read

Kwa Ndugu Msomaji

Asalaam Alaykum

Kitabu hiki kinatolewa na Seminari ya kiislamu (S.L.B. 5425, Karachi, Pakistan). Vitabu vyake vimelengwa kuyatimiza mahitaji ya kiroho ya zama zetu hizi, na msisitizo maalum juu ya kuzisafisha akili na fikara. Juhudi nyingi zimefanywa na Seminari hii kuweka kwenye vitabu vyake yale yaliyo na nguvu na yaliyo ukweli halisi kwenye Uislamu. Unaombwa kukisoma kitabu hiki katika hali iliyodhamiriwa. Vilevile unaombwa kuwasiliana nasi, kuhusu maoni yaliyo huru kuhusu vitabu vyetu, jambo tutakalolipenda mno.

Kuubalighisha ujumbe wa Uislamu ni jukumu lihitajilo ushirikiano wa watu wote. Seminari hii inakukaribisha ushiriki kwenye jukumu hili ukiuitika mwito wa aya ya Qur’ani Tukufu isemayo:

قُلْ إِنَّمَا أَعِظُكُمْ بِوَاحِدَةٍ ۖ أَنْ تَقُومُوا لِلَّهِ مَثْنَىٰ وَفُرَادَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُوا ۚ {46}

“…Sema: Mimi ninakuahidini jambo moja tu, ya kwamba msimame kwa ajili ya Allah, wawiliwawili na mmoja-mmoja…” (As-Saba 34: 46).

Allah na Akubariki.
Nduguyo katika Uislamu,
Katibu wa Uchapishaji.