read

Maswali Na Majibu

Sehemu hii ni ya maswali na majibu ya maswali yaliyoulizwa baada ya hotuba iliyotolewa katika Semina hiyo ya "Golden Crescent Group" iliyofanyika mjini Lushoto mnamo tarehe 22 Oktoba 1977.

Swali 1: Je, inaruhusiwa kwa Msichana aliyevaa ushungi kusoma katika Shule za Mchanganyiko (za Wavu….. na Wasichana)?

Jibu: Iwapo msichana huyo atazifunika sehemu zote za mwili ila uso na vitanga vya mikono (toka vifundo vyo kitanga hadi ncha za vidole), basi itaruhusiwa.

Swali 2: Kama jibu ni "Ndio", basi hataweza kujibu maswali atakayoulizwa na mwalimu, je, itambidi anong’one?

Jibu: Kuzungumza na “Ghair Mahram” (mtu asiyekuwa Mahram yako) huwa haramu kama itakuwepo hatari kuwa “Ghair Mahram” huyo atapata ashki kutokana na kuisikia sauti ya mwanamke huyo.

Swali 3: Je, mwanamke aneweza kushiriki kikamilifu katika maisha ya kijamii na kiuchumi akiwa kajitanda ushungi?

Jibu: Ndio, ilimradi asivuke mipaka iliyowekwa na Sheria ye Kiislamu. Kumbuka kuwa sehemu sahihi kwa mwanamke ni ndani ya mipaka ya nyumba yake tu.

Swali 4: Katika jamii nyingi mume na mke, wote wawili ni lazime wafanye kazi. Kwa mfano katika jamii ya wakulima, kama illvyo nchini Tanzania, mume na mke, wote wawili ni lazima wafanye kazi katika shamba ambalo, bila ya kulishughulikia familia yao itakufa njaa. Nini ushauri wako kuhusu hali hii?

Jibu: Kama mnataka kuufuata Uislamu nilazima muubadili utaratibu huu. Kwa hakika wazo la kuwa katika jamii ya kiukulima lazima mwanamke afanye kazi shambani limetokana na kutoangalia vizuri. Tunawaona wanawake wakifanya kazi nchini Tanzania na kisha tunajumlisha tu kuwa ni msingi wa kijamii. Tunasahau kuwa nchi zinazoulisha ulimwengu kama vile U.S. A., Canada, Australia n.k. ni nchi za Kilimo, lakini kilimo chao hakitegemei wanawake kufanya kazi mashambani. Hivyo, si kilimo kinachowataka kazi ya kuvunja migongo wanawake; bali hali ya kuwa watu wako nyuma sana ndiyo inayowalazimisha wanawake wa Kitanzania kufanya kazi mashambani, si jamii ya kilimo isababishayo hivyo. Na tunaweza kuseme kuwa Uislamu hauipendi hali hii ya kuwa nyuma katika maendeleo. Uislamu unawataka hawa wanawake warudi kwenye nafasi yao maalum, ambayo ni nyumbani. Kwa maneno mengine, jamii ya Kitanzania itawajibikiwa kutumia misingi ya Kiislamu iwapo inapenda kusonga mbele.

Swali 5: Wanachuoni we Kiislamu wameamrishwa kuipinga "Bidat". Ni katika hatua ipi wanapotakiwa kufanya hivyo? Katika hatua ya mwanzoni au ya mwishoni?

Jibu: Katika kila hatua.

Swali 6: Wanawake wa Kiislamu katika nchi tofauti tofauti hujifunika shungi za aina tofauti tofauti. Ni aina gani ya shungi iliyo sahihi kufuatana na misingi ya Kiislamu?

Jibu: Aina yo yote ile itakayowapendezea ilimradi to iwawezeshe kuzifuata sheria za Kiislamu barabara; yaani waifiche miili yao.

Swali 7: Je, si lazima kwa wanawake wetu kwenda kujipatia elimu ya utabibu na elimu ya kufanyiza madawa n.k.? Mwanamke mgonjwa atapendelea ugonjwa wake uchunguzwe na daktari wa kike kuliko wa kiume. Vile vile anaweza kujieleza vizuri bila ya kizuizi cho chote kile kwa mganga wa kike kuliko kwa mganga wa kiume. Viko vyuo vya utabibu vya wanawake viwili tu duniani, na kwa sababu ya uhaba wa madaktari wa kike, ni lazima kwa wanawake wetu kwenda kujiunga katika vyuo vingine na hivyo ni lazima wavue shungi zao.

Jibu: Ni lazima kwa mwanamke kujaribu kwenda kwenye vyuo vya wanawake tu, sio katika vyuo vya mchanganyiko.

Swali 8: Wanawake wengine wamefaulu kulinda heshima zao bila ya kuvaa shungi. Sasa kwa nini wanawake wajitaabishe kuvaa shungi na kumbe wanaweza kujipatia heshima zao hata bila ya kuvaa shungi?

Jibu: Ni lazima kwa wanawake wa Kiislamu wote. Heshima ya mwanamke wa Kiislamu mbele ya Mwenyezi Mungu hutegemea kuvaa kwake ushungi; kwa mfano, itazame Aya hii isemayo:
‘ninyi si kama wanawake wengine ….’ Ni cheo na heshima ya wanawake wa Kiislamu “kukaa majumbani mwenu”. Kama tukijaribu kuitenga heshima yao na “Hijaab”, basi sura yetu haitapatana na sura alivyokusudia Mwenyezi Mungu.

Swali 9: Nina amini kuwa katika Uislamu, mume na mke watahesabiwa kuwa ni sawa katika Siku ya Hukumu. Sasa ikiwa ni hivyo, kwa nini katika hali hii ya sasa, ya kukua kwa hali ya maisha, mwanamke asifanye kazi na kumsaidia mumewe katika kuendesha maisha ya nyumbani?

Jibu: Msifuje mali na jaribuni kubakia ndani ya mipaka ya Uislamu. Mwanamke anaweza kumsaidia mumewe katika kuongezea kipato cha nyumba kwa njia zile tu, ambazo hazimlazimishi kutoka nje ya nyumba yake. Usawa katika Siku ya Hukumu hauna maana ya kushiriki sawa katika kujipatia gharama za maisha katika ulimwengu huu.

Swali 10: Je, wazazi waache kumlazimisha binti yao kuvaa 'Hijaab', ili isimuwiye vigumu anapolazimishwa na watu wa upande wa mumewe kutoivaa?

Jibu: Unapokuwa naye timiza wajibu wako na madaraka yako. Yatakayotokea baada ya anapokuwa na mumewe si wajibu wako. Kama unachelea kuwa baada ya juma moja hutapata chakula cho chote, je, utaanza kufa njaa tangu leo?

Swali 11: Je, ni heshima kwa msichana kuvuliwa ushungi wake na watu wa upande wa mumewe?

Jibu: Hapana. Ni haramu. Ni lazima kwa msichana huyo kukataa.

Swali 12: Hijaab ni wajibu kwa msichana, lakini kama mumewe akimkataza kufanya mambo yaliyo wajibu, basi msichana huyu afanye nini? Je, ni wajibu kwa msichana huyu kumtii mumewe?

Jibu: Hapana. Ni lazima asimtii mume huyo iwapo atamwambia kufanya dhambi. Na mume anapata dhambi maradufu kwa kumlazimisha mkewe kuvua “Hijaab” au kufanya jambo lo lote lililo haramu.

Swali 13: Kufuatana na swali la 12 hapo juu, je, msichana huyo anaweza kuomba apewe talaka?

Jibu: Ndio, aneyo haki ya kuomba talaka iwapo mume huyo atamlazimisha kutovaa Hijaab. Lakini itukiapo hivyo, Mujtahid ataamua kufuatana na hali ilivyo. Kwa mfano itambidi atosheke kuwa huyu mwanamke halitumii hili swuala la Hijaab kwa hila au njia tu ya kujipatia taIaka.

Swali 14: Tukiwa tuishakubali kuwa nafasi ya mwanamke ni nyumbani mwake, je, ni haki kumruhusu mwanamke wa nchi za kimagharibi kufanya kazi ili amsaidie mumewe ambaye kipato chake peke yake hakiwatoshi?

Jibu: Nadhani ni lazima kwanza jambo moja lieleweke wazi wazi kabla ya kulijibu swali hili; mojawapo ya madhambi makuu saba ni kama mtu anaishi mahali ambapo yu huru kabisa kuabudu dini aipendeyo, na anahamia mahali ambapo hatakuwa huru kuweza kuyafuata maamrisho ya dini, kunaitwa Al-Tauba Baed Al-Hijra (maana yake hasa ni Kuhamahama baada ya Hijrat). Ndugu zetu wengi imewabidi kuhamia nchi za Magharibi kwa sababu wasizoweza kuzizuia. Hatu wezi kuwalaumu. Lakini wako wengine waliochagua tu kwenda kuishi katika nchi za Magharibi kwa sababu ya faida za kidunia. Wao wanayo majukumu makubwa, si kwa Akhera yao tu, bali vile vile kwa watoto wao na vizazi vyao vya baadaye.

Sasa tukilijia lile swali, ushauri wa kwanza wa watu wa namna hiyo ni kuwa wasiende katika nchi za namna hivyo ambako hawawezi kujipatia maisha yao bila ya kipato cha mke. Kama wanaishi katika nchi hizo na kwa sababu zisizozuililka basi mwanamke anaweza kufanya kazi nyumbani mwake ili kuongezea kipato cha mumewe. Lakini ni lazima azifuate barabara sheria zote za Kiislamu zinazohusu Hijaab.