ibn Tawus; 30,000 za al-Majlis; 35,000 za Ibn Shahrashub na 100,000 na wengine kama idadi ya watu ambao walijitokeza kupigana dhidi ya Husein.

Hatua zilizochukuliwa kuliongeza jeshi kupigana dhidi ya al-Husein yatosha kuoinyesha kwamba wakazi wote wa Jiji kubwa la Kufa, wafaao kwa kazi za kijeshi, kwa kweli walimiminwa mjini Karbala wakiwa katika muundo wa majeshi ya Yazid.

  • 1. Tabari, II uk. 308.
  • 2. Tabari, cha II, uk. 308-309.
  • 3. Tabari, cha II, uk. 309.