Table of Contents

Mkakati Wa 17: Kuwa Mwenye Majonzi, Unyenyekevu Na Huzuni

Bila shaka, huzuni inauletea moyo wako faida nyingi sana, mojawapo ikiwa ni mapinduzi ya nafsi. Ni ule wakati ambapo una huzuni na majonzi, ambapo unakuwa na uwezo wa kujikusanya na kujipa nguvu ili kuwa mtulivu zaidi katika Swala.

Inakubalika kabisa kwamba akili yenye huzuni imepatanishwa vizuri zaidi kuelekea kwenye lengo (kwa Allah swt, katika suala hili) na yenye uwezo zaidi katika kudumisha kiwango cha hali ya juu cha mazingatio na umakini.

Kusiwe na tatizo lolote katika kutumia aina hii ya hisia kabla ya Swala, kwa vile unapaswa kujionya mwenyewe juu ya haya yafuatayo, ‘Huna njia ya kuweza kujua kama dhambi zako zilizopita zimesamehewa; huna njia ya kuweza kujua kama utajizuia kutenda madhambi hapo baadaye; huna njia ya kujua kwamba vitendo vyako vinapata radhi ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)...’ (As-Sadiq AS)

Mtume (s.a.w.w.) anayaweka yote haya wazi kwa kumwambia Abu Dharr (r.a.): “Ewe Abu Dharr! Allah (s.w.t.) hakuabudiwa kwa kitu chochote kile kama kile cha urefu wa huzuni.

“Ewe Abu Dharr! Yeyote yule aliyepewa elimu ambayo haimsababishi yeye kulia kwa sababu tu amepewa elimu, haitamfaa elimu hiyo. Allah (s.w.t.) amewaelezea wenye elimu na akasema:

‘Kwa hakika wale waliopewa elimu kabla yake, wanapoisomewa wanaanguka juu ya nyuso zao katika kusujudu na wanasema, ‘Utukufu ni wake Mola wetu! Kwa hakika ahadi ya Allah (s.w.t.) itatimia.’ Wanaangukia nyuso zao wakilia na wanazidi kuwa wanyenyekevu.’”

Kufikia hapa, lazima ieleweke kwamba kulia na kutoa machozi kwa sababu za kibinafsi wakati wa Swala kutaifanya Swala yako kuwa batili na tupu.