Table of Contents

Sura Ya 21: Marafiki Wa Husein, Udhaifu Wao Katika Idadi Na Sababu Zake

Mauaji ya jumla ya kikatili na kufungwa jela, hapo Kufa, kwa kila mtu aliyetiliwa shaka ya kuwa na huruma na Husein, chini ya maelekezo ya Ubaydullah bin Ziyad, yasingeweza kuacha nyuma hata kidogo bila kuumiza mtu yeyote yule isipokuwa idadi ndogo sana ya wale watu ambao kwa kweli wangeweza kuelewa wajibu wao wa kumpa msaada.

Marafiki kama hao kutoka Kufa au maeneo mengine lazima, hata hivyo, wawe wameona ni vigumu sana kujiunga na Husein ili kumsaidia, kwani njia zote za kumfikia yeye hapo Karbala kwenye sehemu zote muhimu na za kimikakati kama vile al-Qadisiyya, Khattan, Qutqutana na La’la, zimewekwa chini ya askari doria wa kijeshi pamoja na amri za kuwakamata wale wote ambao walipenda kuendelea kwenda kumsaidia Husein.

Sababu nyingine kwa kuwepo idadi ndogo sana ya watu ambao walijitokeza kumsaidia Husein hapo Karbala ilikuwa kwamba kuwasili kwake pale hakukutegemewa na kulikuwa kwa ghafla na kulikuwa hakujulikani katika viunga vya Kufa, hivyo kwamba hata baada ya siku kupita baada ya matukio haya ya masaibu kutokea pale Karbala, watu wengi walikuwa hawayatambui.

Hata hivyo wale wa upande wa kundi la Shia ambao walianzisha harakati za kumwita Husein kuja Kufa, na kwa kuwasili kwa Muslim bin Aqil huko Kufa, walikula kiapo cha utii kwake katika mkutano wa kwanza na wakaapa kujitoa mhanga katika kumsaidia Husein, na walifika Karbala na walijitoa mhanga kwa ajili ya Husein. Na hakuna hata mmoja katika wao, ambaye hakuweza kwenda kumsaidia Husein ameonekana akipigana dhidi yake.

Jeshi la Umar bin Sa’d liliundwa na watu wa kawaida wa Kufa na jamaa wa makabila wanaoishi katika viunga vya mji. Hawakuweza kutegemewa kuwa na nguvu ya utashi, moyo, ari na uthabiti wa marafiki wa Husein. Watu hawa hawakuwa bora zaidi kuliko watu waliofundishwa kutii kibubusa tu kiongozi wa kikabila, wasiojali au hata kuwa wajinga wa kutojua masuala yaliyowaingiza katika vita ambavyo walikuwa wanapigana.

Baadhi yao hawakuwa tayari kupigana dhidi ya Husein, lakini walikosa nguvu za kiuadilifu kutenda kwa mujibu wa yale yanayoamriwa na dhamira zao wenyewe. Kwa sehemu kubwa walishirikiana pamoja kuunda sifa njema mbele ya macho ya wakuu wao wa kijamii, na zawadi na vyeo walivyoahidiwa na serikali.

Kinyume chake, watu wote wa Kufa ambao walikuwa pamoja na Husein walifanya tabaka la watu wa kiroho wa mjini pale, na walikuwa ni mabwana wadhibiti wa utashi wao na matendo yao mbele ya mitihani mikubwa. Wengi katika wao walikuwa ni watu wenye kufahamika sana wa Kufa, na walifaidi ushawishi na mvuto mkubwa kiasi katika mji.

Watu wa Kufa, kwa ujumla, hawakuweza kuelewa kwa nini watu kama hawa wenye kudumu katika sala kwa utiifu kabisa na wenye kujinyima wamejiingiza katika vita. Watu hawa wakati mwingine huonesha athari yenye nguvu kwa maadui zao kiasi cha kuwaogopesha.

Katika maelezo ya vita vya Karbala mtu mara kwa mara hukutana maelezo ya maadui wanaokimbia mbele ya wapiganaji wa Husein. Kuondoka huku kwa ghafla ghafla kulikuwa ni matokeo tu ya misuto ya dhamira iliyohisiwa na maadui mbele ya watu wenye tabia njema kama hizi kama wafuasi marafiki wa Husein.