Utangulizi

Kila moyo ambao hauwaki sio moyo;
Moyo ulioganda si chochote bali ni ukafi wa udongo wa mfinyazi.
Ewe Mungu! Nipe kifu ambacho kinawaka.
Na katika kifua hicho moyo, na moyo ule unaotafunwa na moto.
(Vashi Kermani, 1583)

Ingawa inaweza kuonekana wazi kwa watu wengi kwamba hakuwezi kuwa na maadili bila kuwa na itikadi au imani katika Mungu, siku zote kumekuwa na mgogoro juu ya suala hili au kwa ujumla zaidi juu ya uhu- siano kati ya maadili na dini.

Miongoni mwa wanateolojia wote wa Kikristo na wa Kiislamu kumekuwepo na baadhi ya wanachuoni ambao wanaamini katika tegemezi kamilifu la maadili juu ya amri za mungu na ufunuo, kama ambavyo kuna wengine ambao wanaamini katika uhuru wa maadili. Kwa mujibu wa kwanza ‘haki ya kimaadili’ maana yake ‘imeamriwa na Mungu’ na ‘makosa ya kimaadili’ maana yake ‘yamekatazwa na Mungu.’

Msimamo wa upande mwingine hushikilia kwamba kuna kigezo tegemezi cha mema na mabaya ambacho huweza kueleweka katika akili zetu. Kwa hiyo kuna uwezekano wa kuwa na maadili tegemezi ya dini.

Hata hivyo, watu hawa kwa kawaida huchukulia kwamba dini inaweza kutoa maelezo ya wazi na mapana zaidi ya maadili. Makundi yote hukubaliana kwamba dini hutoa maadili pamoja na vizuizi. Kwa hiyo, mdahalo miongni mwa wanachuoni wa dini sio kwamba imma dini huchangia kwenye maadili au iwapo kuna kitu kama ‘maadili ya kidini’, bali ni juu ya upeo wa mchango huu.

Katika kitabu hiki nitajaribu kuelezea dhana ya maadili ya kidini na baadhi ya sifa zake na kisha nitalenga juu ya dhana ya upendo kwa kiini cha dhana katika maadili ya kidini. Kuna ushirikiano wa msimamo kwenye upendo miongoni mwa dini zote kubwa za ulimwenguni.

Hata hivyo, wakati mwingine inaeleweka katika njia tofauti ndani ya tamaduni tofauti. Katika sura ya pili na ya tatu nitajaribu kuchunguza umuhimu na misingi ya kiitikadi ya upendo katika dini mbili kubwa za ulimwenguni: Ukristo na Uislamu. Katika kila suala nitachunguza vipengele tofauti vya upendo wa Mungu (kwa Yeye Mwenyewe, kwa viumbe wote na kwa wanadamu) na upendo wa binadamu (kwa Mungu na kwa wanadamu wenzake).

Hapa lazima niseme kwamba kile ambacho kwa hakika nataka kukifanya ni kuchunguza Ukristo na Uislamu wa nyuma, yaani, katika maendeleo yao ya kihistoria, kwa sababu tunachohusika nacho hapa kwa hakika ni kuona, kwa mfano, mchango halisi wa dini hizi kwenye maadili. Kitu ambacho tutafanya ni kuhakikisha kwamba tuna ujuzi wa kuaminika wa kila dini kama ilivyo leo hii.

Ili kuelewa maadili ya Ukristo na Uislamu, utafiti wangu utahusisha baadhi ya tafsir za maandiko matukufu. Nimetegemea zaidi juu ya Bibilia na Qur’ani Tukufu sambamba na hadithi (simulizi za Mtume Muhammad) kama vyanzo vya mwanzo vya maadili ya Kikristo na Kiislamu, hususan wakati ninapojadili wajibu wa upendo katika dini zote. Nilichofanya katika kazi hii kimekuwa ni kugundua kijumla picha inayokubalika ya upendo katika dini mbili hizi. Vinginevyo labda itajwe, nimejaribu kurejea kwenye nukta za kawaida na kile kinachokubalika kwa wote Wakristo na Waislamu.

Hakika katika kanuni, kunaonekana kuwa na tofauti nyingi kati ya wanachuoni tofauti wa kila dini juu ya suala lililoko kwenye mjadala. Natambua kwamba tayari kumekuwa na tafiti nyingi juu ya vipengele tofauti, hususani kuhusu upendo katika Ukristo.

Hata hivyo, nafikri kwamba bado kuna haja ya kufanya utafiti kama huu uliokusudiwa hapa. Faida moja ya utafiti huu ni kwamba unachunguza suala hili kiulinganishi na sio tu katika dini moja. Faida ya pili, utafiti huu hujumisha mjadala kuhusu wajibu wa upendo katika maadili ya Kislamu, ambao huenda ukawa haujulikani kwa wasomaji wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza. Faida ya tatu ni kwamba utafiti huu unatumia njia ya kuenda kwenye vyanzo vya asili vya Kiislamu katika lugha ya Kiarabu na Kifursi. Hivyo natumaini kwamba utafiti huu unaweza kutoa mchango wenye manufaa kwenye nyanja hii.

Hapa ningetaka kutamka kwamba suala la upendo limekuwa lenye kunishughulisha sana katika maisha yote ya ukubwani. Nilikuwa na umri wa miaka 16 tu wakati nilipopatwa na shauku kubwa mno kwa upendo wangu kwa ajili ya kumjua Mungu na kuwa karibu naye kiasi kwamba nilihisi nisingeweza kuendelea tena na maisha yangu ya kawaida. Pamoja na mipango yote ambayo wazazi wangu wamenipangia huko nyuma kwa ajili yangu, niliamua kabisa kuanza maisha mapya.

Pamoja na baraka za wazazi wangu niliondoka mjini kwangu na kwenda kwenye mji wa Qum, ambamo moja ya seminari kubwa ya Kiislamu imekuwepo humo kwa muda kwa zaidi ya miaka elfu moja. Nilijitolea maisha yangu katika kupanua ilmu yangu ya Uislamu, na la muhimu zaidi kujisogeza zaidi kwa Mungu. Ingawa sifurahii mafanikio niliyopata nina imani kabisa kwamba nilifanya uamuzi ulio bora kwa ajili yangu, na nimechagua njia yenye mwanga zaidi, njia ya upendo.

Wakati wa utafiti kwa ajili ya kazi hii, sikusoma tu kuhusu nukta yangu, yaani upendo, bali vile vile nilijaribu kuishi kwa nukta yangu hii na kuishuhudia katika maisha ya wengine. Wakati huo (Julai 1999) nilikaa juma zima pamoja na baadhi ya marafiki wakristo huko Mariapolis mjini Windermere. Huko niliona mambo mengi ya kufanana kati ya Uislamu na Ukristo na jinsi upendo wa kweli kwa Mungu na wanadamu wenzako unavyoweza kuleta moyo mpya kwenye maisha, na maisha mapya kwenye jamii ya kisasa. Nilikumbushwa uzoefu wangu mweyewe wakati nilipoingia seminari ya Qum. Sasa nimewaona wengine ambao huamini kwayo na kufuata njia ile ilenjia ya upendo.

Kuanzia hapo nilifanya kila niwezalo kuendeleza ujuzi wangu wa ukristo, kama ulivyoanza, na kama unavyotekelezwa leo. Sio tu kwamba nime- fanya marafiki wengi binafsi, bali vilevile nilitembelea taasisi mbali mbali za kikristo na sehemu za ibada na elimu. Kwa mfano, mwezi oktoba 1999, nilialikwa kwenye mkutano juu ya Uislamu na Ukristo ulioandaliwa na Focolare Movement mjini Rome. Mbali na kuhudhuria mkutano, nilipata nafasi ya kuwa mzoefu zaidi na Vatican na Roman Catholic Church (kanisa Katoliki). Vilevile nilikaa siku chache mjini Loppiano, mji mdogo karibu na Florence.Wakazi wote wa mji huu hujaribu kutekeleza Focolare kiroho na hususan kumpenda Mungu na jirani yao. Kwa ujumla nilikaa siku kumi nchini Italia ambako vile vile nilipata nafasi ya kukutana na Chiara Lubich, mwasisi wa tasisi na baadhi ya masahaba wake wa mwanzo ambao walizungumzia kuhusu sala na upendo.

Mwezi Februari 2000, nilikaa siku mbili kwenye chuo cha Mt. Yohana (St.Johns college) katika chuo kikuu cha Durham, kituo muhimu ndani ya kanisa la England kwa mafunzo ya uchungaji.
Nilikutana na kuongea na Rt. Revd. Stephen Sykes, mkuu wa St. John’s College na vile vile Mwenyekiti wa Kamisheni ya Mafundisho ya Kanisa la Uingereza (Doctrine Commission of the church of England), na pamoja na Dr. Croft, Dr. Wakefield na kundi la wanafunzi.

Mwezi Mei 2000, nilikaa juma zima huko Ampleforth Abbey ambako nilifanya vikao pamoja na Abbot na baadhi ya watawa wengine. Wakati wa vikao hivi, nilikujaelewa zaidi kuhusu Ukristo kiroho na asili ya maisha ya utawa. Lazima nitoe utajo maalum wa Cyprian Smith, mwandishi wa kitabu; The way of Paradox: Spiritual Life as Taught by Meister Eckhart na The Path of Life, ambaye kwa upole aliongea nami kuhusu mafunzo ya Ki-mungu ya Kikristo na ya kiroho, ya Benedictine order.

Vile vile nilinufaika kutokana na vitabu vya thamani vya maktaba ya watawa. Mwezi Juni 2000 nilikaa juma lingine huku Mariapolis, pamoja na mamia ya marafiki wakristo wa Katoliki na wa Angalikana kutoka Uingereza na sehemu nyingine za ulimwengu huko Stirling Seotland.

Nimejadili upendo katika Ukristo na marafiki wengi Wakristo, kama vile Dom Jonathan Cotton OSB, Leyland, Canon Simor Hoare, Skipton, Dimitrij Bregant, Rome na Dom Wulstan Peterburs OSB, Ampleforth. Watatu wa mwisho walisoma mswada wa sura ya upendo katika Ukristo na wakafanya mapendekezo yenye maana. Hivyo, natumaini nimeweza kupata ujuzi wa haki wa upendo katika Ukristo kama ulivyo katika nadharia na kama ulivyo katika utekelezaji leo.

Mwishowe, ningependa kusema kwamba kazi hii ya sasa ilikuwa asili yake ilitungwa kama tasnifu ya shahada ya M.A. (Religious Ethics: The contribution of Religion to Morality in Christian and Islamic Theology with Particular Reference to the Concept of Love) na kuwasilishwa kwenye Depatment of humanities and Applied Social Studies of the Machester Metropolitan University (Idara ya ubinadamu na uchunguzi wa kijamii ya chuo kikuu cha Manchester Metropolitan) katika mwezi wa Septemba 2000. Katika toleo hili kwa faida ya wasomaji wa kawaida sura mbili juu ya mitazamo ya kimapokeo ya teolojia juu ya uhusiano kati ya dini na maadili zimeondolewa.

Wakati wa kipindi cha utafiti wangu, nimekuwa nikisaidiwa na watu wengi. Shukurani zangu zimwendee, Dr. Denis Bate, ambaye hakuwa mwema tu na msimamizi mkarimu na kiongozi wa kozi, bali vile vile ni rafiki. Kuanzia hatua za mwanzo za masomo yangu hadi mwisho, siku zote alikuwa anapatikana, alikuwa tayari kujadili na kusoma kila chembe ya kazi yangu na kila siku akinipa moyo.

Shukurani zangu vile vile Rt. Revd. Stephen Sykes na Dr. Croft kwa ukarimu wao na msaada wakati wa kukaa kwangu kwenye chuo cha st John’s College, Durham. Napenda kuelezea shukurai zangu kwa Abbot na watawa wa Ampleforth Abbey, hususan Cyprian Smith na Wulstan Peteburs kwa ukarimu wao na mijadala yenye kusaidia.

Ningependa vile vile kuwashukuru wale wote ambao wamesoma na kutoa mapendekezo kwenye kazi yote au sehemu tu ya tasnifu yangu, kama vile mume wangu Dr. Mohamed Shomali, Canon Simon Hoare na Christina Hoare wa Skipton, Dimitry Bregant, Rome, Wulstan Peterburs OSB, Ampleforth.

Vile vile ni mwenye kuwiwa kwenye tasisi ya elimu na utafiti ya Imam Khomein - Qum, Iran, kwa kufadhili masomo ya mume wangu na gharama za kuishi kwetu, ambapo bila hivyo nisingeweza kukaa hapa (Uingereza) na kujifunza. Vile vile namshukuru mno mume wangu na watoto wetu wawili kwa upendo na msaada wao. Vilevile nawashukuru marafiki zangu wa Focolare, hususan

Frank Johnson kwa uaminifu wake na juhudi zake katika kuandaa kitabu hiki kwa ajili ya uchapishaji. Na mwisho lakini si haba, ningependa kutoa hisia za shukuran za dhati kwa Mungu mahala pa kila neema yake juu yetu na juu ya waja wake (neema) zilizopita na ambazo bado zipo.

London, Machi 2001