Table of Contents

Mkakati Wa 14: Kupima Usahihi Na Kukagua

Fuatilia kiwango chako cha uzingatiaji na umakinifu katika Swala. Kama ni kiwango sahihi, basi toa shukurani; kama ni chenye mapungufu, omba maghfira, usamehewe.

Kujirekebisha, kutafakari na kujichunguza ni masharti muhimu sana kwa mwenye kutafuta ukweli ambaye anapigana na nafsi yake. Kurekebisha nafsi au masharti maana yake ni kujifunga mwenyewe kwa uamuzi wa kutofanya kitu chochote dhidi ya amri ya Mwenyezi Mungu.

Imam al-Khumeini (r.a.) anakushauri kuwa hasa katika hali hii ya akili wakati wa usiku, wakati wa kujipima na kujichunguza mwenyewe na wa hadhari ya kina, na kutathmini matendo yako ya kutwa nzima. Huu ndio wakati wa kuona kama umekuwa mwaminifu kwa Mwingi wa Rehema kwa wote, ambaye Kwake kila mtu anawajibika. Kama umekuwa mtiifu Kwake, basi unapaswa umshukuru kwamba Yeye amekuwezesha kufanikiwa katika azma zako. Zaidi ya hayo, Shetani na kundi lake lililolaaniwa wanaweza kuukuza uzito wa shughuli machoni mwako, lakini hizi ni hila ambazo zinafanywa kwa udanganyifu. Unapaswa wakati wote kumlaani ibilisi na mawazo maovu ndani ya vina vya moyo wako na kwenye miliki ya akili yako.

Kuchunguza upya utendaji wako katika Swala za kila siku kuwe ni sehemu ya tafakari unayoifanya kila usiku, ili kuwa na uwezo wa kuchanganua matatizo yote na kupendekeza ufumbuzi unaowezekana. Kwa njia hii, Swala inayofuatia ina tofauti ya wazi kabisa na ile ya iliyopita. Kwa maelezo zaidi tafadhali rejea Kitabu cha mazoezi ya siku thelathini.