Table of Contents

Sura Ya 42:Mabadiliko Ya Fikra.

Lengo la haraka la Husein siyo kuangamiza mamlaka ya Bani Umayyah au utawala wa Yazid kiyakinifu, kwani mafanikio ya lengo hilo yangehitaji msaada wa kutosha kijeshi na vifaa vingine vya kimaada. Yeye alijaribu kufungua uwanja mpya wa mapambano, kuzifanya kifra za watu kuwa shabaha ya mashambulizi yake.

Alipendelea kuanzisha mapinduzi ya kiroho. Majeshi ya Yazid yangeweza kumuua Husein; wasingeweza kwa vyovyote vile kuangamiza (kuua) yale mawazo ambayo Husein aliwataka watu wayachukue kutokana na mfano aliouanzisha yeye.

Qur’ani inawaelekeza Waislamu kumtii Allah, Mtume na kuwatii watu wenye mamlaka miongoni mwao. Wengi mno katika Waislam humtambua Khalifa kama mtu aliyeko katika madaraka ambaye wao wanalazimika kumtii. Mamlaka fulani ya kufanya kanuni za kidini yamekubaliwa pia kwa Khalifa kuwa nayo. Kwa hiyo, mwenendo wa kila

Khalifa lazima uwe umekubaliwa kama ni sahihi, lakini Waislam walio wengi, isipokuwa Shi’a ambao hawaikubali kabisa mitindo iliyokubalika kwa jumla ya utawalishaji wa Makhalifa kama imethibitishwa na kuhalalishwa, wanawa- gawa makhalifa katika tabaka mbili, ‘makhalifa waongofu’ na ‘wengineo.’

Kuzungumzia kwa jumla, Ukhalifa wa Ali, na kipindi cha Ukhalifa wa Hasan kabla ya mkataba wake na Mu’awiyah vinachukuliwa kukifunga kipindi cha Makhalifa waongofu. Mu’awiyah, Yazid na Makhalifa wengine pamoja na Makhalifa wa Bani Abbas wanachukuliwa kuwa ni mbali na Makhalifa waongofu.

Tofauti hii miongoni mwa Makhalifa na kuwashusha chini wengi mno katika wao lazima kuchukuliwe kama ni matokeo ya changamoto ya Husein na namna maalum ya Jihad.

Baada ya upinzani imara wa Husein hapo Karbala, ilikubaliwa kuwa ni mpango wa kudumu kwamba hakuna Khalifa aliyekuwa na mamlaka ya kutunga sheria za kidini, na kwamba alikuwa ni mwenye kupata dhambi kwa matendo yake maovu kama vile Mwislamu mwingine yeyote yule, au hata pengine zaidi.

Hali kadhalika iliamuliwa kwamba wajibu wa utii kwa mtu huyo aliyeko madarakani kwa wakati huo uliendelea tu na kufikia mahali ambapo uasi na uvunjaji wa lengo la Mwenyezi Mungu ulikuwa hauhusiki, na kwamba wakati uridhishwaji wa sheria ya Mwenyezi Mungu uliwezekana tu kwa kumpinga mtu yule aliyeko katika madaraka, ilikuja kuwa ni wajibu kwa kila mtu kujiandaa kutoa upinzani kwake kama ilivyoamriwa na Allah.

Fikra ya kumfuata mtawala kibubusa bila kujitambua kama ng’ombe vipofu wenye kuswagwa hali ambayo ilikuwepo mpaka mwaka wa 60 A.H ilibadilishwa kutokana na matokeo ya kujitoa mhanga maisha yake Husein, kwa hali ya mtu kuyatambua majukumu yake na haja kuziwajibisha serikali za kidhalimu, ili kwamba kuanzia hapo hakuna serikali iliyokubali yenywe kujitia kwenye usingizi wa kuridhika kizembe.

Uvumilivu wa Husein na uimara ulikuwa ni mfano wa kukumbuka katika misiba yote, na umefundisha umadhubuti na ushupavu kwenye nyoyo zenye kuyumbayumba. Katika mwaka wa 71 A.H, majeshi ya Mus’ab bin al-Zubeir yaliogopeshwa na kuwekwa katika hali ya mvurugiko; wakati Abd al-Malik bin Marwan alipomshambulia Mus’ab akiwa na jeshi kubwa zaidi. Mus’ab alimtaka Urwa bin al-Mughira bin Su’ba kumweelezea namna gani Husein alivyokataa kutii amri za Ubaydullah bin Ziyad, na vipi alivyokuwa amejiimarisha yeye kupigana vita vya jihad. Alipokwisha yasikia maelezo ya Urwa, ujasiri wa Musab ulirejea na akasoma shairi lenye maana:

“Watu wa familia ya Hashim wameweka mfano hapo Karbala ambao ni bora sana kwa watu wenye akili za kiungwana.” Kisha baada ya hapo alikabiliana na adui na akafa akiwa yungali anapigana.

Katika njia ile ile nguvu ya subira ilivyoonyeshwa, na ujasiri wa kutoa sura huria kwenye hisia za kweli za mtu zilizoletwa na Husein, zimekuwa tangu zama hizo ishara za hatari kwa tawala za kidhalimu na kiuonevu zenye kukandamiza, na ule ujumbe uliotolewa na Husein kwenye hisia za kibinadamu utabaki na kudumu milele na milele.