read

Safari Yangu Kuelekea Madhehebu Ya Ahlul- Bayt

Hadiya

Kwa aliyezaliwa kwenye ngome ya umaasumu na uchaMwenyezi Mungu, na mashukio ya wahyi na uongofu, na mrithishwa wa fadhila tukufu na ukarimu.

Imwendee mwanamke mwema, na mpambanaji mtoa nasaha, aliye huru mkataaji, na ni muujiza Muhammadiyah, na ni hazina Haydaria, na ni amana Fatmiyah.

Imwendee aliyekuwa mtii wa Mwenyezi Mungu, katika hali ya siri na ya wazi, na aliyetoa changamoto kwa msimamo wake dhidi ya wanafiki na wafitini.
Imwendee aliyewatia hofu masultani wakorofi kwa msimamo wake thabiti, na alizishangaza akili kwa umadhubuti wa moyo wake, na alifanana na baba yake Ali kwa ushujaa wake, na alishabihiana na mama yake Zahra’a kwa utukufu wake na balagha yake.

Imwendee aliye nasibika na ukoo wa kinabii na uimamu, aliyetunukiwa shani ya cheo, utukufu na karama. Imwendee shujaa wa Karbalaa bibi wa kibani Hashim. Sayyidatiy wa Maulatiy Zaynab (a.s.).