Table of Contents

Sura Ya 28: Mihanga Iliyotolewa Na Banu Hashim.

Wakati baada ya kupigana vita na jeshi la Umar bin Sa’d katika siku ya 10 Muharram mwaka wa 61 A.H hapo Karbala, na marafiki wote wa Husein walipopata shahada, jamaa zake waliingia kwenye medani ya vita kupi- gana na adui na kujitoa mhanga maisha yao kwa ajili ya Husein.

Ni udhihirisho wa nadra sana wa utii, upendo na uaminifu wa masahaba wa Husein kwa ajili yake kwamba muda maadam hata kama ni mmoja wao anabakia hai, hakuna hata mtu mmoja wa ukoo wa Hashim aliyebakia angepatwa na huzuni.

Yafuatayo ni maelezo mafupi ya maisha ya ndugu wa al-Husein na jihad zao katika mpangilio ambao waliingia katika medani ya vita:

1. Ali al-Akbar alikuwa mtoto wa Husein na wa kwanza katika mashahidi wa ukoo wa Hashim.1 Mama yake, aitwaye Laila, alikuwa bint wa dada wa mtawala wa Syiria, Mu’awiyah, na binamu ya Yazid. Alikuwa ame- heshimiwa na kutukuzwa sana na marafiki na hata maadui pia. Mu’awiyah aliwahi kuwaambia watumishi wake kwamba Ali bin Husein alikuwa mtu mwenye haki kabisa ya ukhalifa, kwani alikuwa mjukuu wa Mtume na alichanganya ndani yake ushujaa wa Bani Hashim, ukarimu wa Bani Umayyah na heshima binafsi ya kabila la Thaqif ambalo kwalo mama yake alitokezea.

Kwa mujibu wa al-Mufid, Ali al-Akbar alikuwa na umri wa miaka kumi na tisa pale wakati masaibu ya Karbala yalipotokea. Alikuwa na uzuri wa ujanadume usio na kifani na madahiro. Alikuwa kipenzi makhsusi wa Husein kwa sababu alikuwa na mshabihiano mkubwa na Mtume katika sura yake na mwenendo wake. Alikuwa anaitwa Ali al-Akbar kwani alikuwa mkubwa kuliko ndugu yake Ali al-Asghar (Abdallah) ambaye alikuwa pia ameuawa kishahidi hapo Karbala. Hata hivyo, alikuwa mdogo kuliko kaka yake, Ali Zayn al- Abidin.2

Baada ya wafuasi wa Husein kuwa wamekwishajitoa mhanga maisha yao, Ali al-Akbar alikuwa wa kwanza miongoni mwa ndugu zake kumwomba Husein amruhusu kwenda kutekeleza Jiha.

Akiamsha mikono yake juu, Husein alisema, “Ee Mwenyezi Mungu! Kuwa shahidi wangu kwa uonevu wa kikatili wa watu hawa ambao anawaendea yule kijana mzuri, ambaye zaidi ya yote amefanana na Mtume wako kwa sura na mwenendo. Wakati tulipotamani kumwona Mtume Wako, tulitumia kuangalia sura yake huyu.” Dua hii fupi inabeba ushahidi wa kutosha kuhusu uchungu wa moyo wa Husein na kujizuia.

Kisha Ali al-Akbar alijitambulisha kwa maadui kwa mashairi yenye maana kwamba, “Mimi ni Ali, mtoto wa Husein na mjukuu wa Ali bin Abi Talib. Naapa kwa Mwenyezi Mungu wa al-Ka’aba, tunayo stahili bora zaidi ya kumrithi Mtume Wake. Kwa jina la Allah kizazi cha mtu wa uzawa wa haramu hawezi kuamua mambo yenye kutuhusu sisi.”3

Hapa hakuna maneno yaliyotumika kumvutia msomaji juu ya ushujaa wa mzungumzaji, kwa sababu ilikuwa siyo lazima kufanya hivyo, baada ya tangazo kwamba mzungumzaji alikuwa wa ukoo wa Hashim. Ali al-Akbar alikwenda moja kwa moja kwenye kiini cha jambo ambalo liko katika mzozo, na akadai kwa ajili ya Bani Hashim kile cheo bora cha kumrithi Mtume kama Makhalifa wake, akitweza, kwa rejea fupi na zenye nguvu, visingizio vya Yazid kwenye ukhalifa.

Ali al-Akbar aliwashambulia maadui mara nyingi, mara zote akiingiza kuimba mashairi ambayo yamekwishatajwa. Ingawa alijeruhiwa mno, alishikilia kufanya mashambulizi kwa maadui katika mfuatano wa haraka haraka, mpaka alipopata fursa Murr bin Munqidh, askari, alimpiga kwa mkuki ambao ulimchoma ukaingia kifuani mwake. Ali al-Akbar alianguka chini kutoka kwenye farasi wake, na maadui walimzunguka na kuukata mwili wake kwa panga zao katika vipande vipande.

Kifo cha Ali al-Akbar kilikuwa kwa hakika msiba mkubwa kwa Husein ambaye alitamka kwa mshangao, “Namwomba Allah awaangamize watu hawa ambao wamekuua wewe mwanangu! Maisha baada yako hapa duniani hayana thamani kama ilivyo vumbi.”4 Maiti ya Ali al-Akbar kisha ilichukuliwa na vijana wengi wa ukoo wa Hashim na kuletwa katika hema lililofanywa kama kituo cha kuangalilia jeshi la al-Hashim linapopigana.

2. Abdallah ibn Muslim ibn Aqil alikuwa mtoto wa Rukayya, binti ya Ali bin Abi Talib, na kwa hiyo, katika kuongezea kwamba alikuwa mtoto wa binamu ya Husein, Muslim, pia alikuwa mtoto wa dada yake, Rukayya. Alikuwa shahidi wa kwanza hapo Karbala, kutoka miongoni mwa dhuria wa Aqil. Alikuwa kijana mdogo sana katika wakati huo. Kifo cha Ali al-Akbar kilisababisha sauti kubwa za maombolezo na vilio kutoka kambi za Husein kiasi kwamba baadhi ya vijana wadogo, pamoja na Abdallah bin Muslim, walitoka nje ya mahema katika hali ya huzuni kubwa na fadhaa. Hii ilimpa nafasi askari mmoja wa upande wa adui kumuua (Abdallah bin Muslim kwa mshale aliotupiwa.5Tafsiri nyingine ya tukio hili ni kwam- ba askari mmoja asiye na huruma alimshambulia kwa mkuki na kumuua.6

3. Muhammad bin Muslim bin Aqil alikuwa ndugu wa Abdallah bin Muslim kwa mama mwingine. Baada ya kifo cha Abdallah kizazi cha Aqili kilifanya mashambulizi ya pamoja kwa adui, na Husein alitamka kwao kwa sauti kubwa, “Enyi watoto wa ami yangu! Yashikilieni mauti!” Mwishowe mshale aliotupiwa Muhamad bin Muslim ulimchoma na akauawa.

4. Ja’far bin Aqil aliingia katika medani ya vita baada ya Abdallah bin Muslim alipokwishauawa kishahidi. Alianza vita vyake kwa maneno, “Mimi ni mwenyeji wa Makkah, na ninatokana na familia ya Talib, kizazi cha Hashim na nyumba ya Ghalib. Kwa kuhakikisha sisi ndiyo viongozi wa makabila yote na Husein ndiye aliye mtu tohara kabisa kuliko wote katika watu walio tohara.” Aliuawa kwa kupigwa mshale.

5. Abd al-Rahman bin Aqil alikuja katika medani ya vita na akasoma beti za utangulizi za kivita. Kisha aliingia katika vita, akapigana, na baada ya muda kidogo mshale aliotupiwa na muuaji wa ndugu yake Ja’far, ulimuua yeye pia.

6. Muhammad bin Abi Sa’id bin Aqil alipigana katika vita vya Karbala. Alijeruhiwa vibaya sana katika paji la uso kwa mshale, na baada ya muda mfupi tu baadaye alijiunga kwenye safu za mashahidi (alikufa kifo cha kishahidi).

7. Muhamad bin Abdallah bin Ja’far bin Abi Talib alikuwa mtoto wa bina- mu yake Husein, Abdallah, kwa Khawsaa bint ya Hafsa bint Thaqif na ali- tokana na kabila la Bakr bin Wa’il. Muhammad na ndugu yake, Awn ambaye alikuwa mtoto wa Zainab bint Ali, walikuwa wametumwa na baba yao kufuatana na Husein. Ndugu hawa wawili walikutana na Husein muda mfupi tu baada ya yeye kuondoka Makkah, na kutoka hapo walisafiri wote pamoja naye kwenda Karbala. Aliingia kwenye medani ya vita baada ya Abd al-Rahman bin Aqil na baada ya kufanya mapigano machache alikutana na shahada yake, akiwa ameuawa na Amr bin Nahshal al-Tamim.

8. Awn bin Abdallah bin Jafar alikuwa mtoto wa dada yake Husein, Zainab, na aliingia katika uwanja wa vita baada ya ndugu yake Muhammad, na muda mfupi baadaye Abdallah bin Qurba al-Tai’ alimuua.

9. Al-Qasim bin Hasan alikuwa mpwa wa Husein. Alikuwa mtoto mdogo wakati vita vya Karbala vilipotokea, na alikuwa kijana mwenye sura nzuri sana hivyo askari mmoja wa upande wa jeshi la adui alielezea kutokea kwake katika uwanja wa vita kama tazamo la mara moja la mwezi mpya. Alikuwa hakuvaa koti la chuma wakati alipokwenda kupigana na ugwe (kamba) wa kiatu chake kimoja ulikatika.7 Haya yalionyesha wazi kwamba alikuwa hakujizatiti au hakujiandaa kwa vita, bali alikuwa amekwenda tu kupigana katika shauku yake ya kumsaidia Husein.

Umar bin Sa’d bin Nufayl al-Azdi alipiga dharuba kwenye kichwa cha al- Qasim kwa kutoka kwenye farasi wake. Husein alikwenda haraka sana kumsaidia al-Qasim na akakikata kiganja cha muuaji kutoka karibu na kiwiko kwa upanga wake. Jeshi la adui lilimshambulia Husein ili kumwokoa muuaji wa al-Qasim, lakini walifanya hivyo katika mtindo usio wa mpangilio hivyo kwamba ikawa kwa kweli ni kumkanyaga kanyaga juu yake muuaji mpaka kufa.

Kisha kundi hilo likatawanyika, Husein akasimama kwa muda kidogo karibu na maiti ya al-Qasim, akiwa ameshikwa na huzuni isiyoelezeka. Kisha akaichukua (maiti hiyo) na kuipeleka mahali maiti ya Ali al-Akbar na maiti nyingine za ndugu zilipokuwa.

10. Abu Bakr bin Hasan aliuawa kwa mshale. Mama yake alikuwa Umm Is’haaq, bint ya Talha al-Tamimii.

11. Muhammad bin Ali bin Abi Talib alikuwa mdogo zaidi kuliko ndugu yake Muhammad bin al-Hanafiyya. Baada ya kifo cha Ali, alikaa na kuishi na ndugu (kaka) zake, Hasan na Husein kwa mfuatano, mmoja baada ya mwingine. Siku ile ya tarehe 10 ya Muharam alishiriki katika jihad hapo Karbala, na baada ya kuangamiza maadui wengi, na yeye aliuawa kwa kupigwa mshale. Kichwa chake kilikatwa na kikachukuliwa kupelekwa kwa Umar bin Sa’d.8

12. Abdallah bin Ali alikuwa mmoja wa watoto wanne aliowapata Ali kwa mama yao, Umm al-Bani Fatimah, bint ya Hizaam, ambaye alitokana na familia iliyofahamika kwa ushujaa wake. Watoto wengine watatu walikuwa. Abu al-Fadhl Abbas, mkubwa wao kabisa, Uthman na Ja’far, huyu wa mwisho akiwa ndiyo mdogo kabisa katika wao.

Abdallah bin Abi Mahl, mtu mkubwa wa Kufa, alikuwepo katika baraza la Ubaydullah bin Ziyad wakati Shimr alipoondoka kwenda Karbala, pamoja na barua ambayo iliandikwa kwa Umar bin Sa’d ikimwagiza kumuua Husein na sahaba zake kama wangekataa kutoa kiapo cha utii kwa Yazid. Abdallah bin Abi al-Mahl alipata kutoka kwa Ubaydullah bin Ziyad uhakikisho wa usalama kwa ajili ya watoto wa Umm al-Banin ambao wakati huo walikuwa hapo Karbala na Husein kwa vile mama yao alikuwa ana uhusiano wa kindugu naye, na aliipeleka dhamana hiyo ya usalama na ulinzi kwa Abbas na ndugu zake kupitia kwa mmoja wa watumwa wake.

Ndugu hao wanne, hata hivyo walimwambia mjumbe huyo kwamba wao hawakuhitaji kibali cha Ibnu Ziyad kwa ajili ya usalama (wao), na kwam- ba usalama na ulinzi wa pekee wa Mwenyezi Mungu ulikuwa unatosha kwa ajili yao.
Shimr alitokana pia na familia hiyo hiyo kama Umm al-Banin, na baada ya kuitoa barua ya Ubaydullah bin Ziyad kwa Umar bin Sa’d alikutana (alionana) na Abbas na ndugu zake kuwaambia kwamba wamepatiwa dhamana ya usalama. Wao waliukataa ulinzi huo kwa dharau kwani haukumjumlisha Husein.9

Katika siku ya 10 ya Muharram, Abbas aliwapeleka ndugu zake kwenda kupigana kwa ajili ya Husein kabla ya yeye mwenyewe hajaenda kujitoa mhanga maisha yake. Abdallah ambaye alikuwa mkubwa baada ya Abbas aliingia kwenye medani ya vita na baada ya mapigano makali sana alikutana na kifo cha kishahidi.

13. Uthman bin Ali aliitwa hivyo kwa sababu Uthman bin Maz’un aliyekuwa sahaba mkubwa na maarufu wa Mtume, alikuwa rafiki wa Ali binafsi. Alipigana kwa ajili ya Husein na alianguka chini akiwa amejeruhi- wa na mshale. Kisha aliuawa kwa kukatwa kichwa.

14. Ja’far bin Ali alishiriki katika vita vya Karbala baada ya Uthman bin Ali na aliuawa.

15. Abu al-Fadhl Abbas alizaliwa katika mwaka wa 26 A.H, na alikuwa na miaka kumi na nne, wakati Ali alipouawa kishahidi. Kisha Hasan alichukua jukumu la kumlea, na baada ya kifo cha Hasan katika mwaka wa 50 A.H, Abbas alitumia maisha yake na Husein. Alikuwa na umri wa miaka 34 wakati matukio hayo ya kuhuzunisha ya Karbala yalipotokea.

Abbas alikuwa maarufu kwa uzuri, madaha, urefu, nguvu na ushujaa na alikuwa akiitwa Qamar (mwezi mkamilifu wa ukoo wa Hashim). Husein alimfanya kuwa mshika bendera wa jeshi lake dogo, Abbas aliishika bendera hiyo juu sana kwa ushujaa usio wa kawaida na kwa heshima maalum.

Upendo wake mkubwa na utii kwa Husein ulimfanya amfuate Husein katika medani ya vita kama kivuli chake. Wakati wafuasi wengine na ndugu wa Husein walipokuwa wamekwishakufa kama mashahidi, Abbas alisimama peke yake mbele ya ndugu yake kumlinda. Alipoyaona maisha hayavumiliki alimwomba Husein ruhusa ya kupigana. Ruhusa ilitolewa kwa shingo upande, na Husein alimtaka atafute maji. Abbas alichukua kiriba cha maji na alikwenda kufuata mto. Alifanikiwa kupigana kujipatia njia yake kumfikisha mtoni na akakijaza chombo chake na maji.

Yeye mwenyewe alikuwa na kiu kali sana, iliyopita kiasi na akachukua maji mkononi na kuyaelekeza midomoni kama anayetaka kuyanywa, lakini alikumbuka kiu kali aliyonayo Husein na watoto wake, mara moja aliy- atupilia mbali maji hayo, na asijaribu kuonja hata lau tone moja.

Akiwa amekibeba kiriba cha maji kwenye mabega yake alitoka kule mtoni na kuelekea kwenye kambi ya Husein. Adui sasa akajizatiti kwa bidii zao zote katika kuzuia hata tone moja la maji kumfikia Husein. Kwa hiyo, wao walimzunguuka Abbas ambaye alikuwa ameelemewa na kile kiriba cha maji ambacho kimening’inia kwenye mabega yake na bendera ya jeshi la Husein ikiwa katika moja ya mikono yake.

Hata hivyo, Abbas alifanya mashambulizi ya nguvu sana kwa maadui ili kujinasua kutoka kwenye kundi hilo hasimu lakini Hukayn bin Tufayl alimkata mkono wake. Ili aweze kuilinda heshima na utukufu wa bendera hiyo, Abbas aliihamishia kwenye mkono wake wa kushoto ambao nao pia, muda mfupi baadaye ulikatwa na Zayn bin Warqa al-Juhni.

Abbas alijitahidi kuishikilia bendera ya jeshi lake kwa kutumia kifua chake kuikandamiza kwenye mgongo wa farasi wake wakati dharuba moja iliyopigwa kwa kutumia kirungu ilipomwangusha chini ardhini. Wakati Husein alipomfikia Abbas alikuwa katika pumzi za mwisho, anakaribia kufa.

Imeelezewa na Ali bin Abi Talib katika Nahjul-Balaghah kwamba Mtume wa Waislam alikuwa akitumia kuwaweka watu wa nyumba yake na familia katika mstari wa mbele wa vita katika nyakati za hatari, akiwatumia wao kama ngao kuwakinga masahaba zake.

Kuachwa kwa kanuni hii kulifany- wa katika vita vya Karbala. Wafuasi wa Husein na marafiki walijitosa wao kwanza katika kupigana vita na maadui na kuupata utukufu wa ushahidi. Walifuatiwa na ndugu wa Husein, na mwisho wa wote alikwenda Husein, na kupigana hiyo vita takatifu.

Sababu za kuachwa kanuni hii zinaweza kugunduliwa kwenye tofauti kubwa iliyopo kati ya matokeo yaliyotegemewa ya vita vya Karbala na matokeo ambayo yangeweza kutarajiwa kibusara ya vita vilivyopiganwa huko nyuma.

Katika vita nyingine zote, ilitegemewa kwamba baadhi ya washiriki wangebakia salama na hai katika mwisho wa mapigano hayo. Kwa hiyo, ili kuhakikisha kwamba wengi wa wale ambao walibakia sala
ma na bila kuumizwa walikuwa Masahaba wake, Mtume aliwatumia ndugu au jamaa zake kukabiliana na hali zilizo za hatari sana. Siku ya 10 ya Muharram, kila mmoja katika wafuasi wa Husein, wapenzi na ndugu wote kwa pamoja, walijitolea kukabiliana na kifo, na hakuna swali (au hoja) lililojitokeza juu ya jamaa wa Husein la wao kupelekwa kwanza kupigana kuwanusuru wapenzi wake. Hali zilizokuwepo hapo

Karbala zilikuwa za namna kwamba dakika baada ya dakika majaribu ya wapenzi na jamaa wa Husein, na kwa kweli, majaribu ya Husein mwenyewe, yaliongezeka kwa ugumu na joto lenye kuongezeka na mateso ya kiu.

Imam Husein alikuwa na imani ya dhahiri katika uthabiti na uaminifu wa wafuasi wake na ndugu zake, hata hivyo hakulichukilia kwamba ni jambo jema kuwahatarisha kwenye mitihani mikali kama kuwawekea mikazo inayozuilika kwenye uwezo wao wa kustahimili. Ilikuwa kwa hiyo, ikieleweka kwamba angepaswa kuamua kuwatoa kwenda kupigana kwa utaratibu ule alioutumia, kwa utambuzi kamili wa uwezo wa uvumilivu wao, na wake yeye mwenyewe.

Ingekuwa ni jambo rahisi vya kutosha kwa Husein kuyatoa mhanga maisha yake mwenyewe kwanza kabisa katika njia ya haki.

Muhanga huu usingekuwa na daraja la juu zaidi kuliko mhanga, tuseme wa Kristo, ambaye kwa mujibu wa Wakristo alisulubiwa kwa sababu ya kutangaza na kueneza imani (dini) ya kweli, au mhanga wa Socrates ambaye alikunywa sumu kwa kutetea kanuni zake.

Heshima maalum na umuhimu wa mhanga wa Husein vilitokana na ukweli kwamba alivumilia mhanga wa kila mmoja wa wafuasi na wapenzi wake na ndugu zake mbele ya macho yake mwenyewe.

Kutengana kwa mtu na wafuasi wake waaminifu na vipenzi wa zamani, mmoja baada ya mmoja, wakiondoka daima dawamu, kuwaona wapwawe vijana na wazuri wa kupendeza wakiuawa kwa ukatili sana, kushuhudia mtotowe mtanashati na mwenye kuleta matumaini katika maisha akichomwa mkuki na kukatwa katwa mpaka kufa, na kumwona nduguye, mshika bendera wa jeshi la mtu huyo akilemazwa na kuuawa, kutaja tu mifano michache ya misiba yenye kuhuzunisha sana, ilikuwa ni majanga ambayo kwamba kila moja yao (katika hayo) lilikuwa lisilovumilika zaidi kuliko kifo chake mwenyewe mtu.

Tendo kubwa la kumvika taji halikuwa lile tu kwamba alijitolea mhanga maisha yake katika njia ya haki, bali kwamba, kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu, ndiyo alitoa mihanga, mmoja baada ya mwingine ya watu ambao walikuwa vipenzi sana kwake kuliko maisha yake mwenyewe na kwamba alijizuia kule kutoa muhanga maisha yake binafsi mpaka alipokuwa amepitia mkasa wote huu wa kusikitisha. Hakuna mwingine tena anayeelekea kuwahi kupata daraja hii ya juu ya subira na uvumilivu. Je, Husein angeweza kutegemea hayo kwa yeyote yule ambaye angemwacha afe baada yake yeye?

16. Abdallah bin Husein, anayefahamika zaidi kama Ali-Asghar, (Ali mdogo), kitoto kichanga alikuwa katika mikono ya baba yake, Husein wakati mshale uliotupwa na adui ulipomuua.10
Kwa mujibu wa hadith nyingine Husein alikuwa amemnyanyua mikononi mwake wakati wa msisitizo wa Umar bin Sa’d, Harmala bin Khalid al-Asadi alipotupa mshale uliolengwa kwa mtoto huyo asiye na hatia, ukamchoma na kumuua.

Tendo hili la ukatili uliovuka mpaka lililoelekezwa dhidi ya mtoto mchanga asiye na hatia limekutana na shutuma nzito sana kutoka kwa watu ulimwenguni kote, bila kutofautisha itikadi au umbali wa nchi. Liliwaanika kwenye aibu ya kudumu milele, wale maadui wa Husein kama watu ambao wamezima misisimko yote ya dhamira, hisia zote za kibinadamu na wakajiachia wenyewe, kwa ajili ya kupenda mamlaka ya kilimwengu (kidunia), kushushwa hadhi hadi kwenye daraja za chini zaidi kuliko zile
za wanyama.

  • 1. Tabari cha II, uk. 256-257.
  • 2. Al-Irshad, uk. 358.
  • 3. Tabari cha II, uk 356; Irshad, uk. 358.
  • 4. Tabari cha II, uk. 357.
  • 5. Tabari cha II, uk. 357.
  • 6. Al-Irshad, uk. 359.
  • 7. Tabari cha VI, uk. 256; Irshad, uk. 253-254.
  • 8. Tabari cha VI, uk. 257
  • 9. Tabari cha VI, uk. 237; Irshad, uk.242.
  • 10. Tabari cha VI, uk. 257; Al-Akhbar al-Tawel, uk. 255; Irishad, uk. 154.