Table of Contents

Sura Ya 43: Matokeo Yenye Mafunzo.

Ingekuwa ni kuufanyia ukatili mtazamo wa Uislamu na ufahamu wake kwamba matokeo ya mhanga wa Husein uonekane umefungika pekee kwenye kundi lolote lile maalum la jamii ya binadamu. Faida inayotiririka kutokana na mhanga wake wanaweza wakaishirikiana wale wote ambao watapenda kujifunza kutokana nayo juu ya namna wanavyoweza kujichunga katika maisha yao. Faida ambazo zinaongezeka kwenye dini, ubinadamu na Uislamu kutokana na matukio ya Karbala zimetajwa hapa kwa ufupi.

Nguvu Ya Dini Na Imani Ya Kiroho Yaonyeshwa.

Uyakinifu na hali ya kiroho siku zote vimekuwa katika vita baina ya vyenyewe kwa vyenyewe. Dini inashikilia imani ya kiroho hata sasa ingawaje imani ya kiroho haiko katika mtindo katika ulimwengu wa leo. Vita vya Karbala vilikuwa ni vita vya dini dhidi ya uyakinifu (maslahi ya kidunia). Mbali na nguvu zake kubwa mno, jeshi la Yazid halikuweza kukipata kwa kutumia nguvu, kile kiapo walichokitamani sana kutoka kwa Husein, cha utii kwa ajili ya mtawala wake.

Katika majumuisho ya mwisho ilikuwa ni Husein ambaye, ingawa aliuawa na kushindwa kwa muonekano wa nje, ndiye aliibuka mshindi, na pamoja naye ilishinda imani ya kiroho.

Uthibitisho Wa Ukweli Wa Uislamu Na Uenezwaji Wake.

Alama moja muhimu ya ukweli wa dini ni ile subira ya kijabari na umad- hubuti ambao kwamba waanzilishi wake hukabiliana na shida na dhiki, na wanang’ang’ania kwenye misingi yao mpaka mwisho wa siku zao. Msaada uliotolewa kwenye dini yao na wafuasi wake wa kawaida wakikabiliana na dhiki kubwa kishujaa na wakijitoa mhanga maisha yao wenyewe usingeweza kuthibitisha kwa uhakika ukweli wa imani (dini) yao, kwani pengine wangeweza kuwa wamedanganywa au walikuwa pengine hawau- tambui ukweli wenyewe.

Lakini kama mwanzilishi wa dini, wasiri wake na watu wa familia yake ambao ni wajuzi wa ndani wa siri za maisha yake binafsi, na kwa undani wa karibu sana wameizoea hali ya maadili yake na sifa zake nyingine, wanakubali kukabiliana na mitihani katika kuunga mkono kanuni na misingi yake, na kama ni lazima, kuyatoa maisha yao (Kufa) katika kuthibitisha uhalali wa kanuni za dini yake, ukweli wa misingi yake bila shaka yeyote utakuwa umethibitika.

Pamoja na al-Husein, wapenzi na wafuasi wake wote, na pia ndugu zake walijitoa mhanga maisha yao baada ya kupata mateso makali sana na ukandamizwaji.

Mhanga wa Husein haukumpata kwa kimya kimya. Aliendelea taratibu kuwalingania watu kwenye Uislamu wa kweli na halisi. Katika tarehe 9 ya Muharram, wakati adui aliposonga mbele dhidi ya Husein wakati wa jioni bila ya kutanguliwa tangazo kabla, aliomba kusimamishwa mapigano kwa usiku mmoja ili kwa usiku mmoja ili utumike tu katika maombi yake mwisho na Sala kwa Mwenyezi Mungu. Husein na wafuasi wake waliutenga usiku wote kwa lengo ambalo mapatano ya kusimamishwa vita yalikuwa yamekusudiwa.

Katika kufanya hivyo, walionyesha na kuthibitisha kwamba katika hali za mitihani mikali sana kanuni na misingi ya dini lazima izingatiwe na kwamba nguvu za kiroho ni bora kuliko nguvu zote za kilimwengu.

Bado hali ngumu zaidi ya mazingira ilikuwepo wakati siku ya tarehe 10 ya Muharram Husein alipoongoza Sala za mchana ndani ya uwanja wa vita katika mfululizo wa mishale baada ya watu wengi wa kundi lake dogo walipokwishauawa.

Haya yalikuwa maonyesho dhahiri ya ukweli wa mafundisho ya Kiislam ambayo yaliujaza ulimwengu kwa wito wa uzinduzi wa haki, uliamsha dhamira ya Waislamu, na kufichua ukatili wa Yazid na uadui wake kwa Uislamu.
Kila mtu wa kundi la Husein alikuwa kama mhubiri. Mashindano ya Burayr na Yazid bin Ma’qil na kuomba laana za Mwenyezi Mungu ishuke juu ya yeyote yule kati yao aliyesema uwongo, na khutuba za Zuhayr bin al-Qayn zinaweza kutolewa kutoka miongoni mwa idadi kubwa sana ya mifano ambayo ndani yake wapenzi wa Husein walizifafanua sababu ambazo zilimshawishi Husein kuchukua mwenendo ambao aliuchukua. Haina umuhimu kwamba jitihada hizi hazikuleta mafanikio ya haraka, kwani kazi ya mhubiri inahusu tu kuwaita watu kwenye kweli ya ujumbe wake hata katika mazingira yenye kuvunja moyo kabisa.

Mafundisho Ya Kimaadili Na Ya Kijamii Ambayo Yaweza Kupatikana Kutokana Na Masaibu Ya Karbala.

Sawia pamoja na kuwa ni yenye kusikitisha kupita kiasi, matukio ya Karbala si yenye kuleta maomboleza pekee. Yanaelekeza na kubadilisha ili kuupandisha uhai wa binaadamu katika daraja za juu sana za rehema na Ucha-Mungu.

Baadhi ya mafundisho makuu ya matukio ya Karbala yametajwa na kuelezewa kwa ufupi chini ya vichwa vya habari vifuatavyo:

Uhuru: Uhuru maana yake ni kuwa huru wa kutenda kwa mujibu wa inavyoamua dhamira ya mtu bila ya kizuizi chochote kile.

Miongoni mwa vizuizi kwenye uhuru wa kutenda ni mapenzi ya mtu juu ya starehe na vitu ambavyo starehe zinazoendelea umehatarishwa kwa kufuata maamuru ya dhamira ya mtu. Ukombozi kutokana na tamaa unakataa katakata nguvu zote za kidunia za kumfanya mtu mtumwa. Kwa kutenda kwa mujibu wa mwongozo wa dhamira yake, Husein alionyesha kujikomboa kwake kutokana na matamanio katika hali za taabu na dhiki zenye kutisha mno.

Kwa mujibu wa umuhimu ambao jitihada ya Husein zilitoa kwenye uhuru, raia wa nchi huru kwa kweli ni watumwa kama watafuata mambo maovu. Kwa upande mwingine raia wa nchi iliyofanywa utumwa wako huru kama mbali na kuteseka kwa ukandamizaji, wanafuata haki na kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Uimara: Ni uimara kama tu katika kufuata njia ngumu na ya hatari katika vitendo mtu kamwe hatasita wala kukwepa na atadumisha utulivu wake na ushwari. Katika kuzimiliki sifa hizi, mashahidi wa Karbala wanachukua nafasi ya mbele kabisa.

Husein alikuwa amekataa kuapa kiapo cha utii kwa Yazid baada ya kuchunguza undani wa roho yake, na baada ya kupima katika sehemu ya ndani kabisa ya akili yake zile hatari za hali hiyo, na baada ya kujiridhisha mwenyewe kwamba kwa ukubwa wowote ule wa makali ya mateso yake utakaoweza kutokeza, umadhubuti wa uamuzi wake usingetikisika. Wasaidizi wote wa Husein hapo Karbala, pamoja na watoto, walisimama imara katika kuupa athari upinzani uliodhamiriwa na Husein kwa Yazid.

Katika safari ya Husein kwenda Kufa, al-Hurr alikuwa amekutana naye na akiyatabiri mauaji ya Husein kama akishikilia kufuata mwelekeo wake wa kwenda Kufa, alimwomba ajionee huruma mwenyewe na auache mpango wake. Husein alijibu kwamba kifo kilikuwa si kitu kama mtu atakuwa amesimama katika haki. Hivi ndivyo, Ali al-Akbar bin Husein alivyowahi kueleza.

Maadui wa Husein waliijua nguvu ya azma yake. Mnamo siku ya tarehe 9 ya Muharram, Umar bin Sa’d alipokea barua ya Ibn Ziyad ikimuelekeza kwamba ni lazima apate kutoka kwa Husein kiapo cha utii kwa Yazid bila ya masharti au ampige vita.

Umar bin Sa’d mara moja akasema, “Husein kamwe hawezi kukubali kwa namna hii. Roho ya baba yake inadunda ndani ya kifua chake.” Na kila mtu aliona kwamba Husein, kama ukingo wa uimara na umadhubuti, alihimili gharika za mateso na maumivu ambayo yalikuwa yamemzunguka katika medani ya vita.
Kuandaa kundi: Umoja wa hisia, mawazo, malengo na vitendo vinahita- jika kwa ajili uandaaji wa makundi ya watu. Kufanya jambo kwa lengo moja, ambako kunaweza kuonyesha tabia ya kiongozi sio uhakikisho kwamba angejikusanyia wafuasi ambao wote kwa jumla watashirikiana naye katika sifa hii.

Tunazijua neema nyingi sana ambazo wana wa Israeli walizipata kupitia kwa Nabii Musa, lakini walipotakiwa kupigana kuika- mata Nyumba Takatifu (al-Bayt al-Muqaddas) watu wote isipokuwa wawili tu, walikataa kupigana na wafilisti. Yaliyomtokea Kristo hayakuwa mazuri zaidi.

Idadi ya watu ambao waliikubali imani (dini) mikononi mwake ilikuwa ni ndogo. Na alikuwa ni mmojawao aliyemsaliti na kumfanya akamatwe.

Biblia inatuambia kwamba Kristo aliwaambia wafuasi wake kusingekuwa na hata mtu mmoja miongoni mwao ambaye hangeangukia katika kutenda kosa kuhusu yeye. Mmoja wa wanafunzi wake wateule, Petro, alimkana Kristo mara tatu.

Wale wanafunzi wengine hawakutoa msaada wowote ule kwa Kristo na hawakushikilia kwenye njia ya haki. Hali kadhalika matukio kama hayo yalitokea katika Uislamu, na hayo pia ni katika wakati wa uhai wa Mtume.

Tukio moja la namna hiyo lililoelezewa katika Qur’ani linasimulia kuhusu vita vya Uhud, wakati walipopelekewa na Mtume chini ya uongozi wa Abdallah bin Jubayr kukilinda kinjia chembamba katika mlima wa Uhud na kwamba wasilitoke lindo lao hili kwa hali yoyote ile, walikiacha kinjia hicho bila ya ulinzi na wao walikimbilia kwenda kupora vitu vya adui aliyeshindwa, na hivyo wakasababisha Waislamu washindwe. Hata hivyo, wafuasi wa Husein hawakuonyesha dalili yoyote ile ya kuhitilafiana kwa maneno au kitendo toka kwa kiongozi wao katika vita vya Karbala.

Kujiheshimu: Uislamu uliitambua silika ya kibinaadamu ya kuokoa maisha na Qur’ani ikakufanya kujilinda kuwa ni jambo la wajibu pale iliposema, “Usiyaweke maisha yako hatarini.” Njia iliyoteuliwa na Husein kwa ajili yake mwenyewe kwa utekelezaji unaostahili wa majukumu yake ilikubaliana na kanuni iliyoelezewa na yeye mwenyewe kwa maneno, “Kifo ni bora zaidi kuliko fedheha na aibu,” na haya: “Kifo cha heshima ni bora zaidi kuliko maisha ya aibu.” Maneno haya ndiyo maadili ya hekima ya mbele kabisa, ya watu na mataifa ya ulimwengu yenye kujiheshimu. Kwa misemo mifupi hii, akiwa ameamriwa kwa utukufu wa akili na aliye- julishwa vyema juu ya kujiheshimu, Husein aliongeza uzito wa mfano wake mwenyewe na akaifikisha kwa walimengu kwa ujenzi wake wa maadili.

Subira: Sifa ya subira ilikuwa imehusishwa na Husein kwa ukamilifu kiasi kwamba anaitwa ‘Sayyid al-Swaabirin,’ yaani kiongozi wa wale wenye subira.” Ilikuwa siyo kwamba vinyume vya bahati visivyotegemewa vilimpata Husein na sahaba zake pale Karbala, ambavyo dhidi yake hapakuwa na fursa yoyote iliyopatikana, na ambazo zilikuwa kwa lazima zivumiliwe. Mateso yalichukuliwa kama hatari zilizokwishapangwa, kama maendeleo yakaribishwayo ili kwamba haki iweze kuwepo.

Ule ukweli kwamba Husein aliwapeleka wafuasi wake wote, wapenzi wake wote na ndugu zake wote kwenye uwanja wa vita, kuifanya kazi yao na hatimae kufa, bila ya yeye mwenyewe kushiriki katika mapigano; ulikuwa ni mfano, ambao ulisababisha daraja kubwa la subira, ambalo ni Husein peke yake tu aliyeweza kulionyesha. Hata hivyo, moyo huo ulichangiwa kikamilifu na masahaba wote wa Husein. Uhimizaji wa Abu al-Fadl Abbas kwa ndugu zake akisema, “Songeni mbele ili niweze kushuhudia kuuawa kwenu,” unaonyesha shauku hiyo hiyo ya kuteseka kwa kukubali kikamilifu kabisa.

Ushujaa: Ujasiri, kwa maana yake iliyo halisi, haihitaji tu kwamba mtu lazima apigane vita, wakati inapostahili kufanya hivyo, na halafu afanye kile ambacho wajibu ungemtaka kufanya, bila hata kujali matokeo mabaya sana, lakini pia kwamba mtu lazima afanye subira wakati kupigana kutakapokuwa hakustahili, na kutoonyesha papara na kutojali tu kungesaidia, hata ingawa njia kama hiyo ingejaa matatizo mengi.

Ni mwelekeo mmoja tu wa ushujaa wa Husein ambao ulionekana waziwazi hapo Karbala. Mwelekeo mwingine wa ushujaa wake aliuonyesha yeye mwenyewe mapema zaidi wakati alipokuwa akiendelea kuchunga kwa miaka kumi, yale masharti ya mkataba uliofanywa kati ya kaka yake Hasan na Mu’awiyah. Katika kipindi hiki kirefu cha wakati, matukio mengi machungu yalitokea lakini Husein aliyavumilia bila ya kufanya lolote la kuweza kufanya mambo kuwa mabaya zaidi katika hali ambayo tayari ilikuwa ni ngumu.

Ilikuwa ni pale tu alipolifikiria kuwa ni wajibu wake kuzitia changamoto na kupigana na nguvu za uonevu na udhalimu (ukandamizaji) kwamba Husein aliishinda hata milima kwa uimara na umakini.Vitendo vya ushujaa vilivyotimizwa na Husein na watu wake hapo Karbala vinawashangaza watu hata leo hii.

Ni ushujaa gani uliopita kiasi ulioonyeshwa na Husein na masahaba wake wakati waliposimamisha Sala zao za jamaa za wakati wa mchana katika medali ya mapambano ya Karbala wakati vita ilikuwa katika makali yake yaliyozidi mno na mishale ilikuwa inamiminwa kwa wingi juu yao na adui, hivyo kwamba mmoja wa masahaba wa Husein, Sa’idi bin Abdallah al-Hanafi, ambaye alisimama mbele yake kumkinga kutokana na mishale, alianguka chini akafa kutokana na majeraha mengi aliyopata kwa kupigwa mishale mingi katika mwili wake, mara tu Sala zilipomalizika!

Kujinyima: Kutoa umuhimu wa kwanza kwenye mahitaji ya wengine juu ya mahitaji binafsi ya mtu ina maana ya kujihini. Mifano mizuri sana ya sifa hii ilionyeshwa na Husein, na wasaidizi wake hapo Karbala. Husein alitoa funzo la kukumbukwa kuhusu kujinyima wakati alipokuwa njiani kuelekea Iraq, bila ya kujali hali zake mwenyewe za baadaye, aliyatoa maji aliyokuwa ameyahifadhi na kumpa al-Hurr na watu wake ambao walikuwa wanakufa kwa kiu, ingawaje walikuwa ni madui ambao walikuwa wamepewa kazi ya kumzuia kuendelea na safari yake ya kwenda Kufa.

Hapo Karbala, kila mmoja wa wafuasi wa Husein na ndugu waliambatanisha ubora wa kuyalinda maisha ya Husein kwa kulinganisha na maisha yao wenyewe kiasi kwamba walitenda kama vile tayari wamekwishaagana na uhai wao. Sa‘id bin Abdallah al-Hanafi kusimama kwake mbele ya Husein kumkinga kutokana na mishale kwa kipindi cha Sala za mchana kwa kweli ni mfano usiosahaulika na kujihini.

Kila mmoja wa wafuasi wa Husein alijaribu kujitoa mhanga maisha yake kabla ya wengine ili kuwaokoa, hata kama iwe kwa kipindi kifupi sana. Wote walitambua kwamba hakuna ambaye angebakia hai, lakini bado kila mtu alijaribu kuwawsalamisha wengine madhali yeye mwenyewe alikuwa bado yuko hai.

Abbas na ndugu zake, walipata ahadi mbili za usalama, moja kupitia kwa Abdallah bin Abi al-Mahall, mpwa wa mama yao, na nyingine kupitia kwa Shimr. Ahadi zote mbili zilikataliwa bila kuheshimiwa (zilipigwa mateke). Ilikuwa ni udhihirisho usiokuwa wa kawaida wa moyo wa kujitoa kukikaribisha kifo kwa ajili ya mtu mwingine wakati njia kuelekea kwenye usalama iko wazi kabisa. Ilikuwa ni kujihini kwa Husein na wafuasi wake kwamba, ili kuilinda dini na kuukoa ubinaadamu kutoka katika mateso ya kidhalimu, walijitoa mhanga kikamilifu kabisa hapo Karbala.

Ukamilifu katika maingiliano ya jamii: Katika hali ya ustawi na amani, kanuni za adabu za kijamii huwa kwa kawaida zinazingatiwa. Hata hivyo ilikuwa Husein pekee ambaye, akiwa katika ridhaa ya hali zenye kukatisha tamaa na mateso yenye kuzidi hapo Karbala, alifanikiwa kuyatimiza kabisa matakwa yenye kulazimu ya ukamilifu wa maingiliano ya kijamii kwa kutokuacha kamwe kuyaangalia madai ya yeyote yule kati ya wafuasi wake, wa mbalimbali kama wasaidizi, wapenzi, na ndugu, juu ya kujali kwake na huruma, bila kuonyesha upendeleo usiostahili kwa yeyote yule wala kukataa utambuzi wa mtu ambapo cheo na hadhi vilitoa uhalali wake.

Medani ya vita ilikuwa mbali kiasi kutoka kambi ya Husein. Kila wakati alipomruhusu mtu yeyote kati ya wasaidizi wake au marafiki kwenda kupi- gana, alikuwa akiyaangalia mapigano hayo, na pale askari wake alipo- jeruhiwa, Husein alikuwa akimtembelea. Ni lazima ilikuwa iwe ni vigumu mno kwa Husein kufanya matembezi kama hayo katika jua kali, kwa vile watu wake wote mwishowe walianguka wakipigana.
Katika nyakati zilizokuwa ngumu sana na za hatari ambazo Husein alikuwa anazipitia hapo Karbala, wakati akili ya mwanadamu inapoteza udhibiti wake juu ya ufanyaji kazi wake, ilikuwa ni mafanikio ya Husein kwamba aliyapatia uzingativu kamili majukumu ya kijamii. Katika tarehe

10 ya Muharram, zilikuja habari za kukamatwa kwa mtoto wa Bishr bin Amr katikia nchi (jimbo) ya Rayy. Husein alimwambia Bishr aende kum- saidia mwanawe apate kuachiwa. Wakati Bishr alipokataa kumwacha Husein, Husein alimtaka ampeleke mtoto wake mwingine, Muhammad, kwenda kumsaidia ndugu yake. Husein pia alitoa baadhi ya vipande vya kitambaa cha nguo chenye thamani sana kwa Bishr, ili kwamba bei ambayo nguo hiyo ingeipata, iweze kutumika kupata kuachiwa kwa mtoto wa Bishr.

Wakati yeyote yule kutoka miongoni mwa wafuasi wa Husein au ndugu alipoanguka chini kutoka kwenye farasi wake wakati wa Vita vya Karbala; yeye angemgutiakwa sauti Husein ambaye alifikiria kuwa ni wajibu wake kuijibu miito kama hiyo na kutoa msaada wote uwezekanao.

Pia alijitahidi kuhakikisha kwamba hakuna yeyote katika wafuasi wake waliokufa anakatwa kichwa na ni ukweli kwamba isipokuwa kwa wale ambao hawakumwita Husein, hakuna katika wafuasi wake aliyekatwa kichwa.

Husein alijaribu kuhakikisha kwamba maiti za wafuasi wake zinapata ile heshima iliyostahili. Wakati yeyote yule katika wao alipouawa, Husein kwa kawaida alifuatana na watu wengine ambao walipanga mipango ya uwekaji salama wa maiti ya mpenzi wao. hata hivyo, wakati ndugu wa Husein walipoanza kujitoa mhanga maisha yao wenyewe, kazi ya kuzichukua maiti zao kutoka kwenye medani ya vita na kuzipeleka kwenye hema lake ilimwangukia yeye mwenyewe Husein.

Al-Husein aliwafanya vijana wa ukoo wa Bani Hashim wahusike kwa kuichukua maiti ya Ali al- Akhbar kuipeleka kwenye hema lake kutoka kwenye medani ya vita na yeye mwenyewe aliibeba maiti ya al-Qasim kuipeleka kwenye hema. Husein hakupata nafasi ya kuzika mabaki ya watu wazima, lakini hakuacha kabisa kazi ya kuwazika waliokufa. Yeye mwenyewe aliizika ile maiti ya mtoto mdogo, Ali al-Asghar.

Kusema ukweli mtupu: Jitihada ya Husein kutoka mwanzo mpaka mwisho wa msiba wa Karbala ilikuwa ni kuelimisha na kuziweka sawa akili za watu juu ya dhana zote mbaya kuhusu matarajio yake, ili kwamba watu wasije wakamsaidia kwa sababu ya matumaini ya uwongo. Alikuwa akiwaambia watu kwa kukariri mara kwa mara ukweli kuhusu matarajio yake na kutangaza kwa kurudiarudia kwamba matokeo ya mwisho ya safari yake yangekuwa ni mauti. Wakati Husein alipojiandaa kuondoka Makkah, watu walijenga matumaini mema juu ya maisha yake ya baadaye, kwa vile Kufa ulikuwa miji mkuu wa Iraq na ulikuwa makao ya serikali ya Ali. Walifikiria utakuwa ni mji uliojaa wapenzi na marafiki wa Ali. Pia walikuwa wamesikia kwamba barua 129 zilikuwa zimepokelewa kutoka Kufa zikimwita Husein aende huko na kumwahidi msaada wa wakazi wa mji mpaka tone la mwisho la damu yao.

Walikuwa pia wamesikia kwamba watu 18,000 wa Kufa wali- ahidi kutoa kiapo cha utii kwa Husein mikononi mwa Muslim bin Aqil. Hali ya kawaida ya matumaini mema ilitawala kuhusu matarajio ya Husein hapo Kufa, lakini Husein alifikiria ilikuwa lazima kwamba watu hao waambiwe kwamba matumaini yao yalikuwa hayana ukweli wowote.

Siku moja kabla ya kuondoka Makkah, Husein alitoa hotuba ya kukumbukwa, alisema, “Kifo humfuatia mtu kama shada la maua lililozunguush- wa shingoni mwake… Mahali nipapendapo sana ni ile sehemu ambayo, katika kuuawa kwangu, nitaanguka hapo… Yeyote yule apendaye kujitoa mhanga maisha yake pamoja nami, na yuko tayari kufa, anaweza kufuatana nami.” Je, kunaweza kukawa na ushahidi mzuri zaidi wa kusema wazi wazi, ukweli na kuwa na tabia ya kunena bila ya kupendelea kuliko huo?

Baada ya Husein kuwa amekwishaondoka Makkah, baadhi ya makabila wahamaji na watu wengine mbumbumbu wasiojua walijiambatanisha kwenye msafara wake walipojua kwamba alikuwa anakwenda Iraq baada ya kupata mialiko kutoka Kufa.
Idadi yao ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba msafara mdogo ambao alikuwa ameuongoza Husein kutoka Makkah ulionekana kama jeshi.

Kwa mshindania madaraka fedhuli, kundi hili la watu lisiloalikwa lingekuja kama baraka, na angejitahidi kadiri ya uwezo wake wote kushikilia makubaliano nao kwa kutoa ahadi za uwongo na kuleta matumaini yasiyo na msingi. Hata hivyo, Husein hakuruhusu uele- waji mbaya huu kuendelea kwa urefu wowote wa muda.

Alipozipata bahari za kuuawa kwa Muslim bin Aqil na Hani bin Urwa hapo Kufa, alisimama mahali paitwapo Zubala, na akazitoa habari hizo za kusikitisha kwa msafara uliokusanyika, akisema, “Yeyote yule miongoni mwenu anayetaka kurudi nyuma anaweza kufanya hivyo, na mimi sita- mwajibisha juu ya hilo.” Baada ya maelezo haya wengi sana katika wau- mini wapya kwenye msafara wa Husein waliondoka wakaenda zao, wakiwaacha wachache tu, na wale ambao walifuatana pamoja naye kutoka Madina.

Kupinga vita na kuwa na subira: Amani na sera ya ‘kuishi na kuacha wengine waishi’ inaonyesha kwa neno la ‘Uislamu’ ambalo linapatikana kutokana na neno ‘salaam’ likimaanisha amani. Uislamu huwataka waumini wake wasisababishe madhara kwa wengine, wala kuchochea matatizo, wala kugombana na wengine bila sababu zinazostahili. Kanuni ambat- ani ya Uislamu ni kwamba batili na udhalimu kamwe visikubaliwe, na kwamba haki isiruhusiwe kuja kuwa huzuni kwa matokeo ya matendo ya mtu.

Kanuni hizi zilionyeshwa kwa mifano katika uhai wa Mtume, wa Ali, wa Hasan na wa Husein. Mfano usio kifani ulionyeshwa na Mtume wakati mkataba wa al-Hudaybiyya ulipofanywa. Mkataba wa Hasan na Mu’awiyah pia ni mfano mwingine. Husein aliitumia miaka ishirini ya maisha yake katika kuridhia kwa uvumilivu katika mkataba wa kaka yake na Mu’awiyah, miaka kumi wakati wa uhai wa Hasan na miaka kumi baada ya kifo chake, ingawa wakati wa kipindi hiki kirefu mambo mengi yalijitokeza katika uvunjaji kamili wa masharti ya mkataba ambao kwa machungu kabisa uliitahini mno subira ya Husein.

Wingi wa mbinu za Mu’awiyah kutaka mwanawe, Yazid awekwe visivyo halali kama khalifa baada yake haukumshawishi Husein kuchukua hatua kuzuia mipango ya Mu’awiyah. Hatua pekee ambayo aliichukua ilikuwa ni kukataa kutoa kiapo cha utii kwa Yazid. Kwani alifikiria kukataa kwake kwenyewe peke yake kungeeleza ukweli wa jambo hili kwa Waislamu kama walikuwa wameachwa na uwezo wowote wa upambanuzi na uelewa na kwa hali yoyote ile asingewekwa kwenye shitaka la kuunga mkono maovu na makosa.

Angeweza kujihisi hahusiki kuhusu vipi ulimwengu kwa ujumla unavyozichukulia jitihada za Mu’awiyah; angeweza kumkubali Yazid kama mfalme au khalifa, ili mradi tu haikumsumbua kuhusu masuala haya, na kama haikumhitaji kuapa kiapo cha utii kwa Yazid. Akiitambua kanuni hii yenye kuongoza ya maisha ya Husein, Mu’awiyah alifikiria hakuna ulazima wa kuchukua hatua kali dhidi yake kwa sababu alijua kwamba Husein angelishikilia amani, na kuendelea katika mwendo wa amani ilimradi hakulazimishwa kutoa kiapo cha utii kwa Yazid.

Wakati Yazid alipomrithi baba yake Mu’awiyah alikidai kiapo cha utii cha Husein kupitia kwa gavana wa Madina, al-Walid, ambaye alikuwa hana msaada wa kutosha wa kijeshi. Kama Husein angekuwa ameelekea sana (kutaka kutawala) labda angeweza kujiweka kama mtawala wa Madina. Hiyo, hata hivyo ingemaanisha umwagaji damu na maandalizi ya vita vya muda mrefu. Husein, kwa hivyo alichagua kuondoka Madina ili kukwepa kumwaga damu ya Waislam, na akaenda Makkah kuonyesha kwamba lengo lake lilikuwa ni kukwepa kushikilia batili, na pia kuokoa maisha yake na maisha ya wategemezi wake, kwani Makkah ilichukuliwa kutoa hifadhi na usalama kwa kila mtu.

Hapo Makkah, Husein hakufanya kitu kwa hali yoyote ile, bali kuonyesha kwamba alikuwa hana lolote lile isipokuwa tu nia kubwa mno ya amani. Abdallah bin al-Zubeir hakuchukuliwa kwa kuheshimika sana na watu wa Makkah kama alivyokuwa Husein kwa sababu ya uhusiano wa karibu wa Husein na Mtume.

Kama Abdallah bin al-Zubeir angeweza kukusanya pamoja jeshi lenye nguvu za kutosha kuiweka ile serikali iliyoanzishwa katika kushughulika na majaribio ya nguvu kwa muda mrefu, ingekuwa ni rahisi zaidi kwa Husein kuorodhesha askari wa jeshi lenye nguvu zaidi la kumuunga mkono. Hata hivyo, Husein alikaa kwa amani hapo Makkah wakati wote alipokuwa hapo.

Wakati watu wa Iraq walipotambua juu ya kukataa kwa Husein kutoa kiapo cha utii kwa Yazid, walimwandikia maombi 1200 na barua wakimwita kuja Kufa. Baadhi ya barua hizi pia zilipendekeza kwamba kama Husein angependa hivyo, watu wa Kufa wangemwondoa gavana mwenyeji na kumbadilisha wakamweka Husein, ambaye hakupendelea hata kidogo kulitia nguvu wazo hilo, na katika kujibu alisema,

“Imam (kiongozi) ni mtu yule ambaye hutenda kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, anafungwa na uadilifu, anaifanya haki kuwa kanuni na msingi wa maisha yake, na anajitolea binafsi kabisa kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu.”

Muslim bin Aqil ambaye alimtanguliua Husein kwenda Kufa alitoa ushahidi wa makusudio na malengo yasiyo ya kibinafsi ya binamu yake kwa kutenda kwa mwelekeo wa barua ya Husein, iliyonukuliwa sehemu yake hapo juu, alimradi hali ilimruhusu kufanya hivyo. Hakumwingilia kati kabisa Numan bin Bashir, gavana wa Kufa, au taratibu za serikali yake, hata wakati watu 18000 wa Kufa walipokula kiapo cha utii kwa Husein.

Yeye mwenyewe al-Numan alihisi kwamba tabia ya Muslim kwa upande wake ilikuwa siyo ile ya mpinzani, hivyo kwamba wakati vibaraka wa serikali walipomshtaki al-Numan na ulegevu, ingawaje idadi kubwa sana ya watu ilikuwa ikitoa kiapo cha utii kwa Husein, jibu lake lilikuwa kwam- ba angepigana tu na mtu yule ambaye amempiga, na atamshambulia yule tu ambaye atamshambulia yeye na hangetenda kutokana na kudhania tu.

Kuondoka kwa ghafla kwa Husein kutoka Makkah wakati zilikuwa zime- baki siku chacke tu kwa utekelezaji wa ibada ya Hijja ni ushuhuda wa dhahiri wa kuelekea kutokea karibuni sana ambayo aliihisi yeye mwenyewe endapo angebakia pale. Kuchukua hatua za wazi katika kujikinga ili kuzuia hatari ile kungeleta uwezekano wa umwagikaji damu mapema mno.

Husein hakutaka kujiingiza katika vita hapo Makkah kwani kufanya hivi kungenajisi utakatifu wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu na ingekuwa pia inapingana na tabia yake yeye ya amani. Yeye aliwachukua pamoja naye wale tu wanawake wa nyumba yake na watoto wake kama ishara bayana na nia zake za amani.

Wakati al-Hurr alipowasili kuja kuingilia maendeleo ya safari ya Husein kuelekea Kufa, Husein alimwambia yeye (al-Hurr) na jeshi lake, “Sikuwa nimefikiria kuja kwenu mpaka pale barua zenu na wajumbe wenu waliponijia, mkiniambia kwamba mlikuwa hamna Imam, na mkanikaribisha nije kwenu ili kwamba labda pengine mngeweza kuungana katika haki kupitia kwangu… Kama hamtaki huku kufika kwangu mimi hapa, basi nitarudi kule nilikotoka.”

Hakukuweza kuwepo tena mfano mwingine wa kuvutia wa uvumilivu zaidi ya huu. Wakati Husein alipoikariba Karbala, al-Hurr alipokea barua kutoka kwa Ibn Ziyad ambayo iliufanya msimamo wa al-Hurr kuwa mgumu kiasi kwamba alikataa kumruhusu Husein kusonga mbele zaidi, na akasema kwamba alikuwa anayo maagizo ya amri asimruhusu kupiga kambi katika sehemu yoyote ile inayokaliwa, bali akapige kambi katika bonde hame (yenye ukame) ambako maji yangekuwa ni ya taabu sana.

Marafiki na wafuasi wa Husein walipendekeza kwamba wapigane na al- Hurr kwa ajili ya kupata mahali pazuri zaidi pa kupigia kambi yao, kwani jeshi la al-Hurr wakati huo kwa kulinganisha lilikuwa siyo lenye nguvu sana. Husein hakukubaliana na ushauri huo, akikataa kuanzisha vurumai.

Hapo Karbala Husein alianzisha mazungumzo ya kuleta amani na Umar bin Sad, kwa ushahidiu wa wazi na wa kupenda amani na uvumilivu kiasi kwamba Umar bin Sa’d alivutika mno.

Husein pia alipendekeza kwamba yeye angekwenda sehemu za mbali zaidi nje ya Uarabuni ili amani iweze kudumu kama hakumlazimisha kumkubali Yazid kama khalifa halali, au kama mwakilishi wa kweli wa Uislamu. Hatimae Umar bin Sa’d aliandika barua kwa Ibn Ziyad akimpongeza kwa mgeuko mzuri wa mambo na akamwambia kwamba Husein alikuwa yuko tayari kufanya amani na kwamba masharti yake yangeweza kukubaliwa.

Hata katika siku ya 10 ya Muharram, wakati Shimr kwa matusi aliutaja moto uliowashwa katika shimo nyuma ya mahema ya Husein kuwazuia na mashambulizi kutoka upande wa nyuma, kwamba ni kama moto uliotazamiwa katika maisha ya akhera, na Muslim bin Awsaja alimwomba Husein ruhusa ili kumuua Shimr, Husein akakataa kukubali kwani aliona ni karaha kuanzisha vita.

Ingawaje mambo mengi yalitokea ambayo yangeweza kuifanya damu ya mtu ichemke wakati Husein alipotia mguu katika medani ya vita wakati wa asubuhi ya siku ya 10 ya Muharram, hakuonyesha hata dalili ndogo sana ya nia au maandalizi. Hakupanda farasi ambaye hutumika katika vita; bali alipanda ngamia ambaye ni alama ya amani.

Kisha alitoa hotuba ambayo ndani yake alirudia maneno yale ambayo aliwahi hapo mapema kumwambia al-Hurr na Umar bin Sa’d, “Kama hamuoni ni sawa kuja kwangu mimi hapa, (basi) niacheni nirudi kule nilikotoka.” Shuhuda hizi zenye nguvu za upendo na amani na uvumilivu zilimlazimisha al-Hurr kulitelekeza jeshi la Yazid.

Mhanga: Husein alijitoa mhanga maisha yake kwa mujibu wa mpango uliofikiriwa kwa vizuri sana, ili kwamba zamu yake ya kujitoa mhanga yeye mwenyewe maisha yake imfikie kwa pole pole sana na awe amepata taabu na dhiki zilizo kubwa kabisa na idadi kubwa mno ya misiba kwa kuondokewa na watu awapendao sana, wakati atakapojitoa mhanga yeye mwenyewe.

Siku ya mwezi 10 ya Muharram, kwanza kabisa Husein alipata mateso kutokana na mhanga wa wasaidizi (waunga mkono) wake na wenzake wa tangu utotoni mwake.

Kisha aliteseka kutokana na mhanga wa ndugu na jamaa zake wa damu waliokufa mmoja mmoja; mwanawe kama Ali al-Akbar ambaye alikuwa nuru ya macho yake, nguvu ya moyo wake, na tegemeo la umri wake wa uzeeni, mpwa kama al-Qasim, ndugu mwaminifu kama Abbas, na kisha mtoto mchanga kama Ali al-Asghar, ambaye shingo yake ilichomwa kwa mshale hatari. Baada ya moyo (watu) wake wote kutolewa mhanga, hatua ilifikia ya yeye binafsi kujitoa katika mhanga.

Kila sehemu ya mwili wake ilichanwa chanwa, kila tone la damu yake lilimwagika katika mhanga, na Husein hakubakia na chochote kile cha kujitoa mhanga, sehemu rahisi kabisa ya kazi yake, kujitoa mhanga maisha yake mwenyewe, ilibakia bado kufanywa. Na kufikia wakati wa mchana kujitoa mhanga kwake yeye kukawa pia kumekwishafanywa, na kichwa cha Husein kilikatwa kutoka katika mwili wake!

Kamwe mhanga mkubwa na uliokamilika kama huo hautakuja kutolewa tena.