Table of Contents

Sura Ya 33: Haiba Na Mafanikio Ya Husein Yahakikiwa

Mihanga yote katika kuutetea ukweli na haki kabla ya masaibu ya Karbala ilifanywa na watu binafsi wakitenda wao peke yao, kama Zakariyya na Yahya, na wajumbe wengi wengine wa Mwenyezi Mungu pamoja na Kristo ambaye kwa mujibu wa Wakristo, alisulubiwa, au kama vile Socrates ambaye alikunywa kikombe cha sumu.

Mihanga iliyotolewa hapo Karbala ilitofautiana vikubwa sana na mihanga mingine yote kwani hiyo ilitolewa na kundi la wanaume na wanawake na watoto ambao kwamba wanaume walitoa maisha yao baada ya kuvumilia mateso yasiyoelezeka na wanawake na watoto walilazimika kupatwa na mateso yasiyovumilika na dhiki iliyofuatana na umateka.

Wanaume na wanawake na watoto hawa walitokana na makundi ya umri wakati mwingine yakitengana kwa mbali sana kati ya moja na jingine, na idadi yao ilizidi mia moja, na miongoni mwao, mbali na watu huru mara nyingi walikuwa wakutwe humo watumwa, Waarabu na Waturuki, Wahabeshi na Waajemi, waliotokana na tabaka zote zenye kuheshimika za jamii. Hawakuwa na mahali pa kukutana pamoja kati yao isipokuwa umoja wa lengo.

Bila shaka watu wengi mno kwa hiari na kwa uamuzi unaojieleza na uchaguzi waliunganisha mawazo yao, fikra, nia zao, malengo yao na sababu zao za utendaji katika zile za kiongozi wao Husein. Kwa hiyo, ni sawa kabisa kusema kwamba ulimwengu hauna kiongozi na haku- na baraza la watu wa kuonyesha ni nani ambaye angeweza kufanana hata kwa kidogo sana na Husein na wafuasi wake.

lazima ionekane kuwa si wa namna nyingine isipokuwa nzuri ajabu, kwamba ubora wa uongozi wa Husein ulikuwa kiasi kwamba alipokea utii mkubwa wa dhati kutoka kwenye idadi kubwa ya wafuasi wake, ambao waligawanyikana katika jinsia, umri, asili, usuli na hali ya kijamii kiasi kwamba hakuna mfano hata mmoja uwezao kutolewa, wakati yeyote kati ya wafuasi wake angeelezea hisia yoyote ile ambayo ingewaza kuwa na mwelekeo japo mdogo kabisa wa kwenda kinyume na mawazo au fikra zake yeye mwenyewe (a.s.).

Ni jambo la ajabu ya kipekee kwamba wakati ambapo Husein alitoa hotu- ba nyingi kwa maadui zake akiwashawishi waache kumwonea, hakuwahi kuongea hata mara moja na rafiki na ndugu zake kuwasihi wamsaidie. Hasha, kinyume chake aliitumia kila fursa akijaribu kuwazuia wasiungane naye, wakati wao hawakupoteza nafasi yoyote ya kumuelezea hisia zao za nguvu kabisa za upendo.

Kwa njia ya mfano wake mwenyewe wa dhamira isiyobadilika ya kudumisha ukweli na haki, Husein aliwafundisha wafuasi wake kiakili kufuata njia ya wema na kutetea kweli na haki kwa ajili yao wenyewe na kujitoa mhanga maisha yao kwa ajili ya malengo haya. Kwa hiyo katika vita vya Karbala, kila mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Husein alijitokeza mbele kwa hiari yake mwenyewe kukutana na mauti akiyaangalia moja kwa moja machoni, wakati wote akiwa na imani juu ya haki na uhalali wa sababu yake.

Utiaji fora usiokifani wa haiba ya Husein. Husein angeteuliwa kwa ubora wa sifa kama angetoa sauti yake pekee dhidi ya Ukhalifa wa Yazid baada ya kuwa umekubalika kwa watu wengi, lakini alipanda kwenye utukufu wa juu zaidi, wakati aliposisitiza changamoto yake (upinzani wake) na akayakabili makundi makubwa na mengi ya Yazid.

Husein angepata cheo cha juu sana cha shahidi kama baada ya kupitiwa na mitihani yake yote, angejitoa mhanga maisha yake yeye mwenyewe tu. Bali alipanda kwenye vilele vya ushahidi visivyoweza kufikiwa, kwa mhanga wa wafuasi wake wote watiifu, vipenzi wake wakubwa na ndugu zake wa karibu kabisa na muhanga wake yeye binafsi pale Karbala.

Husein angekuwa kiongozi wa watu asiyeshindikana kama, katika mazingira ya kukatisha tamaa, yenye kuvunja moyo na yenye kutisha mno ambayo alijikuta akiwa ndani yake pale Karbala angeliweza kuwabakiza wafuasi wake na kuwa pamoja naye kwa kuwahutubia hotuba nzito zenye kutia hamasa kubwa.
Kwa hakika alipanda kwenye utukufu wa juu zaidi, usio na kifani kwa kutumia kila fursa kuwashauri vinginevyo sahaba zake ili wasifuatane naye na kakutana na kifo kilicho hakika. Ustahiki wake mwenyewe na dhamira thabiti ya kutetea ukweli kuliacha alama hai katika akili za wafuasi wake, kiasi kwamba kila mmoja wao alipata thibitisho la uimara wake mwenyewe na uamuzi.

Husein angebakia kutolinganishika kama angekikaribisha kifo kabla ya wafuasi wake na ndugu zake wakiwa hawajauliwa. Alipata daraja la juu zaidi la mafanikio kwa kuziongezea juu ya huzuni zake, kule kuhudhuria kunakovunja moyo, yale mauaji ya sahaba zake wapenzi wote na ndugu wa karibu.

Husein aliongeza sifa yake ya kiroho kwa kutekeleza bila kutetereka, kila fundisho la Uislamu na kila wajibu ulioamriwa na Uislamu hata wakati alipokabiliwa na mateso yenye kuumiza sana.

Alitenda kufuatana na hali ya kupenda usawa ya Uislamu kwa kuzibeba maiti za watumwa ambao walijitoa mhanga maisha yao kwa ajili yake kwa namna (heshima) ile ile kutoka kwenye medani ya vita kama alivyobeba za wale sahaba zake wapenzi mno na ndugu wa karibu.

Alisimamisha Sala za mchana (Adhuhuri na al-Asri) katika wakati uliopangwa hata wakati vita ilipokuwa imefikia ukali wake kabisa. Husein alikuwa anatekeleza jihad na mara moja akifanya lengo lake lifahamike kwa uonyeshaji wa kivitendo.

Umaarufu wa Husein ungebakia usio kifani kama jihad yake ingemalizika kwa kujitoa mhanga wapenzi wake na ndugu, na mhanga wake mwenywe. Aliongezea kwenye umaarufu wake kwa kuwachukua pamoja nayewanawake na hata watoto wa familia yake kwenda nao katika safari yake ya Iraq - dhidi ya ushauri wa wapenzi wake ambao walijali sana kutoa maoni yao katika jambo hili.

Kwa njia hii aliandaa utangazaji wa lengo la kufa kwake kishahidi katika namna ambayo hakuna mtu mwingine yeyote ambaye angeweza kufanya hivyo, kwani kila mmoja katika wao alikuwa na utambuzi wa kina kabisa juu ya wajibu wake na kushikilia ukweli hivyo kwamba, hata katika baraza la Ubaydullah bin Ziyad kule Kufa, na lile la Yazid hapo Damascus, hakuna hata mtu mmoja miongoni mwa watu wa Husein waliopona vita aliinamisha kichwa chake mbele ya utawala wa Bani Umayyah na dharau aliotupiwa Yazid na Husein ilidumishwa baada ya kifo chake, siyo tu na Ali bin Husein, Zainab na Umm Kulthumu, bali pia na watoto kama vile Sakina na Muhammad bin Ali ibn Husein.