Table of Contents

Mkakati Wa 9: Kuomba Maghfira Na Kukubali Mipaka

Baada ya kila Swala unapaswa kuomba maghfira, kwani hii, bila kutambua waziwazi, itaongeza uzingatiaji wako na umakini wakati wa swala na kukuleta karibu sana kwake Allah (s.w.t.). Pale unapoisoma du’a hii, lazima utubie kwa dhati kwa Allah (s.w.t.) kwamba ile swala ambayo umeimaliza hivi punde haikufikia kiwango kinachotakiwa na kuomba kusamehewa kwa ajili hiyo na Mola Mwenye Huruma. Kisha unamgeukia na kuahidi kwamba swala inayofuata itakuwa nzuri zaidi. Jinsi hii peke yake ni uhamasisho wa kufanya vizuri zaidi safari nyingine unaposimama mbele ya Mwenyezi Mungu. Kukubali kasoro kutajenga shauku ndani yako ya kufanya vizuri zaidi ya hapo.