read

Utangulizi

Kwa Jina La Allah, Mwingi Wa Rehema, Rahimu.

Tangu zamani za kale, mwanadamu amekuwa akiitafuta elimu kupitia milango yake ya fahamu. Hivyo basi, kwa kuvitambua vitu, hujaribu kulitatua tatizo lake. Katika mchakato huu, amekuwa akifanya majaribio, na hatimaye kwa kubahatisha alifikie kwenye ufumbuzi uwezekanao wa matatizo yake. Ikiwa imetegemea juu ya dhana na utendaji huu, sayansi ilistawi kwa ukubwa mno kwenye maeneo na nyanja mbali mbali za matumizi yake.

Kwenye zama hizi mpya za sayansi, mamia na maelfu ya maabara ya utafiti yanavutia nadharia ya wanasayansi ambao hufanya ugunduzi na ubuni- fu mkubwa mno wa kiwango cha kutoaminika cha usahihi wa ala na zana. Vivyo, kitu pekee ambacho hadi sasa sayansi imeshindwa kukikamata ni tatizo la kijamii. Ni dhahiri kwamba matatizo ya kijamii ni matatizo ya wanadamu. Na matatizo ya wanadamu ni ya hali ambayo haiwezi kuingizwa kwenye neli ya majaribio/testityubu (test-tube). Ili kuisadiki habari hii, mtu yuatambua vizuri mno kwa mfano, ya kwamba bado sayansi haijatoa jibu la kutoafikiana na chuki iliyomo miongoni mwa watu au tofauti za kimatabaka zinazokithiri kwenye matabaka ya jamii za wanaadamu.

Historia inatuambia kuhusu ustaarabu mkubwa uliopita hapo kale na mwishowe ukapotea. Hivi sasa tumebakiwa na masalio na magofu bubu yanayotukumbusha zama za kale za wanaadamu, zilizochakaa. Hakuna shaka kwamba sayansi inagundua habari za maisha kwa njia ya ufukuaji wa mashimo yanayodhaniwa kuwa na vitu vya kale kwa ajili ya uchunguzi, na kwa kujifunza masalio ya vitu visivyo na uhai (relics) na (vikisukuku) vile vyenye uhai vilivyogeuka kuwa mawe (fossilis), vilivyogandamana na miamba ya ardhi. Lakini tukiyaachilia mbali yote hayo, hakuna matokeo ya dhahiri yaliyopatikana kuhusiana na matatizo mengi ya wanaadamu.

Imam Ali (a.s.) alimpa dokezo la fikara zake mwanawe ambalo ni lenye kuhusika na jambo hili. Alisema: “Mwanangu mpenzi! Ingawa muda wa maisha yangu si mkubwa kama ule wa watu wengine waliofariki dunia kabla yangu, lakini nilijichukulia hadhari kubwa kujifunza maisha yao, kwa juhudu nyingi niliyapitia matendo yao, nilizifikiria fikara na matendo yao. Niliyachunguza masalio ya vitu vyao visivyo na uhai na magofu; na nikayafikiria maisha yao kwa makini mno kiasi kwamba nilijihisi kana kwamba niliishi na kufanya kazi pamoja nao tangu kwenye zama za awali za historia hadi kwenye hizi nyakati zetu, na ninayajua yaliyowatendea mema na yaliyowadhuru.”

Hakika, historia imeandika habari zote, zile zenye kupendeza na zenye kuchukiza, lakini lile lisikitishalo ni kwamba hakuna yeyote aliyejali kuzama ndani ya kina cha sababu za habari hizo. Ama kuhusu ufumbuzi halisi wa tatizo, liwe kubwa au dogo, hakuna juhudi katika upande wa mwanaadamu uonekanao kwenye historia. Ni yale mambo yasiyo muhimu ndiyo yaliyoshughulikiwa kwa maelezo marefu yaogofyayo.

Kwa kuwa historia ni masimulizi ya matukio ya kale yaliyoandikwa, yana- pata kuwepo kwake kutoka kwa mwandishi wake. Watu walioiandika historia hawakuwa huru kutokana na kiburi cha ubinafsi, rangi au sehemu atokayo mtu, na hivyo basi, lengo lake hasa laonekana kushindwa.

Mbele ya tafsiri mbaya na uzushi wa habari za kihistoria, msomaji wa kawaida wa historia yumo kwenye hasara ya kuuelewa ukweli wa jambo hilo. Ni kama daktari ambaye, kama hana taarifa sahihi kuhusu maradhi ya mgonjwa wake anayemwuguza, hataweza kuchunguza maradhi halisi ya mgonjwa wake huyo.

Hakika sifa moja ya historia iangazayo mno ni kwamba, inazichukua taarifa za maisha ya watu wakuu wa kale. Hakika watu hawa waliiunda historia kwa kuwa walileta mapinduzi na mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya wanaadamu.

Miongoni mwa hawa watu wakuu hakuna hata mmoja aliyeishi maisha yenye mambo mengi, ya kimapinduzi na yenye maana kama aliyoishi Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

Hakuna yeyote miongoni mwao aliyeziacha athari za kudumu kwenye jamii aliyojitokeza kama alivyofanya Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.). Huu ni ukweli uliokubaliwa na karibuni wanahistoria wote, wawe ni wa Mashariki au wa Magharibi.

Kujifunza maisha ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), mkuu zaidi miongoni mwa wanaadamu wote, kunachukuliwa kuwa ni kwenye kuleta hofu na kujierevusha. Nyororo ya matukio ya kabla na ya baada ya kuzaliwa kwa huyu mtu mkuu kunatoa mawazo kwa ajili ya kila mtu aliye na japo punje ndogo tu ya akili na hisia za ulinganifu.

Kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akiwa yu mtoto aliyezaliwa baada ya baba yake kufariki dunia, na kifo cha mama yake, Bibi Amina (a.s.), alipokuwa na umri wa miaka sita tu, na kulelewa kwake, kwanza na babu yake na kisha na ami yake ni mambo yasiyo kifani.

Baada ya kuyapitisha maisha yenye mambo mengi, kujitenga kwake kwenye Pango la Mlima Hira na Ufunuo wa Allah uliofuatia, kuwaitia watu kwenye dini ya Allah, upinzani wa makafiri na wenye kuabudu masanamu, maonevu na mateso yao, umadhubuti wake uliodumu katika kuimarisha ujumbe wa Allah kwenye kipindi cha miaka kumi na mitatu ya mwanzo ya Utume wake mjini Makkahh hadi kwenye muda wa kuhamia kwake Madinah, ni matukio yasiyo kifani kwenye historia.

Miaka kumi ya mwisho ya maisha yake mjini Madina, kuimarisha kwake juhudi za ujumbe wake kwa ajili ya uenezaji wa Uislamu, kushiriki kwake kwenye vita nyingi dhidi ya makafiri na hatimaye kutekwa kwa Makkahh bado ni matukio makuu yenye kuonekana kuwa si ya kuaminika, lakini yameandikwa kwenye historia kuwa ni mafanikio ya kimiujiza.

Mamia ya vitabu yameandika kuhusiana na maisha na ujumbe wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) lakini vitabu hivi haviwezi kuchukuliwa kuwa ni wasifu kamili juu ya sifa na mafanikio yake. Hasa yale maandishi ya mustashrik yameingiliwa na chuki, makosa na tafsiri potofu.

Kitabu hiki sio tu kwamba kinatoa mambo yenye kuongoza, bali vile vile kimezitegemeza taarifa zake kwenye maandiko ya kihistoria yaliyo ukweli. Moja ya sifa zake zijidhihirishazo mno ni kwamba mwandishi amechukua hadhari kubwa katika kuyasimulia matukio ya kihistoria, na wakati huohuo amejitahidi, akiwa yu mwanachuoni mtafiti, kuyaendea matukio hayo kwa fikara zenye kuchanganua mambo pia.

Sifa nyingine, ya kitabu hiki yenye kuvutia ni kuwa kiko huru kabisa kutokana na uzushi na hadithi zilizobuniwa zilizozushwa na faida zilizofichwa.
Kwa maneno mengine ni kwamba, kiko kabisa kwenye hali ya kusalia kwenye kiwango kihitajikacho cha ukweli wa kihistoria. Kwa kifupi ni kwamba, kinapelekwa kwa Waislamu kwa ujumla, bila ya upen- deleo na kiburi.

Tunategemea ya kwamba kitabu hiki kitalifikia lengo lake la kukiongoza kizazi kichanga chenye shauku kuu ya kujipatia taarifa za kweli na zenye kutegemewa juu ya huyu Mtume Mkuu wa Uislamu (s.a.w.w), na tunaamini ya kwamba vijana wetu wa kiislamu watajipatia mwongozo kutokana na kitabu hiki katika kuyatengeneza maisha yao kwa mujibu wa maamrisho ya Allah pamoja na sifa tukufu za Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na Dhuria wake Wateule (a.s.).