read

Muhtasari Wa Utafiti

Hakika mauti si kutoweka bali ni kuingia kwenye uhai halisi wa Barzakh. Na sera ya waislamu zamani hadi sasa imeendelea kuwa ni kutawasali kupitia Manabii na Mawalii walio hai na wafu bila kutofautisha kati ya dhati yao na dua. Hivyo unadhihirika usahihi wa rai isemayo: Inaruhusiwa kutawasali. Na inathibiti ubatilifu wa kauli isemayo: Ni haramu na imekatazwa.

Pia njia za kuombea ambazo mja anajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia njia hizo hazitokani na juhudi za kielimu, bali zinatolewa na kuwekewa mipaka na Sheria, na inawezekana kuzipata kupitia Sheria. Na kila njia ya kuombea iliyo nje ya mpaka huu ni bidaa na upotofu.

Na mwisho wa maombi yetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe.