Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, The Message, kilichoandikwa na Sheikh Ja’far Subhani. Sisi tumekiita, Ujumbe. Kwa vile kitabu hiki ni kikubwa, tumekigawa katika juzuu nne ili kuwarahisishia wasomaji wetu kukisoma kwa makini katika kila sehemu. Hii uliyonayo mkononi ni Juzuu ya Nne.

Kitabu hiki kilichoandikwa na mwanachuoni mkubwa Sheikh Ja’far Subhani kimekuwa ni miongoni mwa vitabu bora vilivyofanya utafiti wa kina kuhusu historia ya Uislamu na Waislamu.