Table of Contents

Sura Ya 40 : Kuanguka Kwa Bani Umayyah.

Kihistoria ni kweli kwamba wakati watu wowote wapatapo lile daraja la utawala ambalo huwapatia wale walioko kwenye uongozi wa mambo yao, siyo tu mahitaji ya maisha bali pia na wingi wa mambo ya anasa, wanakuwa mawindo ya kupenda starehe, roho mbaya, ubinafsi na umimi, na kutaka kuona mbele na kuchukua njia yenye walau upinzani mdogo kabisa. Matokeo yake wanakuwa waoga.

Bani Umayyah walishindana na wafalme wa Roma na Uajemi katika mali (utajiri) na fahari na katika kadiri ya milki zao za nchi wanazozitawala. Kuangamia kwao kuliharakishwa na Yazid, ambaye alimuua al-Husein, bila ya kujali utukufu wake wa kiroho na ile nguvu yake isiyoshindika ya uadilifu.

Yalikuwa ni yale mauaji ya kikatili na kidhalimu ya Husein ambayo yalimpa Abdallah bin Zubeir kisingizio cha kupinga mamlaka ya Yazid, akawageuza wakazi wa Madina ambao hapo awali walikuwa ni watu wasiojishughulisha wakawa dhidi yake Yazid, akashawishi lile kundi la wenye kutubia makosa yao kuanzisha kampeni ya nguvu ingawa isiyo na mafanikio, ya kulipiza kisasi kwa wauaji wa Husein, akamchochea al-Mukhtar kujiingiza katika idadi ya mapigano ili kuwauwa wauaji wa Husein, akamsukuma Zayd bin Ali bin al-Husein katika mwaka wa 112 A.H. kuasi dhidi ya Bani Umayyah, na kuacha nyuma kundi ambalo kisiasa lilikuwa na madhara sana kwa Bani Umayyah, ingawaje yeye mwenyewe hakufanikiwa (katika kampeni hizo).

Mwishowe, ilikuwa ni hamu hiyo hiyo ya kutoa adhabu kwa umwagaji wa damu ya al-Husein ambayo iliwasaidia Bani Abbas kuwaangamiza na kuwatokomeza kabisa Bani Umayyah.

Baadhi ya vyama hivi vilikuwa vya kisiasa hasa kwa asili ambayo dhuria ya a-Husein, wenyewe walijitenga navyo kabisa.

Wakati Abu Muslim al-Khurasani aliposiamamisha bendera ya uasi dhidi ya Bani Umayyah pale Marv na lengo lililotangazwa la kulipiza kisasi kwa mauaji ya Husein, maelfu ya watu walikusanya nguvu kumsaidia na mfalme wa mwisho wa Bani Umayyah, Marwan bin Muhammad aliuawa katika vita vya Zab 1 na pamoja naye mamlaka ya Bani Umayyah yakaangamia kabisa.

  • 1. Tabari, juz. 9, uk. 136.