Table of Contents

Sura Ya 22: Mazungumzo Ya Amani

Tamaa ya mamlaka ya kidunia na utukufu vilimfanya Umar bin Sa’d kukubali mapatano na Ubaydullah bin Ziyad, ambayo aliyajua kuwa ni mabaya, ya kuliongoza jeshi lake kwenda Karbala kumwaga damu ya Husein kwa malipo ya kuupata utawala wa eneo la Rayy. Alitamani sana kujiokoa kwa njia ya kiwerevu kutokana na shughuli hii chafu na alipofika Karbala, alijaribu kugundua uwezekano wa kuwepo ufumbuzi wa amani kuhusu mgogoro uliopo kati ya pande husika.

Alimtuma Qurra bin Qays al-Hanzali kwa Husein kwenda kujua kutoka kwake lengo la jambo lililomfanya kuitembelea Iraq, kwa kutokea mbali kote huko katika nchi ya Hijaz.

Husein alimwambia Qurra kwamba wenyeji wa Kufa walimwita kuja katika mji wao, na kwamba kwa vile walionekana kutokupenda kuwepo kwake hapo mjini, alikuwa yuko tayari kurudi alikotoka. Qurra alilifikisha jibu hili la wazi kwa Umar bin Sa’d ambaye aliliona ndani yake kuwepo mwanzo ya kuleta amani.

Alimwandikia Ubayddullah bin Ziyad yale yote ambayo yametokea kati yake na Husein. Alipokwishaipata barua hii Ubaydullah alisoma shairi, linalomaanisha “Sasa kwa vile wako katika makucha ya mikono yetu, wanaomba waachiliwe. Hawawezi kutukimbia.”

Alimwandikia Umar bin Sa’d majibu, akisema, “… unaweza sasa ukamshauri Husein kwamba yeye na sahaba zake wote lazima watoe kiapo cha utii kwa Yazid. Nitalifikiria suala hili tena wakati hili (la kiapo) limekwisha tendeka.”1
Barua hii ilivunja matumaini ya Umar bin Sa’d ya amani kati ya makundi haya. Kuleta suala la Husein kutoa kiapo cha utii kwa Yazid lilikuwa jambo lisilo la haki kabisa. Pia, hata kama ni kwa ajili ya hoja tu, mtu angekubali kwamba jambo lisilowezekana lingetokea, hakuna ahadi kwa tendo lolote lile lipendezalo lilionekana limeshikwa kwa ajili ya Husein serikali ingeweza hata hapo kumpa aina ya adhabu ambayo wangeiona ni yenye kufaa.

Ubaydullah bin Ziyad alishindwa kabisa kuelewa maana ya jibu la Husein kwa Umar bin Sa’d. Lilikuwa tu limetegemezwa juu ya jaribio la kumaliza mabishano yote na kuondoa uwezekano wa kutokea vita kati ya makundi haya. Ubaydullah alifikiria kwamba labda Husein alikuwa ametishwa na majeshi makubwa yaliyotumwa na yeye kwenda Karbala, na kwa hiyo, akaamua kurudi alikotoka. Umar bin Sa’d, ambaye alikuwa akimchunguza Husein kwa ukaribu zaidi katika sehemu za makazi yake alijua vizuri zaidi, na akasema, “Nilijua kwamba Ubaydullah bin Ziyad hataki amani.”2
Aliipeleka barua yake kwa Husein ambaye alitengeneza jibu hili tu, “Hili haliwezi kamwe kuwa. Lililo kubwa kabisa ambalo laweza kuni- angukia ni kifo na mimi niko tayari kukikaribisha.”3

  • 1. Tabari, uk. 311.
  • 2. Ibid.
  • 3. Al-Akhbar al-Tiwal, uk. 254.