Sehemu Ya Kwanza

1. Maadili Ya Kidini Uadilifu Unamaanisha Nini?

Kabla ya majadiliano yeyote kuhusu ‘maadili ya dini’; mtu lazima afafanue anachomaanisha mtu kwa kusema ‘maadili au ‘-a kimaadili’ kwa upande mmoja na ‘dini’ au ‘-a kidini’ kwa upande mwingine. Katika kitabu hiki sitofautishi kati ya ‘kimaadili’ na ‘uadilifu’ ingawa natambua kwamba kwa asili maneno haya mawili yanatokana na asili tofauti:1

Maadili huonesha watu jinsi ya kuondoa sifa mbaya kwao wenyewe na jinsi ya kukuza sifa nzuri. Mifumo tofauti ya maadili yaweza kutofautiana katika msisitizo wao. Kwa mfano, katika maadili ya kimagharibi msisitizo mkubwa (au msisitizo pekee) kwa kawaida umewekwa juu ya tabia ya mwanadamu na desturi. Na hivyo Paul Foulqilie anafafanua maadili kama mfumo wa desturi, mila ambayo huwaongoza wanadamu kwenye malengo yao.2

Kwa upande mwingine tunaona kwamba baadhi ya mifumo ya maadili huchukua tabia za wanadamu kwa uzito zaidi. Kwa mfano Sadr al-Din al- shirazi, mwanafalsafa Mwislamu mashuhuri, huelezea tabia za wanadamu na desturi zilizochimbukia kutoka kwenye tabia hizi kama masuala ya maudhui mbili tofauti.3

Ili kuelezea ni aina gani ya uchunguzi wa maadili uliohusishwa hapa wakati wa kujadili maadili ya kidini lazima nioneshe kwamba kuna aina tatu za uchunguzi wa kimaadili: maadili ya kielelezo, maadili kusanifisha na maadili uchanganuzi.

Maadili ya kielelezo ni jabarati ya uchunguzi wa mifumo ya unyofu au desturi za mtu fulani au kundi au jamii au dini au vitu kama hivyo. Kwa mfano, maadili ya kielelezo yaweza kufanya jukumu la kutupatia sisi maelezo ya uadilifu wa Socrates au Ugiriki ya kale au maadili ya Kiislamu au hata ya ki-Marx. Mbinu hapa ni kivielelezo tu ili kutoa taarifa sahihi juu ya ni nini haswa mfumo wa maadili, au mfano au desturi, na sio nini kitakachokuwa pale. Hivyo, hakuna hukumu ya kitathimini inayohitajika hapa.

Maadili kusanifisha hushughulikia nadharia za maadili juu ya usahihi wema na uovu. Hujibu maswali kama haya: Ni kitu gani kinafanya kiten- do kuwa sahihi kimaadili au makosa kimaadili? Je, kitendo ni kizuri au sahihi kama kimeleta furaha au raha, au je kitendo ni kizuri kama ni kizuri kwa chenyewe bila kujali matokeo yake? Vile vile maadili kusanifisha hujadili hadhi ya maadili ya suala makhususi kwa mfano; kutoa mimba ni kitendo kizuri au kibaya?

Maadili ya uchanganuzi hayashughuliki na jarabati au ukweli wa kihisto- ria. Wala hayashughuliki na uamuzi wa kutathimini au kusanifu. Bali huchunguza maswali kuhusu maadili kama: Nini maana au matumizi ya maneno kama vile sahihi au kosa?’ Je, maadili na uamuzi wa kutathimini waweza kuthibitishwa? Kama ndio, vipi? Nini asili ya uadilifu? Ni nini kinachomaanishwa na wakala huria au wakala mhusika?

Kihistoria, filosofia ya maadili ya uchanganuzi imejumuisha maadili ya kielelezo na ya kusanifisha. Hata hivyo, wanafalsafa wengi wa hivi karibuni, wanatetea zaidi filosofia ya uchaganuzi, wameifanya ya pekee kwa maadili ya uchaganuzi.
Wanaamini kwamba uchunguzi wa kifilosofia unawezekana tu katika kushughulikia masuala ya maadili ya uchaganuzi. Hapa, inafaa kuangaliwa kwamba wanafalsafa wa maadili kwa kawaida huchukuwa sentensi ya maadili kuwa sentensi ambayo ina moja ya dhana saba zilizotajwa hapa chini kama kiarifu chake. Dhana hizo saba ni: wema dhidi ya ubaya, sahihi dhidi ya makosa, kupasika dhidi ya kutopaswa, na jukumu. Kwa mfano, ‘kusema ukweli ni vizuri’ ni sentensi ya maadili kwa sababu kiarifu chake ni moja ya dhana za maadili. Hata hivyo, ‘Wema ndio unaeleta furaha kubwa kwa idadi kubwa mno ya watu’ sio sentensi ya maadili, ingawa inahusiana na maadili. Kwa maneno mengine ni uchanganuzi wa maadili zaidi kuliko uadilifu.4

2. Ni Nini Kinachomaanishwa Na Dini?

Nikiwa nimefafanua kinachomaanishwa na ‘maadili’, sasa nitafafanua ninachomaanisha kwa ‘dini’ au ‘-a kidini’; kuna maoni tofauti kuhusiana na ufafanuzi wa dini; kwa hiyo eneo pana la madhehebu zinafikiriwa kuwa ni za ‘kidini’; kwa mfano, David Edward anafafanua dini kama ‘mtazamo wa heshima ya kumwogopa Mungu, au miungu au mapepo au fumbo la uhai likifuatiwa na imani na kuathiri mielekeo ya msingi ya mtu binafsi na tabia ya kikundi.5

Mimi binafsi sitaweza kukubaliana na ufafanuzi wa kijumla kama huu, hata hivyo, nafikiri katika utekelezaji hakuna haja ya kujisumbua sisi wenyewe kuhusu maswala ya uhusikaji wa jumla. Hapa nashughulika na dini katika muktadha mahususi.

Kwa hiyo, katika kitabu hiki kwa kusema ‘dini’ namaanisha tu dini zenye kumpwekesha Mungu, ukiwemo Ukristo na Uislam, na kwa ‘maadili ya kidini’ namaanisha kanuni za maadili, mifumo ya sheria au mifumo ya dini hizi. Uchunguzi wangu wa mifumo hii ya uadilifu utakuwa zaidi wa kivielelezo, kwa vile nitaelezea misimamo ya Uislamu au Ukiristo, au msimamo wa Waislamu binafsi au Wakiristo juu ya masuala kama vile upendo.

3. Sifa Bainifu Za Maadili Ya Kidini

Ilidokezwa (Markham, 1998) kwamba kuna baadhi ya nukta zinazofanana kwenye uadilifu wote wa kidini. Hapa nitaelezea nne katika hizo kama tabia za maadili ya kidini: Imani katika mapepo, utegemezi juu ya vyanzo vya kidini; imani katika kutopendelea; na athari ya ukweli wa maadili, na shughuli za kuchangiwa.

Katika dini zenye kumpwekesha Mungu, kuna asili yenye nguvu ya hali ya juu ambayo ina mamlaka juu ya wanadamu kuwaeleza mwenendo bora wa maisha na kuwaonesha jinsi ya kufikia mwenedo huo. Wafuasi wa dini yeyote ambao wana sababu fulani za kuamini katika ukweli wa dini hiyo hawatakuwa na swali kuhusu mamlaka ya chanzo hicho.

Maadili ya kidini yanaweza kufafanuliwa kama aina ya maadili ambayo hupata uhalali wake kutoka mamlaka ya kidini. Kwa hiyo mafundisho ‘yaliyofunuliwa ya mamlaka hiyo yana wajibu mkubwa katika kuamua ni kipi ni sahihi au makosa. Mafundisho ya mamlaka hiyo yanaonekana katika vitabu vya dini hiyo kama Bibilia ya Wakiristo na Qur’ani ya Waislamu.

Kama ilivyo, vyanzo vya kidini kwa ajili ya maadili haviishii kwenye vitabu (maandiko). Imependekezwa (Markhamu, 1998) kwamba kunaweza kuwa na vyanzo vingine vinne ambavyo simulizi (Hadith) tofauti za kidini hutumia wakati wa kufanya maamuzi ya kimaadili.

Chanzo cha pili cha mwongozo wa kimaadili ni taasisi na desturi za kila dini. Mara nyingi hizi hufikiriwa kama nyongeza kwenye chanzo cha kwanza, yaani maandiko katika Ukiristo kwa mfano, wale walioko katka mila ya Ukatoliki wa Roma (Roman Catholics) wanazungumza kuhusu

Kanisa kama chombo kilichotolewa na Mungu kutafsiri maandiko kwa kila zama mpya. Kama tutakavyoona baadaye, katika Uislamu, Sunnah ni muhimu mno katika kutengeneza sheria za Kiislamu.

Chanzo cha tatu cha mwongozo wa kimaadili ni akili ya mwanadamu. Jukumu la akili katika mwongozo wa kimaadili unatakikana kujadiliwa kwa kujitegemea. Hata hivyo, kwa ufupi naweza kusema kwamba Uyahudi na Uislamu una mtazamo wa kimatumaini wa ubinadamu. Katika hali zote zawadi ya akili kwa mwanadamu ambayo, hututofautisha sisi na wanyama, ni chanzo tulichopewa na Mungu ambacho lazima kitusaidie katika kufikia kwenye uamuzi sahihi wa maadili.

Katika Ukiristo suala hili lina utata zaidi kwa kuwepo mafundisho ya dhambi ya asili. Hata hivyo desturi kubwa za Ukiristo huchangia busara kwamba ingawa dhambi imelemaza uwezo wa mwanadamu kutumia akili zao sawasawa, bado ni yenye uwezo. Hakika ni wazo hili ambalo hupelekea kwenye mafundisho ya Romani Katoliki kanuni asilia. Nadharia ya kanuni asilia hushikilia kwamba watu wote kila mahali, bila msaada wa maelezo ya ufunuo, wana uwezo kwa kiasi fulani wa kuelewa ukweli wa maadili. Kwa ajili hii watu wote wanakuwa hawana kisingizio. Kuhusiana na kanuni ya maadili asilia mtazamo ulioruhusiwa wa kanisa Romani katoliki ni kama ifuatayo:

“Mtu hushiriki katika hekima na wema wa Muumba ambaye humpa yeye ustadi juu ya vitendo vyake na uwezo wa kujitawala mwenyewe pamoja na maoni kwenye lile la kweli na la wema. Kanuni asilia huelezea chimbuko la hisia ya maadili ambayo humuwezesha mtu kumaizi kwa akili mema na maovu, ukweli na uwongo.6

Chanzo cha nne cha elimu ya maadili inadaiwa kuwa ni utaratibu wa kiasili. Ian Markham (1998) anadokeza kwamba Romani katoliki ni mila bora ijulikanayo ambayo hutumia utaratibu asilia wa ulimwengu. Anatoa rejea kutoka kwenye kitabu cha st. Thomas Aquinas (aliyemfuata Aristotle) ambaye aliamini kwamba “Mungu amejenga kwenye maumbo ya viumbe wake kanuni asilia” ambapo ‘ile telos* ya kila shughuli ni madhumuni sahihi kwa ajili ya shughuli hiyo.’

Markham anatoa mfano mashuhuri wa uume, ambao kwa mujibu wa mafundisho ya Romani Katoliki una telos* ya uzazi. Kwa hiyo ni kiyume na maumbilena hivyo utovu wa maadili - kuutumia uume kwa shughuli nyingine kama vile punyeto na ulawiti, au kuuzuia uume kutotekeleza madhumuni ya asili kwa matumizi ya dawa au vifaa vya kuzuia uzazi7

Chanzo cha tano na cha mwisho cha athari za maadili ni uzoefu wa kidini. Desturi nyingine huamini kwamba unaweza kugundua kile Mungu ana- chotaka kwa ajili yako kupitia uzoefu wa kidini na swala, ambazo wakati mwingine yaweza kuwa dhidi ya maadili yanayokubalika ya zama fulani.

Desturi zote kubwa za kidini huamini kwamba maamuzi ya kimaadili ni mambo ya ukweli na ugunduzi. Ingawa kunaweza kukawa na kutokuelewana kati ya baadhi za dini kuhusu maudhui ya uadilifu, kana kuelewana juu ya tabia ya uadilifu. Wanachukulia uadilifu kuwa yameota mizizi katika umbo la ulimwengu na nje ya mipaka ya maamuzi ya mwanadamu. Wanaamini kwamba athari za maadili huvuka uwezo wa jumuiya za wanadamu, zimechibiwa chini, kwa namna fulani ndani ya maumbo ya ulimwengu, na zenye kuwabana watu wote kila mahali.

Licha ya uchagamano wa kila dini moja, nukta zinazofanana kati ya dini zote ni kwamba zote zinachukulia fikra fulani kuwa zenye umuhimu sana kwa wanadamu wote. Sasa tutafanya rejea kwenye fikra nne kama hizo: kujifunga kwenye upendo, umuhimu wa familia, umuhimu wa ibada, na ulinzi wa maisha ya mwanadamu. Kuna ushirikiano wa uwajibikaji kwenye upendo na huruma. Ingawa sifa hizi zinajulikana katika njia tofauti ndani ya desturi tofauti, ni sifa zinazotambulika kiulimwengu. Katika sehemu mbili zifuatazo za kitabu hiki nitachunguza mitazamo ya Ukristo na Uislamu juu ya upendo.

Fikira ya pili ambayo inapatikana kwenye desturi kubwa za kidini ni umuhimu wa familia na wajibu mkamilifu wa wanaume na wanawake. Katika (mafundisho ya) dini ya Uyahudi, Ukiristo na Uislamu, Hawa (mwakilishi wa wanawake) aliumbwa kumsaidia Adamu (mwakilishi wa wanaume). Dini zote hizi imani ziwe zinaruhusu au la, huchukulia talaka kama kitu kisichofaa.

Katika dini zote hizi, ibada ina jukumu kubwa katika kumtengeneza mtu mwema. Ibada ni utaratibu ambao kwao maisha hugeuka kuwa ya kidini. Ibada huhuska kwenye vipengele vyote vya maisha pamoja na mwanzo na mwisho wa maisha.

Kalenda (ratiba) za kidini huhusisha ibada fulani kwa siku, majuma, miezi, na miaka. Saumu (kufunga) katika siku fulani tukufu ni kawaida kwa desturi nyingi za kidini. Ibada husaidia katika kuupa shime uadilifu na kuleta nidhamu ambazo humkinga mtu na maovu.

Desturi nyingi za kidini husisitiza ukuu na umuhimu wa mtu na maisha ya mwanadamu. Maisha ya mtu yanachukuliwa kuwa ni yenye thamani sana na lazima yaheshimiwe. Hii sio kusema kwamba bila kuwepo shuruti zozote zile maisha ya mtu yaweze kuchukuliwa; desturi nyingi za kidini huruhusu vita na adhabu kubwa katika mazingira fulani. Lakini maisha ya mwanadamu yanapewa hadhi maalumu katika mitazamo ya kimaadili.

Baada ya kujadili kile ambacho kwa kawaida huchukuliwa kama tabia za uadilifu wote wa kidini, sasa nitafafanua zaidi juu ya maadili ya Ukristo na Uislamu, vyanzo vyao na baadhi ya maswali ya kimbinu kuhusiana na uvumbuzi wao.

4. Maadili Ya Ukiristo

Msingi wa maadili ya Ukristo uko kwenye Taurati ya Wayahudi, lakini sifa bainifu ya maadili ya Ukristo inaweza kugunduliwa kwa kuchunguza mafundisho ya Yesu katika Injili nne.8

Kama mambo yalivyo, lazima itajwe kwamba hakuna maelezo ya kinaganaga ya mafundisho ya maadili ya Yesu katika Injili. Preston anasema: “Injili ya nne huakisi katika njia yake yenyewe sifa bainifu za Yesu za mafundisho ya maadili. Hakuna hukumu juu ya suala lolote makhususi. Umakinifu uko juu ya changamoto kali ambayo Yesu analeta ili kukubali njia [yaani, mafundisho ya maadili yanayotokana na Taurati].”9

Khutba aliyoitoa juu ya mlima (Mt.5-7) ni mkusanyo (wa maandiko) unaokubalika zaidi wa mafundisho ya Yesu. Ingawa kulikuwa na taarifa nyingi za kihistoria na uchunguzi mkali wa Injili hizo, hapana shaka yoyote chanzo muhimu zaidi kwa Ukiristo leo ni Bibilia.

Kuwa na uwezo wa kuchunguza maadili ya Ukristo, mbali na uchunguzi wa msinngi wake katika ujumbe wa Yesu, lazima tuchunguze sehemu zinazotafsirika za Injili. Mkalimani wa Yesu ambaye kwamba tuna ushahidi zaidi kwake ni Mt. Paul. Anaonekana kuwa Mkiristo wa kwanza ambaye alitakiwa kueleza kuelewa kwake maadili ya Ukiristo kuhusiana na matatizo yaliyotangulizwa na makanisa.

5. Maadili Ya Uislamu

Kuna vyanzo viwili vikubwa vya maadili ya Kiislamu; Qu’ani na Sunnah. Qur’ani huchukuliwa na Waislamu kama Kitabu cha Mbiguni, kimejeng- wa kutokana na kutoka tu kwenye ufunuo wa Mungu. Waislamu huamini kwamba maana na maneno ya Qur’ani vyote hutoka kwa Mungu. Kimatendo, hakuna mgogoro mkubwa miongoni mwa Waislamu kuhusu tafsiri ya Aya hizo za Qur’ani ambazo zinahusika na uadilifu au kuhusu mfumo wa maadili wa ki-Qur’ani.

Sunnah yaweza kuchukuliwa kama utekelezaji wa mafundisho ya ki-Qur’ani kwenye matatizo ya maisha kama ilivyooneshwa kwa mifano katika matendo ya Mtume, misemo na uthibitisho (wa matendo au misemo ya wengine mbele yake). Kwa kawaida Sunnah ina maelezo zadi.

Miongoni mwa Shi’a, Sunnah hujumuisha Sunnah za Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake, Ahul-Bayt, ambao wanachukuliwa kama warithi wa ilmu wake na wafuasi wa kazi yake kwa kuwasilisha na kuelezea mafundisho halisi ya Uislamu kama yalivyo katika njia ambayo yalifunuliwa kwake. Utajiri wa maandiko mbali mbali kutoka kwa Maimamu wa Shi’a juu ya masuala ya maadili ni ya msaada mkubwa kwao katika kufafanua misimamo ya Kiislamu juu ya masuala yaliyoelezewa ya maadili.

Kwa Shi’a na Waislamu wengine, chanzo kingine muhimu ni hoja au akili, al-aql. Ingawa chanzo kikubwa kwa kusisitizia juu ya jukumu la akili ni Qur’ani yenyewe, kumekuweko na mgogoro miongoni mwa wanachuoni wa kidini wa madhehebu za Sunni kuhusu jukumu la akili na jinsi ya kufanya uwiano kati ya akili na ufunuo. Mgogoro kati ya Ash’ariyah na Mutazilah juu ya suala hili ni mashuhuri. Shi’a wana msimamo wa wazi kuhusiana na akili.

Kuna msemo mashuhuri miongoni mwa wanachuoni wa Shi’a, ambao mara nyingi huwa unatekelezwa kama hukumu nao ni: Kullama hakama bihi al-‘aql hakama bihi al-Shar’wa kullama hakama bihi al-Shar hakam bihi al-aql. Ina maana kwamba hukumu yoyote itakayofanywa kwa kutumia akili hukumu hiyo hiyo inafanywa na sheria ya kidini au Shari’ah na kinyume chake. Kwa hiyo, uthibitisho wa akili kuhusiana na masuala ya ibada unaweza kuchukuliwa kama uthibitisho wa kuruhusiwa kwake katika Shariah. Kwa mfano, kama haki kimantiki ni nzuri au sahihi halikadhalika itakuwa hivyo hivyo halali.

 • 1. Maneno yaliyotumika hapo ni "Ethical! & Moral": Ethical Iinatokana na neno la kigiriki lenye maana ya tabia ya mtu binafsi. Moral ni neno la kilatini lenye maana ya desturi ya kijamii. Taz.Walliams 1997 uk 546. Sisi tumetafsiri neno "ethics" kama "maadili" na neno "moral" kama "Maadili" vile vile, na neno "morality" kama " uadilifu" Neno " religion" kama dini na neno "religious" kama "-a kidini!" Maneno Moral na Morality kwa Kiswahili yanaweza kuwa na maana ya "nyofu" na "unyofu" lakini kwenye tarjuma ya kitabu hiki maneno haya tumeyatumia kama "maadili na uadilifu". (Mtarjima)
 • 2. Kama ilivyoelezwa katika Modarresi, 1997 uk. 18
 • 3. Tazama al-Shirazi, 1378 A.H. Juz. 4 uk. 116
 • 4. Taz. Frankena, 1973, uk. 10 na 98.
 • 5. Edwards, 1999, uk. 745
 • 6. Katekesimo ya Kanisa Katoliki, 1999, no. 1954
 • 7. Taz. Markham, 1998, uk. 801-802
  * Telos ni dhana ya kifilosofia yenye maana ya madhumuni au lengo.
 • 8. Kama ilivyo, kuna tofauti kati ya Injili hizo nne. Kama Preston anavyosema, Injili ya Yohana "inaweza kuchukuliwa kama teule na maandiko yaliyokomaa ya tafakuri juu ya maudhui kubwa za Injili tatu za kwanza, iwapo mwandishi anazijua au simulizi tu za mdomo nyuma yake." Preston,1996, uk. 94.
 • 9. Preston 1996, uk. 97.