Table of Contents

Sura Ya 41:Utawala Wa Bani Abbas.

Madai ya Ukhalifa yaliyotolewa na kizazi cha Abbas, ami yake Mtume, kwa ajili yao wakati fulani baada ya mauaji ya Husein pale Karbala na kufuzu ambako kuliambatana na jitihada za Abu Muslim al-Khurasani katika kuyatanguliza mbele maslahi ya Bani Abbas na kuzitenganisha huruma za Waislamu kwa Bani Umayyah kulitegemea hasa zaidi hisia za upendo wa watu juu ya watu wa nyumba ya Mtume.

Ingawaje uvaaji wa nguo nyeusi uliofanywa na Bani Abbas haukuhusika na kuonyesha sura yoyote ile ya huzuni juu ya kuuliwa kwa Husein pale Karbala, wale ambao hawakujua ukweli halisi walilifikiria hilo la uvaaji wa mavazi meusi kuwa ni udhihirisho wa huzuni kwa kuuawa Husein.

Maoni haya yalitiwa nguvu na lile jambo la kwamba, ilikuwa ni tarehe 10 ya Muharram mwaka wa 132 A.H wakati ambapo, baada ya mauaji ya khalifa wa mwisho wa Bani Umayyah, Marwan, Bani Abbas na wafuasi wao, wakiwa wamevalia mavazi meusi, walikusanyika katika msikiti wa Sala za jamaa mjini Kufa.

Kwa kweli kundi hili lilikusanywa pamoja hivyo ili kuomboleza juu ya kifo cha muasisi wa kundi hilo, Muhammad bin Ali bin Abdallah bin Abbas1 na kuuawa kwa Ibrahim bin Muhammad2 kiongozi wa kundi hilo ambaye pia alikuwa mtoto wa muasisi huyo.

Watu walikuwa wamevutiwa na kundi hilo kwa kukumbuka sifa bora na madai ya watu wa nyumba ya Mtume kwenye Ukhalifa. Kiapo cha utii ambacho kilikuwa kikitumika kuchukuliwa kutoka kwa watu na waeneza propaganda wa Bani Abbas kilikuwa si kwa mtawala yeyote yule kwa kutajwa jina. Ilikuwa ni katika mpango ufuatao: “Nachukua kiapo cha utii kwako kwa kukitii Kitabu cha Allah, Sunna za Mtume na mtu atakayeidhinishwa na watu wa Nyumba ya Mtume.” 3

Wakati mnamo mwezi 11 ya Muharram mwaka wa 132 A.H. pale utawala wa Bani Hashim (yaani Bani Abbas) ulipotangazwa, Abu Salama Hafs bin Suleiman, rafiki wa watu wa nyumba ya Mtume aliteuliwa kuwa waziri, na Abu Muslim al-Khurasani aliitwa “Muaminiwa wa dhuria ya Mtume.”4

Dhuria wahusika wa Mtume walijua kwamba jina lao lilikuwa likitumiwa kuhusiana na kundi hilo kwa sababu tu ya kutumikia malengo ya kisiasa. Matokeo yake, wakati barua ya kumpa Ukhalifa ilipopokelewa na Imam Jafar as-Sadiq aliichoma moto hapo hapo, akisema kwamba watu wa Khurasani walikuwa siyo Shi’a (wafuasi) wa Ali wa kweli, na kwamba Abu Salama alikuwa amedanganywa na hivi karibuni atauawa.5

Muda mfupi tu baada ya kupanda Abu al-Saffah Abdallah ibn Muhammad ibn Ali ibn Abdallah ibn Abbas kwenye Ukhalifa, Abu Salama akauawa6 na baada ya al-Saffah, dhuria wa Mtume walipokea kutoka kwa Bani Abbas, utendewaji mbaya na wa kila mara ulio sawa na uleule waliokuwa wakitendewa na Bani Umayyah. Hata hivyo mambo haya hayabadilishi ule ukweli wa kwamba Bani Abbas walipanda madarakani juu ya wimbi la chuki dhidi ya kuuawa Husein

  • 1. Al-Akhbar al-Tiwal, uk. 324.
  • 2. Ibid, uk. 243.
  • 3. Tabari, juz. 9, uk. 99.
  • 4. Tabari, juz. 9, uk. 142.
  • 5. Al-Wuzar Waal Kuttub, uk.57.
  • 6. Ibid, uk. 60.