Table of Contents

Dibaji

Kitabu hiki kinajadili umuhimu wa zile Swala tano za kila Siku na nafasi yake mbele ya Allah (s.w.t.). Kitabu hiki pia kinajadili mikakati unayoweza kutumia kujenga na kudumisha kiwango cha hali ya juu cha uangalifu na umakinifu wakati unapowasiliana na Allah (s.w.t.), Ambaye anawataka waja Wake kuwa watulivu katika swala zao, zaidi kuliko ibada nyingine yoyote.Yeye, Muumba na Msanifu wa Ulimwengu, anamwambia yule mtu, ambaye anaiswali Swala yake kwa uangalifu mdogo, utulivu wa akili na umakinifu mdogo:

“Ewe Muongo! Unataka kunidanganya Mimi? Naapa kwa Ufahari na Utukufu Wangu kwamba Nitakunyima furaha ya maombi yako na starehe ya mawasiliano yako binafsi na Mimi.”(Hadith al-Qudsi)

Jameel Kermali amefanya utafiti wa uangalifu wa hali ya juu na amegawana nasi matokeo ya kazi yake katika hali ya uwazi na yenye kutia hamu ya kusoma.

Muhsin Alidina

Maelezo Muhimu

Hili zoezi la Siku – 30 ni zoezi kamili la kujenga uangalifu na umakini katika Swala. Kwa wale wanaotaka usaidizi, mnaweza kuwasiliana na mtunzi mwenyewe moja kwa moja kwa kutumia anuani hii: jameelyk@aol.com Yeyote anayemaliza hili Zoezi la Siku 30 pamoja na fomu zote kujazwa, mtunzi atashukuru kama matokeo na faida zake yatatumwa kwake na yanaweza kuchanganuliwa. Faida za zoezi hili zitachapishwa, Insha Allah, katika jarida la kiislamu.

Wasifu Wa Mtunzi

Jameel Kermali ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza, mwenye shahada ya kwanza (Hons) katika Saikolojia, ametaalimikia zaidi katika Saikolojia ya Afya. Yeye pia ni Mtaalamu wa Magonjwa ya Saikolojia aliyethibitishwa na Bodi na ni Daktari Mthibitishwa na Board of Certified Biofeedback Practitioner, akitaalimu hasa katika EEG Biofeedback. Shahada yake ya Udaktari ni ya madawa ya matibabu ya asili (Naturopathic Medicine) na nyanja yake maalum ni pamoja na tiba inayotoa dalili za ugonjwa kwa mtu asiye na ugonjwa huo (Homeopathic), Lishe na Dawa za Mitishamba. Jameel pia ni Mshauri wa Lishe aliyethibitishwa na Bodi ya Washauri wa Lishe.

Alikuwa mhitimu wa juu kabisa katika darasa lake katika al-Hussain Madrassa iliyoko Dar es salaam na yeye ni mwalimu katika masomo ya Kiislamu.

Anayo shughuli yake binafsi huko Long Island, New York Jameel pia ni sehemu ya timu ambayo imeanzisha Bodi ya Hajj ya Michezo (Hajj Board Game), ya kwanza ya aina yake, tayari kutolewa hivi karibuni. Hajj Board Game, inayofanana na umiliki pekee, inatoa maelezo kwa ufupi ya Hijja kwenye Nyumba ya Allah swt, yakikusanya elimu, burudani na mwujiza. Mchezo huo unawafaa watu wazima na vijana, wale wanaokwenda Hijja, wale ambao walikwisha kwenda Hijja na wale ambao bado hawajajaaliwa kwenda safari hii tukufu. Unakuja kamilifu pamoja na dadu 2 zenye doa moja, madoa mawili na isiyo na doa, kipima wakati; vifaa vinne vya kuchezea, kadi 90 za A, 90 za B, 90 za C, 90 za D, 90 za fursa ya uchaguzi, na 90 za kuokota na kadi za tahadhari.

Jameel pia ni mtunzi wa kitabu kilichotafitiwa sana, The Truth of Islam – A Contemporary Approach Towards Understanding Islamic Beliefs and Practices, ambacho kiko kwenye matayarisho. Kitabu hiki ni kazi ya kisayansi inayohusiana na Dhana ya Nguvu katika Ulimwengu, Habari zake, na jinsi imani na vitendo vya Kiislamu zinavyokubaliana moja kwa moja na ugunduzi wa kisayansi na wa kisasa unaojulikana.