read

Neno La Jumuiya

Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na Kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha ni kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiisilamu.

Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanachuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za Ujumbe wa Ahlul-Bait.

Wanachuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote.

Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea tukufu za Ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu.

Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa Kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama.

Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanachuoni wa Kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni vya aina ya pekee, kwa sababu una nguzo ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na uzalendo uliyokatazwa.

Unazungumza na wasomi na wanaharakati wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanaituliza akili na yanapokewa na maumbile salama.

Jaribio hili la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Baiti limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizo- pita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya nchi zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Jumuia imejiepusha na udadisi uliokatazwa na ni yenye kuhangaikia kuzi- dadisi akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya Ahlul-Bait ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee.

Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati Maalumu toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi.

Tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tunachokiweza kati- ka juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulioanao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola Wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aidhihirishe juu kuliko dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.

JUMUIYA YA KIMATAIFA YA AHLUL-BAITI KITENGO CHA UTAMADUNI