Dibaji

Maudhui iliyoshughulikiwa katika kitabu hiki ni ya umuhimu mkubwa sana. Inataka kuonesha vipi upendo ulivyo katika moyo wa kiroho na maadili ya imani mbili kubwa, kati kati yake ambapo kujuana kukubwa na kufahamiana baina ya imani hizi mbili kunahitajika kwa haraka mno iwezekanavyo.

Uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu umepatwa na athari ya urithi wa historia wa mashaka na chuki inayojitokeza katika nyakati ambapo falme zenye nguvu na ustaarabu ulioshirikishwa nazo, wamejikuta wenyewe katika mizozo na mapambano. Ushindi wa Waislamu wa rasi ya Iberia, vita vya msalaba, kuanguka kwa Constantinople, nia ya ukubwa wa dola ya Ottoman na ubeberu wa magharibi wa karne ya 19 na ya 20, yote haya yameacha mabaki ya machungu na uadui.

Hii imeendelea leo kujidhihirisha yenyewe katika Mashariki ya Kati, katika Balkan na katika sehemu mbali mbali za ulimwengu. Katika jamii za magharibi taarifa za vyombo vya habari juu ya harakati za vurugu za Waislamu wanaowaita wa siasa kali au imani kali vimeelekea pasina haki kabisa, kuhusisha Uislamu na Waislamu na ushabiki wa dini ambao kwa kiasi kikubwa umeondolewa katika upendo. Ni kana kwamba ule uhusiano kati ya Wakatoliki na Waprotestanti katika Northern Ireland ni wa kuwakilisha uhalisi wa Ukiristo.

Pamoja na mambo haya ya kusikitisha, kuna vipengele zaidi mno vya historia ambavyo ni bayana vya uhusiano kati ya imani hizi mbili na ustaarabu wao. Ni rahisi mno kusahau miundo mingi ya elimu ya wote pamoja na utajiri wa utamaduni walioshirikiana katika sanaa, usanifu majengo, filosofia, hisabati, sayansi, na fasihi kwa karne nyingi.

Maeneo ya mapatano ya kiteolojia kati yao (na vile vile na uyahudi), yamekuwa vile vile yanafahamika kwa kiasi kidogo sana. Wana kukubaliana kwa sawa sawa kuhusu ufunuo wa vitabu vya dini na simulizi za kiutume za imani hizi mbili; uthibitisho wa pamoja wa imani katika Mungu wa Ibrahim; na msisitizo mkali juu ya umuhimu wa kumtukuza Mungu katika ibada na kuishi maisha katika njia iliyoelekezwa na sheria Zake.

Kufanana na mwingiliano wa fikra na kiroho wa baadhi ya walimu wakubwa na mairifani wakati wa kipindi cha karne za kati huonekana vile vile kusahauliwa kabisa.

Hata hivyo, katika kubadilisha maadili ya kijamii ya mfumo wa misimamo mingi zaidi ya kidini, hali ya uungaji mkono ya ukoloni katika nchi za magharibi, na hisia kubwa ya jumuiya ya ulimengu mzima (utandawazi) iliyoletwa na mawasiliano bora, kwa haraka misimamo inageuka. Mazungumzo kati ya imani za dini na utashi wa kutafuta ujuzi wa kweli, kuachwa huru kutoka chapa za zamani na za kisasa, kumejitokeza zaidi mno katika nchi za magharibi, shukurani kwa kazi za wanachuoni kama vile John Esposito na Ninian Smart.

Ingawa kukua kwa jumuiya za Kiislamu katika jamii za watu wa Ulaya hakukuwa bila matatizo na migogoro, utashi mkubwa unajitokeza miongni mwa kizazi cha vijana ili kuweka hali ya baadaye ya pamoja iliyosimama juu ya kuheshimiana na kujifunza imani na utamaduni kutoka kwa kila mmojawao.

Ni kwa ajili ya moyo huu kwamba kitabu hiki kimeandikwa. Kwa mtazamo wa matatizo mazito ambayo yamejitokeza kati ya Iran, U.S.A na U.K. kwa miongo miwili iliyopita, haya yote ni ya muhimu zaidi kwamba kitabu hiki ni cha mwanachuo kijana, Shia wa Iran, Mahnaz Heydarpoor. Mhitimu wa Chuo Kikuu mashuhuri cha Qum, ambaye alikuja Uingereza na mumewe na familia yake katika mwaka wa 1997, mara tu alionesha kuvutiwa katika kuchukua mafunzo zaidi na utafiti. Imekuwa ni furaha kubwa kwangu kuwa msimamizi wake na kukutana na wote, Mahnaz na mumewe Mohammad Shomali, ambaye yeye mwenyewe ni mwanachuoni mwenye kuheshimika. Wote wamekuwa mabalozi wazuri kwa Iran na kwa Uislamu na nimejfunza mengi kutoka kwao kuhusu tabia na moyo wa Uislamu kisha kutokana na kusoma vitabu vingi.
Shauku ya Mahnaz ya kuamua kuongeza ujuzi wake wa Ukiristo na juhudi na nguvu ambazo kwazo amefuatilia lengo lake hili, sio tu kwa kusoma vitabu, bali pia kwa kukutana na Wakristo wa usuli za madhehebu mbali mbali na vikundi kama vile Chama cha Focolare, imekuwa ya kuvutia mno.

Uchanganuzi wake juu ya upendo katika Ukiristo ni wa kisomi na wa utambuzi mno, lakini itakuwa ni ufafanuzi wake wa ukuu wa upendo katika teolojia ya Kiislamu na maadili ambao hususan utakuwa wa kuvutia kwa wasomaji wa Magharibi, Wakristo na wengineo.

Inatumainiwa kwamba ari ya Mahnaz itaweza kulipwa na wasomi wengi, kama yeye wanaotafuta maeneo ya mazungumzo ili kuzidisha tathmini ya wote na ujuzi kati ya Uislamu na Ukiristo. Vile vile inatumainiwa kwamba ukunjufu na ukarimu wa kiroho (kwa neno, upendo wake) vile vile utalipwa, ili kwamba uponaji wa vidonda vya huzuni vilivyosababishwa na chuki ya karne nyingi na kutokuelewana kunaweza kuharakishwa kwa faida ya mamilioni.

Dr. Dennis Bates, Manchester
Metropolitan University.