Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho al-Haqiqatu ‘dh-Dha’i’ah kilichoandikwa na Sheikh Mu’tasim Sayyid Ahmad. Sisi tumekiita, Ukweli Uliopotea. Kwa vile kitabu hiki ni kikubwa, sisi tumekigawa katika juzuu tano ili kiwe chepesi kusomwa na wasomaji wetu wa Kiswahili. Hiki ulichonacho mkononi mwako ni juzuu ya pili.

Kitabu hiki ni utafiti uliofanywa na mwanachuoni huyo wa Kiislamu kuhusu madhehebu za Kiislamu. Utafiti wake huu ulihusisha pia maho- jiano na mijadala baina yake na na masheikh wa Kiwahabi na maustadh wake katika chuo alikosoma.