read

Kuhusiana Nasi

(Inawahusu watoaji wa toleo la Kiingereza ambalo kitabu hiki ni tafsiri yake)

Leo hii, akili iliyo macho huyaona mabadiliko kwenye maisha ya kiakili ya mwanaadamu. Sayansi na teknolojia, vikiwa kwenye ustawi wake wa juu zaidi, vyaelekea kukifikia kipeo chake cha mwisho. Mahitaji ya kimwili pamoja na tamaa ya mamlaka na tawala vimemwongoza mwanaadamu kwenye ufisadi wa dhahiri wa maadili yake. Katika hali hii ya kukatisha tamaa, mtu alazimika kutulia na kuitathmini hatari iliyojificha na inayowatishia wanaadamu wote kwa ujumla. Mwanaadamu, tayari kaisha mkodolea macho tena Allah, Mwingi wa rehema, Rahimu, kwa kuwa, sasa kaishatambua ya kwamba ufumbuzi wa matatizo yake na wokovu wake umo kwenye kuzifuata Amri za Allah.

Mgeuko huu, wa kutoka kwenye fikara za kimwili na kuja kwenye fikara za kiroho unaafikiana kabisa na malengo na shabaha za hii Seminari ya kiislamu. Mafundisho ya dini yanakwenda sambamba na maendeleo ya huu wakati wetu, yakitoa kimbilio lihitajiwalo mno na akili yenye kusumbuka na mashaka. Haya ni matokeo ya mtanabahisho, ya kwamba sasa inatambulikana ya kwamba siri ya kuishi maisha ya kiuchamungu kwenye ulimwengu huu huongoza kwenye baraka ya milele ya maisha ya Ahera. Huu ndio ujumbe wa UISLAMU kwa ulimwengu mzima.

Hii Seminari ya kiislamu inadhamiria kuinua juu kurunzi ya mwongozo wa kiroho na kusaidia kwa juhudi zote katika kuukuza urithi wa mwanaadamu. Inaionyesha njia ya maisha ifundishwayo na Qur’ani katika utukufu wake wa asili. Inayaonyesha yale yenye nguvu na yaliyo ya kweli tu. Vitabu vyake vimekusudiwa kufaa katika kuyafikia mahitaji ya kiroho ya zama zetu hizi. Vitatumika kama kijito kitiririkacho maji daima, kwa wale walio na kiu ya elimu.

Hii Seminari ya kiislamu ni taasisi ya ulimwengu mzima yenye kujitahidi katika kudumisha udugu wa kiislamu. Inafurahia mchango wa akili zilizo bora zaidi, zaidi ya kuwa na msaada wa kimataifa kwa ajili ya kuyafikia malengo yake makuu. Inavyo vituo Canada, na Mashariki ya Mbali.

Orodha ya anwani iko kwenye kurasa za mwisho za kitabu hiki. Msomaji (wa Kiingereza) anaweza kukiandikia barua chochote miongoni mwa vituo hivi ili kuvipata vitabu vyetu.

Islamic Seminary Publications