read

Ali Ibn Abi Talib, Khalifa Wa Nne Wa Waislamu

Ali alitokana na ukoo wa Bani Hashim, ukoo mashuhuri sana katika Arabia yote; na katika Bani Hashim, alitokana na familia maarufu sana – familia ya Abdul Muttalib. Huyu Abdul Muttalib alikuwa na watoto wa kiume kumi. Wawili wao walikuwa ni Abdallah, baba yake Muhammad Mustafa, na Abu Talib, baba yake Ali. Abdallah na Abu Talib walikuwa ni watoto wa mama mmoja ambapo hao ndugu zao wengine walizaliwa na wake wengine wawili wa baba yao.

Mama yake Ali, Fatima, pia alitokana na ukoo wa Hashim. Alikuwa binti ya Asad, mtoto wa Hashim. Asad na Abdul Muttalib walikuwa ni ndugu. Alikuwa kwa hiyo, ndiye dada binamu wa kwanza wa Abdallah na Abu Talib.

Mama yake Ali, Fatima binti Asad, alikuwa ni mwanamke wa pili katika Arabia yote kuukubali Uislam, wa kwanza akiwa ni Khadija.
Fatima binti Asad alikuwa ndiye mama wa kunyonya wa Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah swt. Alimlea kama mwanawe mwenyewe, na kwa kweli alimpenda kuliko hata wato- to wake mwenyewe, na yeye Mtume, alikuwa akimwita yeye, mama yake.

Baba yake Ali, Abu Talib, alikuwa ndiye Mtetezi wa Uislam, na alikuwa ndiye Mlinzi na Mlezi wa Muhammad. Aliuunga mkono Uislam na Muhammad kama kawaida, na alikuwa hana hofu mbele ya upinzani na vitisho kutoka kwa wapagani.

Akiwa Makka na Madina, kote Muhammad Mustafa alitangaza kwamba Ali alikuwa ni ndugu yake katika dunia hii na katika ile ya Akhera.

Ali alikuwa ndiye mshindi wa vita vya Badr. Na pia aliwauwa nusu ya idadi ya watu wa Makka wote waliokuwa wameuawa katika vita hivyo.

Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah swt. alimuoza binti yake wa pekee, Fatima Zahra kwa Ali. Mwenyezi Mungu aliibariki ndoa hii na watoto. Watoto wale walikuwa ni waja wachamungu kwelikweli. Furaha yao kuu maishani mwao ilikuwa ni kuwa na subira juu ya Mola wao.

Katika vita vya Uhud, Waislam wengi walikimbia kutoka kwenye uwanja wa mapambano. Mmoja ambaye hakukimbia alikuwa ni Ali. Aliyaokoa maisha ya bwana wake, Muhammad, siku hiyo.

Katika kuzingirwa kwa Madina, Ali alimuua Amr ibn Abd Wudd, na hapo akaiokoa Madina kutokana na kuvamiwa, na watu wake kutokana na kuuawa kwa halaiki.

Ali aliiteka Khaybar. Kwa ushindi wa Khaybar, ukawa ni dola lenye eneo. Hadi ushindi wa Khaybar, Uislam ulikuwa ni dola ya mji, iliyoishia kwenye kuta za Madina. Ali alikuwa ndiye mwandishi aliyeandika ule Mkataba wa Hudaybiyya.

Wakati Makka iliposalimu amri kwa Mtume (s.a.w.w.), Ali alipanda mabegani mwa Mtume na akavunja yale masanamu yaliyokuwa ndani ya Al-Kaaba. Yeye na bwana wake, Muhammad, wakaitakasa Nyumba ya Allah kwa nyakati zote kwa kuondoa alama za uabudu masanamu na ushirikina kutoka ndani yake. Kwa namna hii, Ali alishirikiana na Muhammad, Mtume wa Allah swt. kuanzia mwanzo hadi mwisho, katika kuunda mfumo wa Ufalme wa Mbinguni juu ya Ardhi.

Katika vita vya Hunain, Waislam walikimbia kwa mara nyingine tena. Ali akajiweka katikati ya Mtume na wapiganaji wa kipagani waliotaka kumuua. Alipigana dhidi yao mpaka Waislam walipokusanyika. Mnamo Oktoba mwaka 630 (9 A.H.) Mtume aliongoza msafara wa kwenda Tabuk, na akamchagua Ali kuwa mwakilishi wake hapo Madina.

Miongoni mwa masahaba wote wa Mtume (s.a.w.w.), Ali alikuwa ndiye mjuzi zaidi. Alikuwa na ujuzi kamili wa Qur’an na tafsiri yake. Alikuwa mbora wa mahakimu wote, na alikuwa ndiye msemaji mwenye ufasaha wa lugha zaidi wa Waarabu.

Kabla tu ya kifo chake, Mtume alitayarisha na kuandaa jeshi la kwenda Syria, na akamteua Usama bin Zayd bin Haritha, kuwa kiongozi wake. Ukimuacha Ali peke yake, aliwaamu- ru Muhajirina wote kutumika chini ya Usama. Ali alikuwa abakie na Mtume hapo Madina.

Katika kuutetea Uislam, ilikuwa ni familia ya Ali ambayo ndiyo iliyojitoa mhanga zaidi. Ubaidullah ibn al-Harith ambaye aliuawa kwenye vita vya Badr, na alikuwa shahidi wa kwanza wa Kiislam katika medani ya vita, alikuwa ni binamu yake wa kwanza. Mas’ab ibn Umayr na Hamza waliuawa katika vita vya Uhud, na wote wawili walikuwa ni ami zake. Jafar Tayyar ambaye aliuawa kwenye vita vya Muutah alikuwa ni kaka yake mkubwa.

Wakati Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) alipofariki, Ali aliandaa mazishi yake, na akamzika. Alikuwa anajua ni nini masahaba wengine walichokuwa wakikifanya wakati yeye akishughulika na kazi hizi lakini hakuruhusu kitu chochote kumvuruga mawazo. Alitanguliza wajibu wake mbele, kabla ya maslahi yake, na kanuni zake mbele ya siasa.

Edward Gibbon:

“Kuzaliwa, muungano, tabia ya Ali, vilivyomnyanyua yeye juu ya watu wake wote, kunaweza kuthibitisha haki yake kwenye nafasi ya uongozi iliyowazi ya Arabia. Mwana wa Abu Talib alikuwa, katika haki yake mwenyewe, ndiye mkuu wa familia ya Hashim, na mrithi wa ufalme au mlezi wa mji na hekalu la Makka. Nuru ya utume ilikuwa imekwishazimika; lakini mumewe Fatima angeweza kutegemea urithi na baraka za baba yake; Waarabu walikuwa aghalabu wakivumilia utawala wa kike; na wale wajukuu wawili wa Mtume walikuwa mara kwa mara wakibembelezwa kwenye mapaja yake, na kuonyeshwa kwenye mimbari yake, kama matumaini ya zama zake, na Mabwana wa Vijana wa Peponi.

Waumini wa kweli wa mwanzoni wangetamani kutembea mbele yao katika dunia hii na hiyo ijayo; na kama wengine wangekuwa hali ya tabia ya hatari na ngumu sana, ghera na uadilifu wa Ali havikuzidiwa kamwe na mbadili dini yeyote wa hivi karibuni. Aliunganisha sifa za mshairi, mpiganaji, na walii: hekima zake bado ziko hai katika mkusanyiko wa Hadith za kimaadili na kidini; na kila adui, katika mapambano ya ulimi au ya upanga, alitulizwa na ufasaha na ujasiri wake.

Tangu dakika za mwanzo za ujumbe wake mpaka kwenye ibada za mwisho za mazishi yake, Mtume hakuachwa kamwe na rafiki mkubwa, ambaye alifurahia sana kumwita ndugu yake, mshika makamu wake, na Harun Mwaminifu wa Musa wa pili. Mwana wa Abu Talib alikuja kulaumiwa baadae kwa kupuuza kulinda maslahi yake kwa tamko lenye uzito tu la haki yake, ambalo lingenyamazisha mashindano yote, na akaidhinisha urithi wake kwa maagizo ya Mbinguni. Lakini shujaa huyu asiyekuwa na wasiwasi alijiamini mwenyewe: wivu wa himaya, na pengine hofu ya upinzani, vingeweza kuahirisha uamuzi wa Muhammad; na kitanda cha kuugulia kilikuwa kimezingirwa na mwerevu Aisha, binti ya Abu Bakr.

Madai ya urithi na ari kubwa ya Ali vilikuwa ni chukizo kwa tabaka la juu la watu wazima, wenye shauku ya kutawazwa na kutwaa tena fimbo ya enzi kwa uchaguzi huru na wa mara kwa mara; Makuraish hawakuweza kamwe kukubaliana na fahari ya kupindukia ya kizazi cha Hashim.”
(The Decline and Fall of the Roman Empire)

Maelezo mafupi hayo ya wasifa, yaliyopita ni sahihi kwa jumla lakini kauli nyingine zinahitaji mabadiliko kidogo. Gibbon amekosea katika kueleza kwamba Ali hakulinda maslahi yake kwa tamko lenye uzito la Mtume. Mtume alikuwa ametoa matamko kama hayo, sio mara moja bali ni mara nyingi sana kama ilivyoelezwa kabla.

Mwanahistoria huyu amezungumzia pia juu ya “hofu ya upinzani” ya Mtume. Mtume (s.a.w.w.) hakuwa na hofu juu ya mtu yeyote. Alikuwa amewashinda maadui wenye kuogopesha zaidi kuliko wale ambao upinzani wao ungeweza “kumtishia” yeye katika saa yake ushindi.

Gibbon anaendelea kuzungumzia juu ya “uchaguzi huru na wa mara kwa mara.” Hilo tabaka la juu la watu wazima lilikuwa na shauku ya kutawazwa na kutwaa tena fimbo ya enzi lakini kwa ajili yao tu, na sio kwa uchaguzi huru na wa mara kwa mara. Upandaji wa Abu Bakr kwenye madaraka ulikuwa ni “ufaraguzi,” na Umar alikuwa ndiye “mwenye sauti ya uchaguzi” katika suala lake.

Pale Abu Bakr alipokuwa anafariki, alimteua Umar kama mrithi wake kwa amri. Kwa kufanya hivyo, alitupilia mbali upuuzi wa uchaguzi. Umar, kabla ya kifo chake, aliunda jopo la wateuzi sita, na aliizuilia nafasi ya khalifa iwe ndani yake. Hakuna mtu yeyote nje ya jopo hili anayeweza kuchagukiwa kama khalifa.

Uchaguzi pekee ambao ulikuwa huru kweli ni ule wa Ali ibn Abi Talib. Alichaguliwa katika uchaguzi huru wa kwanza na wa mwisho daima katika historia yote ya Uislam.

Mwishowe, Gibbon anasema kwamba Makuraish hawakuweza kukubaliana na fahari ya kupindukia ya kizazi cha Hashim. Ni sawa. Lakini Makuraish hao hao ambao hawakuweza kupatanishwa na fahari ya kupindukia ya kizazi cha Hashim, walikuwa na shauku ya kukubaliana na fahari ya kupindukia ya kizazi cha waabudu masanamu wa zamani na wala-riba wa Makka. Katika hamu yao ya kutaka kupatanishwa nao hawa, Makuraish ambao walikuwa wamechukua fimbo ya enzi hapo kabla, sasa wakaiweka juu yao.

Kurejeshwa Ufalme Wa Mbinguni Juu Ya Ardhi

(Ukhalifa Wa Ali Ibn Abi Talib)

Baada ya kuuawa kwa Uthman, woga na hofu viliwaingia masahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Wajumbe wa kamati ya uteuzi ya Umar walikimbilia kwenye usalama wa kutojulikana kwao. Mauti ya Uthman yametia hofu katika nyoyo zao. Nchi nzima ilikuwa imejawa na fadhaa, na hakuna hata mtu mmoja, haidhuru angekuwa jasiri na mwenye shauku kiasi gani, ambaye alikuwa tayari kutia shingo yake kwenye kitanzi kwa kulikubali jukumu la kuiendesha serikali. Ilikuwa ni dhima iliyojaa hatari kubwa na mbaya sana.

Lakini ilikuwa ni lazima jambo lifanyike. Chombo cha Uislamu hakingeweza kuachwa kuelea ovyo kwa muda mrefu, na mkono imara ilibidi upatikane wa kukiendesha bila ya kuyumba.

Miaka kumi na mbili ya utawala mbovu imewaamsha Waislam katika usingizi wao mrefu na kuridhika kwao. Sasa wametambua kwamba uongozi wa umma ulipaswa kuwa katika mikono ya mtu ambaye angeweka maslahi ya umma mbele ya maslahi ya familia yake mwenyewe. Kwa hiyo, mara tu baada ya Uthman alipokufa, macho yote yalimgeukia Ali. Masahaba wa Mtume hawakuweza kufikiria juu ya mtu mwingine yeyote ambaye alikuwa na uwezo na ujasiri wa kukomesha rushwa katika serikali na vurugu katika nchi, na kudu- misha amani, na sheria na utaratibu kwenye Dar-ul-Islam - Nchi ya Kiislam ambayo ilikuwa imeharibiwa na migogoro ya kiuchumi na kijamii, na ilikuwa imekubwa na mfuatano wa haraka haraka wa viwewe.

Muhajirina na Ansari mashuhuri wote, kwa hiyo, walikusanyika kwenye Msikiti wa Mtume (s.a.w.w.), na wakakubaliana, katika mkutano wa siri, kumwomba Ali kuchukua madaraka ya serikali na kuliongoza jahazi la taifa kwenye usalama. Ujumbe kwa hiyo ulimwendea kwa Ali, na kumwomba akubali jukumu hili.

Tabari anasema katika Tarikh yake kwamba Muhajirina na Ansari karibu wamsonge Ali. Walimwambia kwamba umma ulikuwa hauna msimamizi, na serikali ilikuwa haina kiongozi, na kwamba yeye, Ali, pekee alikuwa ndio mtu mwenye sifa stahilifu kabisa za kuijaza nafasi hiyo, sio tu kwa sababu ya ukaribu wake na Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah swt., bali pia kwa sababu ya sifa zake binafsi na utumishi wake kwa Uislam.

Ilikuwa ni mara ya kwanza tangu kufa kwa Mtume wa Allah swt ambapo ilionekana kwa mtu yoyote hapo Madina kwamba kulikuwa na kitu kama “sifa” za kuwa khalifa. Huko nyuma suala la sifa lilifutikwa kila mara kiongozi mpya alipokuwa apatikane. Umar alimfanya Abu Bakr kuwa khalifa kwa sababu yeye alikuwa ndio mtu mzima zaidi katika masahaba wote. Abu Bakr alililipia fadhila tendo la urafiki la Umar kwa kumchagua yeye kama mrithi wake. Uthman alichaguliwa kuwa khalifa kwa sababu alikuwa tajiri na mdhaifu.

Ali, hata hivyo, hakulikubali pendekezo la masahaba hao, na akasema kwamba alipende- lea kuwa mshauri zaidi kuliko kuwa khalifa.

Lakini masahaba hao pia hawakukubali kukataa kwa Ali, na wakasema: “Hakuna mtu aliyetoa utumishi wa kutambulika kwa Uislam, wala hakuna mtu aliyeko karibu zaidi na Muhammad kuliko wewe. Tunakuona wewe kama mtu mwenye kustahiki zaidi kati ya watu wote kuwa Khalifa wetu.”
(Tarikh Kamil, Juz.111, uk.99, Ibn Athir)

Ali bado hakukubali, na masahaba bado wakachagiza, na wakasema: “Tunakusihi kwa jina la Allah swt ukubali huu ukhalifa. Kwani wewe huioni hali ya umma? Je, huzioni hatari mpya zikizuka kila mahali katika nchi za Kiislam? Nani atazisimamisha kama sio wewe?” (Tarikh Kamil, Juz.111, uk.99, Ibn Athir)

Lakini Ali ni wazi alikuwa ametulia kwenye wazo la kukubali ukhalifa. Haukuwa ni utulivu wa kawaida bali ulikuwa ni matokeo ya fikra za muda mrefu na za busara.

Huko nyuma, wakati mmoja, “tamaa” ilimgharimu Ali kiti cha utawala wa Arabia. Umar alizungumzia kwamba angemchagua Ali kama mtawala wa Waislam kama yeye Ali asingekuwa na “tama” sana. Umar alizungumza kana kwamba tamaa ni kitu cha kushutumiwa.
Kauli yake vilevile ilimaanisha kwamba yeye mwenyewe na baadhi ya wengine wamekuwa makhalifa bila ya tamaa yoyote ile. Huenda ukhalifa ulikuwa ni kitu ambacho kimelazimishwa juu yao zaidi ya kupenda kwao; na hawakuwa na nafasi ila kukubali mzigo wa dhima hiyo!

Kwa vile Umar na Abu Bakr hawakuwa na tamaa, wote hao, na Abu Ubaidah ibn al-Jarrah, wote watatu, lazima wawe ama wamesukumwa na kuburuzwa kwenda kwenye banda la Saqifah!

Kupokea kwa Ali kwa maombi ya masahaba kukubali huo ukhalifa, kungeashiria kwamba alikuwa, hatimaye, ameagana na tama. Huko nyuma, alikuwa kamwe hajapoteza fursa ya kuvuta nadhari ya umma kwenye ubora wa haki zake binafsi, na kwenye haki ya suala lake.

Aliamini kwamba ilikuwa ni haki yake ya asli kuwa mrithi wa kwanza wa Mtume wa Allah. Haki hii haikuwa ni kitu ambacho watu wengine wangeweza “kumpa” yeye, ingawa waliweza kuiondoa kutoka kwake, na waliiondoa.

Jambo muhimu katika sera ya serikali ya Saqifa, kama ilivyoonyeshwa kabla, ilikuwa ni kumpinga Ali na Bani Hashim kwenye ukhalifa. Katika hili washika cheo wake wawili wa kwanza walifanikiwa. Mshika cheo wa tatu, hata hivyo, aliuawa katikati ya mvurugiko wa sheria na utaratibu, na hakupata muda wa kuteua mrithi wake mwenyewe. Lakini kama angeishi, angeweza, bila shaka yoyote, kumchagua mkwe wake, Marwan, au binamu yake, Mu’awiyah, kuwa mrithi wake.

Ali alikiukwa katika mara tatu mfululizo huko nyuma. Lakini sasa, baada ya kifo cha Uthman, Waislam walihisi kwamba walikuwa, kwa mara ya kwanza, huru hasa kuteua au kuchagua khalifa kwa ajili yao wenyewe, na chaguo lao kwa hafasi hiyo lilikuwa ni Ali. Kugongana kwa matukio hatimaye, kumeleta ule ukhalifa uilokuwa ukitafutwa kwa muda mrefu, karibu yake. Lakini kwa mshangao wa kila mmoja, Ali hakuonyesha shauku yoy- ote ya kuukamata. Kwa nini?

Kwa kweli, shauku ya Ali ya kuwa khalifa haikuchochewa na tamaa kama Umar alivyokuwa amedai ingawa hata hivyo hakuna kosa lolote katika kuwa na tamaa. Ali alitaka kuwa khalifa kwa sababu alijua kwamba yeye na yeye peke yake ndiye aliyekuwa na uwezo wa kukiongoza chombo cha Uislam katika mkondo uleule ambao Mtume wa Allah swt. ameupangilia kwa ajili yake. Watu wengine, yeye alijua, waliukosa uwezo huu.

Taasisi ya ukhalifa ambayo ilikuwa ni urithi wa Muhammad, Mtume wa Allah swt., na ambayo kwa hiyo, ilipaswa kuwa ishara ya unyofu na mamlaka ya kiroho ya Uislam kwa dunia yote, imekuwa, badala yake, katika muda wa robo tatu karne tangu kifo chake, ni ishara ya anasa isiyofifishwa na ubeberu wa dhahiri. Mabadiliko makubwa yamejitokeza katika mtindo wa maisha wa Waislam.

Badala ya kuigiza maisha halisi na ya kimaadili ya Muhammad (s.a.w.w.), wengi wao waliiga mitindo ya maisha ya kigeni. Kilichowasukuma wao sasa, hakikuwa ni maadili ya Kiislam bali ni tamaa ya kuwa matajiri na wenye mam- laka kwa gharama yoyote ile. Ule urahisi wa asili na kule kupenda usawa kwa enzi za Mtume wa Uislam, hakukubakia tena. Ubora wa maisha ya umma kwa dhahiri kabisa ulikuwa umeshuka.

Ali aliyajua yote haya vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Alikuwa akiyapima mapigo ya moyo ya umma wa Waislam, na alikuwa amefuatilia maendeleo yake au kukosa maendeleo kwake katika pande zote.

Ali pia alijua kwamba ukhalifa haukua tena kitu ambacho mtu anaweza kukichukua na “mazuri na matatizo yake.” Mazuri yote yalikuwa yametoweka; na yote yaliyokuwa yamebakia, yalikuwa ni yale matatizo yake. Kuukubali ukhalifa sasa kutakuwa na maana tu ya kujitwika matatizo hayo. Mwaka 656 ukhalifa ulikuwa urithi wa fujo na kasoro.

Ali aliona kwamba kama ataukubali ukhalifa, kutakuwa na njia mbili za wazi mbele yake, na itambidi atwae mojawapo. Njia moja itakuwa ni kufuata mkondo wa matukio; kuridhia katika kushuka kwa jumla kwa maadili; kufumbia macho ufisadi na tamaa ya mali ya magavana wa majimbo; kuruhusu urasimu katika kunyonya na kukandamiza umma; na kuvumilia vitendo visivyo vya Kiislam na vya upagani mamboleo vya waungwana wapya. Lakini njia kama hiyo ni kinyume na Uislam, na kwa hiyo, ilikuwa ni ya kinyume zaidi kwake.
Njia ya pili kwa Ali, ilikuwa ni kukubali upinzani wa dunia nzima ambao lazima utajipanga wenyewe dhidi yake, na kupigana nao bila kujali matokeo yake madhali ulikuwa unavunja amri za Allah swt. Kama atafanya hivyo, atakuwa anamuigiza tu rafiki na bwana wake wa zamani, Muhammad (s.a.w.w.). Huyu pia aliipinga dunia yote na alipigana dhidi yake bila ya kujali matokeo yake pale alipotangaza ujumbe wake kwa mara ya kwanza. Ali alijua kwamba ikiwa ataukubali ukhalifa, lile tabaka jipya la waungwana wa Kiarabu lita- mpinga, na utawala wake utaanza na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita vya wenyewe kwa wenyewe sio mwanzo wenye ndege njema lakini ni ipi njia nyingine mbadala kwake?

Chaguo lililokuwa mbele ya Ali halikuwa kati ya kushinda vita vya wenyewe kwa wenyewe, kama ilikuwepo moja, wala sio kupigana kamwe; badala yake lilikuwa, kati ya ni lipi lililokuwa sawa na lipi ni makosa; kati ya ukweli na uongo; kati ya kushika kanuni na kufuata siasa-halisi. Alitaka kujenga upya miundombinu ya jamii ya Kiislam au hasa kurudisha ile miundombinu kama vile tu ilivyokuwa wakati wa Mtume wa Allah swt. laki- ni alitambua kwamba angeweza kufanya hivyo tu katika meno ya upinzani uliodhamiriwa hasa kutoka kwa Makuraish.

Ali aliyapima yote haya, na kisha bila kutaka kuanza ukhalifa wake kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe, akalikataa ombi la masahaba la kuwa khalifa wa Waislam.

Mwandishi wa kitabu cha Kitabul-ul-Imama was-Siyassa anatoa maelezo yafuatayo ya matukio haya:

Wakati ujumbe wa Muhajirina na Ansari ulipomwendea Ali na kumwomba kuukubali ukhalifa, yeye alikataa. Ujumbe huo ukarudi Msikitini na ukatoa taarifa ya kushindwa kwake kwa masahaba waliokuwa wapo hapo. Lakini hao masahaba wakasema, “Wakati habari za kifo cha Uthman zitakapofika kwenye sehemu nyingine za himaya hii, hakuna atakayesita kuuliza kama khalifa mpya amechaguliwa au la, na vurugu ambayo sasa ipo kwenye mipaka ya Madina tu, itaenea kwenye majimbo yote. Kuna njia moja tu ya kudhibiti uhalifu usienee, na hiyo ni kumlazimisha Ali kuwa khalifa. Kwa hiyo, rudini kwake, na sisitizeni juu ya kuchukua kwake madaraka ya serikali, na msirejee mpaka awe amekubali kufanya hivyo. Kwa njia hii, habari za kifo cha Uthman na kupanda kwa Ali kwenye kiti cha mamlaka, zitasafiri pamoja kwenda kwenye kila sehemu ya Dar-ul-Islam, na hali itabakia shwari chini ya udhibiti.”

Ujumbe huo ulirudi kwenda kumuona Ali, na safari hii, wajumbe wake walivuka mipaka ya ushawishi wa kawaida. Walisema kwamba umma wa Waislam uko kwenye shida kubwa, na ikiwa yeye hataunasua, atawajibika mbele ya Allah swt. na Mtume Wake kwa ajili hiyo. Je, ataucha umma wa Muhammad kwenye hiyo shida kubwa, waliuliza. Kidokezi hiki kipya cha kufaa kilielekea kufanya kazi. Lakini akiwa mwenye kutambua huo upinzani mkubwa kwake wa Makuraish, Ali alikuwa bado anasitasita kulikubali pendekezo hilo. Yeye, kwa hiyo, aliweka kukubali kwake kwa masharti yake mwenyewe, na akauambia ujumbe huo:

“Ninao ujuzi na ufahamu kamili wa Kitabu cha Allah swt., na sunna na mwendo wa Mtume Wake. Katika kuutawala umma wa Waislam, nitatanguliza amri na makatazo yao mbele ya kitu chochote kingine. Sitaonyesha kuyumba katika jambo hili. Nitachukua madaraka ya serikali ikiwa tu sharti hili litakubalika kwenu. Kama ndivyo, na Waislam wapo tayari kuchukua kiapo cha utii kwangu, basi waambieni wakusanyike ndani ya Msikiti wa Mtume.” Ujumbe huo ulikuwa tayari kukubali masharti yoyote, na tayari kabisa ukakubali kushika masharti ya Ali. (Kitab-ul-Imama was-Siyassa)

Baada ya kifo cha Umar, msiri wake, Abdur Rahman bin Auf, alipendekeza ukhalifa kwa Ali kwa sharti kwamba atatoa kiapo cha kufuata sera na taratibu za Abu Bakr na Umar. Ali alikataa kutoa kiapo chochote, na akalikaidi pendekezo lililotolewa na Abdur Rahman bin Auf. Sasa ukhalifa ule ule ulikuwa unapendekezwa kwake kwa mara nyingine tena lakini bila ya masharti yoyote. Kwa kweli, ilikuwa ni yeye Ali ambaye alikuwa anaweka mashar- ti juu ya kukubali kwake pendekezo la kufanywa khalifa na umma wa Waislam.

Ali aliwaambia masahaba kwamba yeye hataridhia uamuzi wao; badala yake, wao watalazimika kuridhia uamuzi wake ikiwa watashikilia juu ya kuchukua kwake madaraka ya serikali. Na aliongeza kwamba wao – Waislam – wampe yeye utii usio na maswali – wakati wa amani na wa vita. Wao wakakubali. Kukubali kwao kulikuwa ni ushindi wa maadili. Umma wa Waislam ulikuwa, hatimaye, umesalimu amri kwenye maadili ya Ali!

Umma wa Muhammad, Mtume wa Allah aliyebarikiwa, katika kutafuta usalama na wokovu, walikuwa “wamemwita” Ali ibn Abi Talib kuugeuza ule mwelekeo wa kwenye vurugu na machafuko ndani ya Dar-ul-Islam. Tabari, mwanahistoria huyu, anasema kwam- ba Ali alipewa “mwito” huo siku ya Alhamisi. Raia wa Madina walikuwa na furaha sana kwa mafanikio yao ya “kumwita” yeye, na walisema kwamba wataswali Swala yao ya Ijumaa pamoja na khalifa wao mpya.

“Kwa nini isiwe aliyembora zaidi?” lilikuwa ndio swali akilini mwa umma wa Waislam pale “walipomwita” Ali kama khalifa wa Uislam. Wakati hatimae walipokuwa huru kuch- agua, wakachagua, kwa silka na bila kukwepa, yule mbora zaidi. Vilevile, wakati umma wa Waislam ulipokuwa unashikilia kwamba Ali achukue cheo cha juu kabisa katika Uislam, ulikuwa, bila kujijua, unasukumizia mbali wale “walafi wa marupurupu” ambao walikuwa wameitapakaa Dar-ul-Islam.

Siku ya Ijumaa, mwezi 18 ya Dhil-Hajj, mwaka wa 35H.A. (Juni 17, 656) Ali ibn Abi Talib aliingia kwenye Msikiti wa Mtume hapo Madina, na alielekea kwenye mimbari kupitia katikati ya kundi la Waislam. Kundi hilo lilikaa katika hali ya kungojea, mikondo ya msisimko ikilimulika kundi hilo, na lilielekea kunyanyuka kwa mtingishiko. Ilikuwepo takriban hali ya mtukuto wa dhahiri na ubadilikaji upya katika mwelekeo wa “kitaifa” wa Waislam.

Ali alishikilia upinde mkononi mwake, na akaegemea kwenye mimbari vile Waislam walipoanza kutoa kiapo cha utii kwake. Kati yake na wao, ulikuwa ni “mkataba wa wazi uliofikiwa waziwazi,” na hapakuwa na lolote la siri kuuhusu. Wengi wa Muhajirina na Ansari waliokuwa wapo Madina walimpa kiapo chao cha utii.

Ibn Hajar Makki ameandika katika kitabu chake maarufu cha al-Sawa’iq al-Muhriqah: “Wale wakongwe wa vita vya Badr wakasema (kumwambia Ali): ‘Hakuna mtu anayestahili ukhalifa zaidi yako wewe. Nyoosha mkono wako ili tuweze kukupa wewe kiapo chetu cha utii.’ Na hapo wakatoa kiapo cha utii wao kwake.”

Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza na ya mwisho katika historia ya Uislam, ambapo mtawala hakuwekwa kwa kulazimisha juu ya Waislam. Walichagua mtawala wao wenyewe, na chaguo lao lilikuwa la hiari. Haikutumika ama nguvu, wala tishio la kutumia nguvu, wala shinikizo ama mahongo, wala ulaghai wa maneno katika kuchaguliwa kwake. Hapakuwa na mpagao wa kutwaa madaraka. Kila mmoja alikuwa huru kutoa au kukataa na kiapo chake. Ali mwenyewe alikuwa akipokea viapo takriban bila kufikiri, kama alivyokuwa amezama kwenye njozi juu ya nyakati za bwana wake, Muhammad (s.a.w.w), alipokuwa akipokea kiapo cha Makuraish mara tu baada ya kutekwa kwa Makka mnamo mwaka 630.

Edward Gibbon:

“Vurugu ya makelele ya siku tano ilitulizwa kwa kutawazwa kwa Ali; kukataa kwake kungechochea mauji ya jumla. Katika hali hii ya kuhuzunisha yeye aliimarisha heshi- ma inayostahili ya kiongozi wa Bani Hashim; alitamka kwamba bora angetumikia kuliko kutawala; alikaripia ukaidi wa wageni; na akataka ridhaa rasmi kama sio ya hiari ya wakuu wa taifa.” (The Decline and Fall of the Roman Empire)

Talha na Zubeir walikuwa ndio wa kwanza wa masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) kuchukua kiapo cha utii kwa khalifa mpya. Muhajirina na Ansari ndio waliofuatia. Wakafuatiwa na watu wa kawaida. Wa kwanza ambaye hakuwa sahaba kuchukua kiapo cha utii kwa Ali alikuwa ni Malik ibn Ashtar, askari wa upanga mashuhuri zaidi wa Arabia.

Hudhaifa ibn Al-Yamani alikuwa ni mmoja wa masahaba maarufu wa Mtume (s.a.w.w.). Alikuwa akiishi huko Kufa na alikuwa amezuiwa kitandani na maradhi ya muda mrefu. Alipozisikia habari za kupanda kwa Ali kwenye kiti cha utawala, aliomba apelekwe kwenye msikiti mkuu wa Kufa. Wakati Waislam walipokusanyika kwa ajili ya Swala, alipanda kwenye mimbari na akasoma khutba. Alimshukuru Allah swt. kwa baraka Zake, na akaomba rehema Zake Allah swt. ziwe juu ya Mtume Wake, Muhammad (s.a.w.w.), na juu ya kizazi chake, na akasema:

“Enyi Waislam! Nimepokea habari kwamba huko Madina, Ali ibn Abi Talib amechaguliwa kuwa mrithi wa Mtume wa Allah swt. Mimi ninawasihi mtoe kiapo chenu cha utii kwake kwa sababu yeye yuko pamoja na Haki na Haki iko pamoja na yeye, na baada ya Mtume mwenyewe, yeye ndiye mbora wa wale wote walioumbwa au watakaoumbwa kamwe.
Hudhaifa ndipo kwa njia ya ishara akaweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto, na akasema: “Ewe Allah! Kuwa Wewe Shahidi kwamba nimechukua kiapo cha utii kwa Ali, khalifa wangu mpya. Zikubali shukurani zangu kwamba Wewe umenipa muda wa kutosha mpaka kumuona yeye akiwa mtawala wa umma wa Muhammad, Mtume Wako.”

Hudhaifa alirudishwa nyumbani kwake, na siku chache baadae akafariki. Alikuwa mmoja wa marafiki waaminifu na wapendwa sana wa Muhammad Mustafa.

Ansari, kwa jumla, walikuwa wameonyesha shauku kubwa sana katika kumleta Ali kwenye mamlaka lakini miongoni mwao walikuwepo watu wengine ambao walivizuia viapo vyao vya utii kwake. Hawa walikuwa ni:

• Zayd bin Thabit

• Hassan bin Thabit

• Kaab bin Malik

• Abu Said Khudri

• Muhammad bin Maslama

• Nu’man bin Bashir

• Rafa’ bin Khudaij

• Maslama bin Mukhalid

• Kaab bin’Arja

Miongoni mwa watu wa Makka, masahaba wafuatao hawakutoa kiapo chao cha utii kwa Ali:

• Abdallah bin Umar bin al-Khattab

• Saad bin Abi Waqqas

• Mughira bin Shaaba

• Abdallah bin Salam

• Qadama bin Ma’azun

• Suhaib bin Sinan

• Wahban bin Saifi

• Usama bin Zayd bin Haritha

Wakati nadhari ya Ali ilipokuwa imeelekezwa kwa wale watu ambao walikuwa hawakumpa kiapo chao cha utii, alisema kwamba utii sio kitu ambacho kinaweza kupatikana kwa nguvu. Ili kueleweka vema alisema, utii ni lazima uwe wa hiari. Baadae, ilifikishwa taarifa kwake kwamba watu hao hao walikuwa wakitoroka kimya kimya kuondoka Madina. Ali hakufanya jaribio lolote la kuwazuia. Alisema kwamba chini ya utawala wake, kila mtu alikuwa na uhuru wa kukaa Madina au kuondoka, na kwamba yeye binafsi hatamlazimisha mtu yeyote kukaa au kuondoka. Wapinzani wake wa kisiasa wote waliondoka Madina, na wengi wao walikwenda Syria au Makka.

(Miezi michache baadae, vita ya Basra au vita vya Ngamia vilipiganwa. Abdallah bin Umar bin al-Khattab na Saad bin Abi Waqqas walitoa tamko la kutokuwa upande wowote katika vita hivyo. Kwao kulikuwa ni kutokuwa na upande wowote kwa hiari juu ya masuala ya haki na upotofu ingawa walijua ni nani alikuwa haki na nani alikuwa muovu. Wengine wao pia walidai kuwa walikuwa “hawafungamani” na upande wowote, lakini walikuwa “hawafungamani” kwa faida ya maadui wa Ali).

Yaqubi, mwanahistoria huyu, anasema kwamba baada ya kutawazwa huko, Sa’sa’a ibn Sauhan ‘Abidi, aliyekuwa sahaba, alimwambia Ali: “Wallahi, umeleta heshima na utukufu kwenye ukhalifa. Ukhalifa haukuleta heshima na utukufu kwako wewe. Umeunyanyua kwa kuukubali; wala haukukunyanyua wewe. Wewe hukuuhitaji, bali wenyewe ulikuhitaji wewe.”

Mwanahistoria mwingine, Khattib Baghdadi, amemnukuu Imam Ahmad bin Hanbal akisema: “Ukhalifa haukuwa pambo kwa Ali; yeye ndiye alikuwa pambo kwa ukhalifa.”

Imam Ahmad bin Hanbal aliuweka ukweli wote kwa kifupi. Ali alikuwa kwa hakika ndiye pambo na utukufu wa ukhalifa.
Wakati huo, Muadhini akaleta adhana kwa ajili ya Swala ya Ijumaa. Ali, khalifa mpya, akaongoza jamaa hiyo. Baada ya Swala, alitoa hotuba ya uzinduzi. Alianza mazungumzo yake kwa kumtukuza Allah swt., na kwa kumshukuru Yeye kwa neema na baraka Zake nyingi zisizo na idadi mojawapo ikiwa ni kwamba Ameirudisha haki ya Ali kwake.

Alimtakia rehema na amani za Allah, juu ya Muhammad Mustafa na watu wa Nyumbani kwake, na kisha akasema: “Enyi Waislam! Mmenipa mimi kiapo chenu cha utii, na ninajua kwamba hamku- fanya hivyo bila ya busara ya kutosha. Hata hivyo, malengo yenu na malengo yangu katika kazi zilizoko mbele yetu, sio lazima ziwe zinafanana. Ninataka kuwahama- sisha kwa ajili ya utii na ibada kwa Allah swt; lakini wengi miongoni mwenu wanategemea kwamba nitawapa mali nyingi au vyeo vikubwa katika serikali. Hiki ni kitu ambacho hakitatokea.

“Kumbukeni kwamba kuna njia mbili za maisha; ya haki na ya upotovu. Wengine wenu watatwaa ile njia ya haki na wengine ile ya upotofu. Mnao uhuru wa kuchagua. Lakini kama mtaona kwamba kundi kubwa limefuata ile njia ya upotofu, msifadhaishwe au kushangazwa nalo. Imekuwa kama hivyo mara nyingi, na dunia imejaa ukweli ambao kuaminika kwake ni kwa mashaka. Lakini haki na uadilifu vitashinda mwishoni hata kama ni katika muda maalum vitaonekana kuwa katika hali ya kujihami.

“Kwa kweli, pale Allah swt. alipomtuma Muhammad kama Mtume Wake kwa ulimwengu huu, hapakuwa na hata mtu mmoja katika Arabia yote aliyekuwa akijua chochote kuhusu uongofu na unyoofu. Aliwatoa Waarabu katika giza la dhambi na uovu mpaka wakaiona nuru ya uongofu, na wakaipata njia ya kwenye wokovu wa milele. Nilikuwa pembeni mwake tangu mwanzo wa kazi yake mpaka mwisho wake, na nilipigana dhidi ya kumuasi Allah maisha yangu yote. Sikuhisi kamwe uchovu wa mapambano hayo wala sikuogofyeshwa na upinzani wa walezi na mabingwa wa utaratibu wa kabla ya Uislam, hata kama ulikuwa wa kutisha kiasi gani.

“Enyi Waislam! Ninawasihi mnisaidie katika ratiba yangu ya kujenga upya. Allah ni Shahidi wa kauli yangu kwamba shabaha yangu kuu ni kurudisha haki katika Dar-ul- Islam (dola ya Kiislam), kama vile tu ilivyokuwa ni matilaba yake kwamba mimi nifanye hivyo. Sitapumzika mpaka niwe nimeuangamiza udhalimu. Sikilizeni hili kwa makini: Sitavuka mipaka ya Kitabu cha Allah kwa kitu chochote. Sitakuwa na upendeleo kwa yeyote yule awaye. Machoni mwangu, ninyi wote mnalingana. Nitazieneza Sheria za Allah ambazo zimehifadhiwa ndani ya Kitabu Chake, na nitafanya hivyo kwa kuzingatia vigezo tu vya Mtume Wake, Muhammad, aliyebarikiwa.

“Kazi yangu leo hii ni ile ile kama ilivyokuwa katika nyakati za Mtume wa Allah, Muhammad; rehema na amani ziwe juu yake na kizazi chake, na ni kuanzisha au kusi- mamisha upya Ufalme wa Allah swt. katika dunia hii.”

Kwa maneno haya, Ali alionyesha sera za serikali yake. Alifafanua malengo yake, na akaelezea namna ya jinsi atakavyoyafanikisha. Alilenga katika kuirudisha upya ile ofisi kuu kabisa katika Uislam, na alizieleza kwa mukhtasari zile taratibu za falsafa yake ya kisiasa.

Watu wenye utambuzi waliweza kuhisi kwamba serikali ya Ali ingekuwa tofauti kabisa na zile serikali zilizopita, sio tu katika mtindo, sura na nguvu, bali pia katika sifa bainifu, msingi na falsafa. Walihisi kwamba kutakuwepo na tofauti ya ukamilifu na ubora kati ya serikali hizo.

Walijua kwamba atahakiki mmomonyoko na uharibifu wa viwango vya maadili binafsi na ya jamii. Kupanda kwake madarakani, kwa hiyo, hakukupendelewa na walezi wa mfumo wa kijamii ambao mategemeo yake yalikuwa upendeleo na nguvu, na kutokujali maadili na ukiukaji wa kanuni.

Kwa mshangao kabisa, ilionekana kana kwamba historia ilikuwa inataka kujirudia yenyewe. Huko Makka, Muhammad Mustafa alikabiliwa na walezi wa mfumo wa jamii ambao ulitegemea upendeleo, nguvu na unyonyaji. Alipojaribu kuubadili mfumo ule, wasi- mamizi wake walimpinga. Upinzani wao ulisababisha mapambano ya silaha. Sasa Ali alikabiliwa na mfumo uleule, na jaribio lake la kuubadili, lilikuwa pia liishie kwenye mapambano ya silaha na wasimamizi wake.

Kwa upande mwingine, kupanda madarakani kwa Ali kulipokewa sana na kwenye tabaka jingine la watu – lile litokanalo na masikini, mafukara, wasiojiweza, wasio na nguvu, walionyonywa, na wale waliokuwa wanaishi kwa woga na hofu kuu. Watu wa tabaka hili walijua, kana kwamba kwa silika, kwamba Ali atawapatia uhuru kutokana na hofu na umasikini. Walijua vilevile kwamba akipewa nafasi, Ali ataufanyia kazi uhusiano wote wa jamii ya Waislam, na ataubadilisha. Mahadhi, mwendo na mwelekeo wa hotuba zake vili- washa mishumaa ya nuru ya matumaini mapya na kanuni fulani za maisha ndani ya nyoyo zao, na waliweza kutabiri kwamba ataweza kuhuisha ule urithi wa kisiasa wa Muhammad, Mtume wa Allah swt. katika serikali yake.

Hali Ya Umma Wakati Wa Kuingia Madarakani Kwa Ali

Wakati Ali alipochukua mamlaka ya serikali mikononi mwake, alikabiliwa na hali ya kutisha sana. Nchi yote ilikuwa inasisimka kwa uchochezi, na maadui zake walitapakaa kila mahali kama mavu. Wanahistoria wawili wa kisasa wa Pakistani, Profesa Sayed Abdul Qadir na Profesa Muhammad Shuja-ud-Din, wametoa mukhtasari wa hali ya Dar-ul-Islam katika mwaka 656 kama ifuatavyo:

Waislam hawakuwa tena wameungana. Walikuwa wamegawanyika katika kambi nyingi. Waislam wengi waliweka maslahi yao binafsi mbele ya maslahi ya jumla ya umma.

Mapambano ya hivi karibuni yameleta mikononi mwa Waislam ule utajiri mkubwa wa himaya mbili tajiri sana za dunia – ya Uajemi na ile ya Roma. Kila mmoja wao alitaka sehemu kutoka kwenye mafanikio haya, na walijaribu kunyakua kila kile mtu alichoweza. Katika utafutaji huo wa kikatili wa pesa, Waislam wengi waliweka pembeni mifano bora ya Kiislam kana kwamba ilikuwa isiyopasika.

Ingawa Talha na Zubeir, wawili wa masahaba wenye nguvu sana, walikuwa wa kwanza kutoa kiapo cha utii kwa Ali, walikuwa wa kwanza pia kukikana. Kwa kuvunja kiapo chao, waliusukuma umma kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mu’awiyah alikuwa gavana wa Uthman huko Syria. Ule uasi wa Talha na Zubeir dhidi ya mamlaka halali huko Madina, ulimtia moyo yeye wa kuukaidi. Ali alimtaka yeye atoe kiapo chake cha utii kwake lakini alikataa, na badala yake, alidai kutoka kwa Ali, zichukuliwe hatua dhidi ya wauaji wa Uthman. Mu’awiyah alikuwa na mapenzi kidogo sana na Uthman lakini alikuwa na mapenzi makubwa sana ya kuongezea matatizo ya Ali. Alitegemea kwamba Ali atajaribu kuwaadhibu wale watu wote ambao walikuwa wameasi dhidi ya Uthman, nao wangempinga yeye, na upinzani wao ungesababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita vya wenyewe kwa wenyewe hapo Madina, yeye aliwaza moyoni, vingefanya iwezekane kwa yeye kuukamata ukhalifa.

Lakini Ali hakunasa katika mtego wake, na alimwambia Mu’awiyah: “Kwanza nipe kiapo chako cha utii, na uniache nirudishe amani katika dola. Mara hali itakaporudia kwenye kawaida, ndipo sisi wote, tutakapowafikisha wauaji wa Uthman mashtakani, na haki itatawala.”

Lakini Mu’awiyah hakuwa na nia ya kutoa kiapo cha utii kwa Ali. Yeye, kwa hiyo, alishikilia juu ya kukamatwa na kuuawa kwa wauaji wa Uthman.

Wakitoa maoni yao juu ya majibu ya Mu’awiyah kwa Ali, maprofesa hawa wawili wanaendelea kusema kwamba: “Kwa maoni yetu sisi, Ali alikuwa na haki kabisa. Maslahi ya watu binafsi, hata kama yangekuwa na umuhimu kiasi gani, hayawezi kutolewa muhanga kwa maslahi ya ‘Taifa.’

Hata kuwepo na misiba mikubwa kiasi gani ya mtu mashuhuri sana, umoja wa nchi lazima ulindwe kwa gharama zote. Maslahi ya ‘Taifa’ bado yanabakia kuwa ni muhimu, na hayawezi kutolewa muhanga kwa ajili ya maslahi ya mtu binafsi. Kuhakikisha usalama wa dola ya Kiislam ni wajibu wa kwanza wa kiongozi wa umma wa Waislam. Ikiwa kama Ali angefuata ushauri wa Mu’awiyah, vita vingezu- ka katika kila sehemu ya dola. Lakini maadui wa Ali hawakushiriki katika kujishuhulisha kwake juu ya amani, na msimamo wao ulisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe miongoni mwa Waislam. Kama Talha, Zubeir na Mu’awiyah wangekuwa na ukweli wowote, wangeyaweka chini maslahi yao wenyewe mbele ya maslahi ya Uislam, na Waislam wasingemwaga damu ya kila mmoja wao.” (History of Islam, Part 1)

Yaliyoelezwa hapo ni makadirio sahihi ya ghasia za kisiasa katika Bunge la Uislam wakati Ali alipochukua madaraka ya serikali. Wanahistoria wengine wengi pia wameyachambua matukio yaliyotokea kabla ya vile vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Waislam.

Wamejaribu kuonyesha sababu zake lakini wengi wao, inavyoelekea, wameacha jambo muhimu sana, au kama hawakuliacha, basi wamejaribu kulificha.

Kuporomoka kwa bunge la Saqifah kulikuwa na uhakika wa kufuatiwa na ghasia nyingi, kubwa. Lakini jambo ambalo wanahistoria hawa walikuwa hawako tayari kulikubali ni kwamba vile vikwazo vikali vilivyochipukia katika wakati wa ukhalifa wa Ali, vilipandikizwa katika nyakati za (viongozi) waliomtangulia. Maasi yaliyotokea ghafla katika wakati wake, yote yalipata mizizi wakati wa huko nyuma. Sir John Glubb, mwanahistoria wa kisasa, anaandika katika kuhusu ukhalifa wa Uthman bin Abdul Aziz kama ifuatavyo:

“Utawala wa Umar bin Abdul Aziz, ulikuwa umesafika kabisa kutokana na maasi na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, lakini bado inaweza kujengwa hoja kwamba ilikuwa ni katika wakati wake ambapo mbegu zilipandwa, za yale mapinduzi ambayo yalikuwa yaangushe kabisa himaya hiyo. Hili halikuwa lenye kushangaza bali hasa lilikubaliana na maendeleo ya kawaida ya kisiasa. Kwani imekuwa ikitokea mara kwa mara kwamba nchi imebakia shwari katika vipindi vya utawala wa kidhalimu na kidikteta lakini kwamba uasi ulitokea ghafla mara tu utawala wa haki na huru zaidi ulipokuwa umeanzishwa. Hivyo ule ukhalifa mwema wa Umar bin Abdul Aziz ulianzisha vuguvugu ambalo lilikuwa liongozee kwenye kuiangamiza familia yake.” (The Empire of the Arabs, uk.175, 1963)

Sir John Glubb ametoa tafsiri sahihi na potovu pia katika kifungu kilichoelezwa hapo juu. Yuko sahihi katika kueleza kwamba “imetokea mara nyingi kwamba nchi imebakia shwari katika vipindi vya utawala wa kidhalimu na kidikteta lakini maasi yakatokea ghafla mara tu baada ya utawala wa haki na huru zaidi ulipoanzishwa.” Falme ya Waarabu ilikuwa shwari katika vipindi vya utawala wa kidhalimu na kidikteta vya serikali ya Saqifah lakini uasi uliibuka ghafla mara baada ya ule utawala wa haki na huru wa Ali ulipokuwa umeanzishwa.

Lakini hatuwezi kukubaliana na mwanahistoria huyu pale anapodai kwamba ilikuwa ni katika wakati wa Umar ibn Abdul Aziz ambapo “mbegu zilipandwa, za yale mapinduzi ambayo yaliangamiza kabisa ufalme wa Bani Umayya.” Mbegu kama hizo hazikupandwa wakati wa Umar ibn Abdul Aziz bali zilipandwa na watangulizi wake na warithi wake pia.

Wala hatuwezi kukubaliana na madai ya mwanahistoria huyu kwamba “ukhalifa mwema wa Umar ibn Abdul Aziz ulianzisha vuguvugu ambalo lilikuwa lisababishe kuangamia kwa familia yake.” Ukweli wenyewe ni kinyume chake. Yumkini kabisa kwamba mwenendo wa kitakatifu wa Umar ibn Abdul Aziz ulitoa ucheleweshaji kwa muda kwa Bani Umayya, na kwamba, bila ya yeye, wao wangeweza kuangamia mapema zaidi kuliko pale walipoangamia.

Umar ibn Abdul Aziz hastahili kwenye mtindo usiobadilika wa Bani Umayya. Alikuwa mchamungu na mpenzi wa Mungu sana na wao walikuwa wasiomjua Mungu kiasi kwamba hawakuweza kupatana. Walimuua kwa kutumia sumu.

Dr. Hamid-ud-Din:

“Hapakuwa na mapambano makubwa wala nchi yoyote mpya iliyotekwa wakati wa ukhalifa wa Umar ibn Abdul Aziz. Na bado ukhalifa wake ulikuwa maarufu sana katika historia ya Uislam kwa sababu ya mabadiliko aliyoyaanzisha. Alihuisha democra- sia halisi ya Kiislam mienendo ya Khulafa-i-Rashida (makhalifa walioongoka).

Kuanzia wakati wa Mu’awiyah, ukhalifa uligeuka kuwa ni serikali binafsi ya khalifa. Yale maovu yote ambayo ni sehemu ya serikali za kidikteta na kidhalimu, yaliingia kwenye ukhalifa. Watu walikuwa wamepoteza uhuru wao. Baytul-Mal (hazina ya umma) imekuwa ni mfuko binafsi wa mtawala. Hakuna chochote kilichotumika kuondoa dhiki za maskini, na yote ilitumika kwenye fahari na starehe za tabaka la watawala. Umar ibn Abdul Aziz alikusudia kukomesha vitendo hivi. Kitu cha kwanza alichokifanya, kilikuwa ni kukamata yale mashamba makubwa ambayo wafanyabiashara wa Bani Umayya walijitwalia wao wenyewe.
Njia nyingi zisizokuwa za haki na za haramu zilitumika kulita mapato zaidi kwenye hazina ya umma. Kwa mfano, wale Dhimmiy (wasiokuwa Waislam wanoishi chini ya ulinzi wa Dola ya Kiislam)), ambao walikuja kuukubali Uislam, walilazimishwa kulipa jizya (kodi ya kichwa). Kwa mujibu wa sheria ya Qur’an, ni wale raia wasiokuwa Waislam tu wa Dola ya Kiislam, waliopaswa kulipa jizya. Umar ibn Abdul Aziz ali- tuma maagizo kwa magavana wote katika majimbo kwamba endapo Dhimmiy yoyote atasilimu, basi asidaiwe jizya. Aliikomesha tabia hii, na mamia ya maelfu ya Dhimmiy wakawa Waislam baada ya kuenezwa kwa agizo hili.

Mu’awiyah alikuwa ameanza desturi ya kumlaani Ali ibn Abi Talib hadharani.Yeye mwenyewe na magavana wake na watendaji wa dola walitumia takriban lugha isiyo na kiasi na ya matusi kutoka juu ya mimbari za misikiti juu ya Ali. Baada ya Mu’awiyah, warithi wake waliiendeleza tabia hii. Lakini Umar ibn Abdul Aziz ali- ikomesha. Aliwaamuru magavana wake kusoma Aya za Qur’an kutoka juu ya mimbari badala ya kumlaani Ali.

Mabadiliko haya hayakupendelewa na kundi la wale wenye mamlaka la Bani Umayya, na mapenzi ya khalifa ya kufuata sheria na haki hayakumfanya apendwe sana pamoja nayo. Wafanyibiashara wa Bani Umayya waliamini kwamba kama angetawala himaya hiyo kwa muda mrefu wa kiasi chochote kile, basi watakuja kupoteza mamlaka yao na marupurupu yao. Wao, kwa hiyo, walibuni njama, na wakamlisha sumu katika chakula chake. Alikufa kutokana na athari za sumu hii mnamo mwezi wa Rajab wa mwaka 101 H.A.
(720 A.D.)
(History of Islam, kilichochapishwa na Ferozsons Ltd, Karachi na Lahore, Pakistan, uk.324, 331 3,1971).

Ilikuwa haikwepeki kwamba mtu kama Umar ibn Abdul Aziz angekuwa shahidi. Yeye ni mmoja wa Waislam waliokufa kishahidi. Mwenyezi Mungu aihurumie roho yake njema.

Ali alikabilana na mabishano ya mawanda makubwa mno. Lakini hayakumtisha. Kwa moyo safi na akili yenye msimamo juu ya Mapenzi ya Allah, swt., aliianza kazi ya kurudisha amani na utawala wa Allah kwenye dola ya Uislam. Kuchukua kiapo kwa Ali hakukuwahi kumalizika wakati uasi ulipoibuka pande zote kumzunguka yeye. Kama aliushughulikia mmojawapo, mwingine ulichomoza kichwa chake. Hivyo ile miaka michache ya utawala wake ilitumika katika kuizima. Baadhi ya wakosoaji wake walisingizia kwamba maasi hayo yalikuwa ni matokeo ya “ujinga” wake.

Maasi ya wakati wa utawala wa Ali hayakusababishwa na ujinga wake. Kama ilivyoonyeshwa hapo juu, yaliota mizizi huko nyuma. Mtu mwingine yoyote angeweza kukabiliwa na wimbi hilo hilo la matatizo, na inaelekea kabisa kwamba angeshindwa kupambana nayo.

Kwa hali hiyo, Ali aliendesha utawala wa nchi, na pia alijaribu kuyazuia maasi hayo kama ilivyokuwa wajibu wake. Alilishinda kundi moja la maasi huko Basra, na angeweza kul- ishinda lile jingine huko Siffin kama kundi hilo lisingechukua kimbilio kwenye usaliti. Hata katika nyakati hizi za ghasia, alitekeleza mabadiliko muhimu ya kiuchumi na kijamii.

Ingawa sababu za maasi zilitokea kabla ya ukhalifa wa Ali mwenyewe, chache kati ya hizo zinaweza kuelezwa zaidi kama ifuatavyo kwa uelewa mzuri zaidi wa matukio yaliyotokea baadae.

1. Sera ya Ali ilikuwa ni ya ki-Qur’an halisi. Hakuwa aafikiane na maadili na taratibu za Kiislam kwa ajili ya kung’ang’ania tu kwenye madaraka na mamlaka. Kama angekuwa ametwaa sera za kisiasa hasa pia, angeweza kufanikiwa vizuri sana lakini kufanya hivyo kungebadili mwelekeo wa serikali yake kutoka ile ya Kiislam na kuwa ya “kikabila.”

Ahmad Hasan Zayyat wa Misri, anasema ndani ya kitabu chake, Adab al-Araby (uk.174) hivi: “Ali hakuyumba kabisa katika masuala ya dini, na hakuujua udanganyifu katika mambo ya kidunia. Ilikuwa ni utukufu huu wa tabia yake ambao Mu’awiyah aliutu- mia kwa manufaa yake.”

2. Ali hakujaribu kuwaridhisha matajiri na wenye nguvu dhidi ya masikini na wany- onge. Yeye siku zote aliyaweka maslahi ya masikini na wanyonge mbele ya maslahi ya tabaka la waungwana wa Kiarabu. Tabaka hili la waungwana wa Kiarabu lililichukia hili, na lilimuonyesha kuchukia kwao.

Alipokuwa akigawanya mapato ya hazina ya umma, Ali hakutofautisha kati ya mabwana na watwana, matajiri na masikini, na Waarabu na wasiokuwa Waarabu. Machoni mwake, wote walikuwa sawa. Mamwinyi wa Kiarabu walilalamika dhidi utendewaji wa namna hii lakini yeye aliyapuuza malalamiko yao. Mara malalamiko yao yalilipukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

3. Mara tu baada ya Ali kuchukua madaraka ya serikali, aliwauzulu magavana na watendaji wote waliokuwa wameteuliwa na Uthman. Lakini wengi wao hawakuwa na nia ya kuachia nafasi zao.

Kufukuzwa Kwa Magavana Wa Uthman

Wakati Ali alipochukua madaraka ya serikali, magavana na wakusanya kodi wa Uthman walikuwa wakkipora nchi bila ya hofu ya kuhojiwa na serikali kuu. Kitendo cha kwanza cha Ali kilikuwa ni kutoa amri ya kufukuzwa kwao.

Mughira bin Shaaba alikuwa mmoja wa masahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Umar alikuwa amemteua kuwa gavana wa Kufa lakini Uthman alimfukuza. Yeye alikuwa hajachukua kiapo cha utii kwa Ali lakini alimshauri dhidi ya kufanya mabadiliko yoyote ya mazito katika sera na watumishi. Alisema kwamba kama magavana walioteuliwa na Uthman hawakutambua mamlaka yake yeye (Ali) kama khalifa.basi asiwaondoe kwenye kazi zao. Alimtahadharisha Ali kwamba kama atawafukuza, kabla ya kuimarisha madaraka yake mwenyewe, wataasi dhidi ya mamlaka yake.

Binamu wa kwanza wa Ali, Abdallah ibn Abbas, pia alimpa ushauri ambao, kimsingi, ulikuwa sawa na ule wa Mughira. Busara, alisema, inaamuru uangalifu kwa wakati huu. Lakini ushauri kama huo ulikuwa haukubaliki kwa Ali. Yeye aliamini kwamba ni mwenye kuwajibika kwa Allah swt. kwa matendo yake yote, na asingeweza, kwa hiyo, kuruhusu watu wasiofaa na madhalimu kutawala juu ya Waislam. Yeye, kwa kweli, alijiona yeye mwenyewe mwenye kuwajibika kwa Allah swt., sio tu kwa matendo yake binafsi, bali pia kwa matendo ya magavana wake. Yeye kwa hiyo, aliweka imani yake kwa Allah swt., akijua kwamba alikuwa anafanya jambo la sawasawa, na akakataa kubatilisha maagizo yake.

Colonel Osborne:

“Ali alishauriwa na baadhi ya washauri wake kuahirisha kuwafukuza wale magavana waovu waliokuwa wameteuliwa kabla mpaka yeye mwenyewe atakapokuwa salama dhidi ya maadui zake wote. Ngome ya Uislam hii, shujaa asiye na woga wala fedheha alikataa kuwa na hatia ya unafiki wowote au kukubaliana na dhulma. Hii tabia yake ya kiungwana isiyoyumba ilimgharimu dola na maisha yake. Yeye kamwe hathamini kitu chochote juu ya haki na ukweli.

Watu wengine wanadhani kwamba kama Ali asingewafukuza magavana wa Uthman, asingewachochea katika kumpinga yeye. Lakini wazo kama hilo limeegemea kwenye ushamba. Magavana hao wa Uthman wangempinga Ali bila ya kujali ni nini alichokifanya. Walikuwa ni maadui zake wa tangu zamani.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu za kwa nini Ali aliwafukuza magavana wa Uthman:

1. Makusudio ya Ali yalikuwa ni kurudisha ile serikali ya Muhammad Mustafa, na kutekeleza mfumo wa Kiislam. Ili kufanya hivi, ilimbidi “kusafisha” ile serikali aliyokuwa ameirithi, kwa kuondoa kutoka humo lile kundi la walafi la Bani Umayya. Badala yao, ilikuwa ateuwe watu wachamungu ambao waliamini kwamba wanawajibika kwa Allah swt. kwa yote yale ambayo wameyatenda.

2. Waislam walikuwa wamemuomba Uthman awaondoe magavana wake wenye majivuno na ubinafsi, na kuteuwa watu wachamungu badala yao. Lakini aliwageuzia sikio la uziwi kwenye maombi yao ambapo walichukua hatua zingine kulazimisha kubadilishwa kwa magavana. Kama Ali angepitisha muda kwenye suala hili, wangeipindua serikali yake kama vile walivyoipindua ile serikali ya mtangulizi wake.

3. Kama Ali asingewafukuza magavana wa Uthman, angejifanya mwenyewe awe mwenye kubanwa na kosa la “kuwa na hatia kwa ushirikiano.”

4. Mu’awiyah hakuwa ametosheka na kutawala Syria peke yake; alitaka kutawala dola yote ya Waislam kama khalifa wake. Alipogundua kwamba Uthman alikuwa amejifanyia maadui wengi sana yeye mwenyewe binafsi, alijaribu kutumia fursa ya hali hiyo. Alimshauri Uthman kwamba angeondoka Madina na aende naye (Mu’awiyah) Syria, ambako, alimhakikishia yeye, kwamba atakuwa salama ambapo katika makao makuu yake mwenyewe, alimtahadharisha, kuwa angeweza kuuawa. Mu’awiyah alikuwa na sababu nzuri sana za kujaribu kumchukua Uthman kwenda naye Damascus, Uthman angekuwa “khalifa asiyekuwa na madaraka.” Mu’awiyah angemnyang’anya mamlaka yake yote na kuyachukua mikononi mwake mwenyewe, na kwa hiyo, angekuwa khalifa asiyepingika katika uhai wake Uthman mwenyewe, na halali kisheria baada ya kifo chake Uthman. Lakini Uthman hakwenda Syria, na mkakati wa Mu’awiyah haukufanya kazi. Lakini wakati Uthman alipouawa, Mu’awiyah alianzisha kampeni yake dhidi ya Ali akitafuta kulipiza kisasi kwa ajili ya damu yake. Ali hakuwa na fursa japo ndogo ya uchaguzi katika jambo hilo ila kumfukuza Mu’awiyah.

5. Uthman alikuwa ameteua magavana, sio kwa sababu walikuwa na uwezo wowote ule au kwa kuwa walipenda kuwatumikia Waislam. Aliwateua kwa sababu tu walikuwa na udugu naye. Ali aliuona uchaguzi huu kama ni kuingilia kati juu ya haki za wale watu ambao walikuwa wanafaa kwa uwezo wao, uchamungu, na utumiishi kwa Uislam, kutawala Waislam. Yeye, kwa hiyo, akawaondoa hao.

6. Uthman alikuwa amewateua watu wa familia yake mwenyewe kama magavana wa majimbo. Magavana wake walikuwa na watu na vifaa muhimu kwa vita. Uthman alikuwa amezingirwa, chini ya ulinzi ndani ya kasri lake kwa muda wa siku 49. Alituma maombi mengi sana kwao ili waje kumuokoa lakini hawakuja, na akauawa. Ikiwa kama magavana hawa wameweza kumtelekeza mfadhili wao wenyewe kwa urahisi namna hiyo, ni vipi Ali angeweza kuwategemea wao katika kuhitajika sana kumtii yeye? Yeye kwa hiyo, aliamua kutokuwa chini ya miguu yao.

Mtu mmoja kwa jina la Abu Tufail Kinani, mkazi wa Madina, wakati mmoja alikwenda Damascus kumuona Mu’awiyah. Walipokutana, mabishano yafuatayo yalitokea kati yao:

Mu’awiyah: Ulikuwa wapi wewe wakati Uthman alipouawa?
Kinani: Nilikuwa niko Madina.
Mu’awiyah: Je, ulifanya chochote ili kuokoa maisha yake kutokana na maadui zake?
Kinani: Hapana.
Mu’awiyah: Kwa nini hukufanya? Ulijua kwamba ilikuwa ni wajibu wako kufanya kila linalowezekana ili kumuokoa yeye.
Kinani: Ninadhani ilikuwa iwe hivyo. Lakini chochote kile kilichokuzuia wewe kujaribu kuokoa maisha yake, pia kilinizuia na mimi kujaribu kuokoa maisha yake.

Magavana Wapya

Katika mwezi wa Muharram wa mwaka wa 36 H.A., Ali aliwateua magavana wafuatao:

1. Qays Ibn Saad Ansari, Gavana Wa Misri.

Qays aliweza kuingia Misri bila ya upinzani na kuchukua mamlaka ya serikali. Huko Misri, aliwakuta Waislam wamegawanyika katika makundi matatu. Moja lilikuwa likiundwa na wafuasi wake mwenyewe; la pili la wapinzani wake, yaani, wafuasi wa Uthman; na kundi la tatu lilikuwa halijakata shauri katika utiifu wao. Qays aliamua kujishughulisha na haya makundi mawili ya mwisho, lakini kutoa uangalifu wa moyo wake wote kwenye utawala wa nchi.

Qays, kwa muonekano wa dhahiri, alikuwa ndiye mtu wa kuvutia sana hapo Madina.

Alikuwa mrefu, mkali na mwenye nguvu kimaumbile; na alikuwa ni mashuhuri kwa elimu yake, uchamungu na ufasaha. Alikuwa pia ni mtu wa ufahamu na uonambali mkubwa, na alikuwa halingani kabisa na watu kama akina Mu’awiyah, Amr bin Al-Aas na Mughira bin Shaaba katika maarifa na akili. Lakini kama bwana mkubwa wake mwenyewe, Ali, yeye pia hakuamini kwamba penye nia pana njia. Falsafa yake ya maisha ilikuwa ikitawaliwa na ile kanuni kwamba sera ya kisiasa lazima itegemee mafundisho ya Qur’an.

2. Uthman Bin Hunaif, Gavana Wa Basra.

Uthman aliweza pia kuingia Basra na kuchukua madaraka ya serikali. Yeye pia aliwakuta Waislam huko Basra wamegawanyika katika makundi matatu kama Qays alivyokuta huko Misri, na yeye pia alitwaa sera kama ile aliyokuwa ametumia Qays huko Misri.

Uthman bin Hunaif alitokana na familia mashuhuri ya Ansari. Alikuwa ni rafiki wa karibu wa Mtume (s.a.w.w.). Wakati wa ukhalifa wa Umar, alikuwa ndiye kamishna wa fedha wa Iraq.

3. Ammara Bin Shihab Ansari, Gavana-Mteule Wa Kufa.

Ammara aliondoka Madina kwenda kushika kazi yake huko Kufa. Lakini pale alipofika Zabala, kituo cha njiani kwenye njia iendayo Iraq, alikutana na mtu mmoja, Talha bin Khuwaylid Asadi, akitokea Kufa. Alimshauri Ammara kurejea Madina, ama vinginevyo, alisema, atakwenda kuuawa huko Kufa. Papo hapo, Ammara hakwenda Kufa, na akarudi Madina.

4. Sahl Bin Hunaif Ansari, Gavana-Mteule Wa Syria.

Sahl aliondoka Madina. Kabla hajaukuta mpaka wa Syria, alikutana na kundi la askari wapanda farasi. Walimuuliza yeye ni nani na alikuwa akienda wapi. Aliwaambia kuwa yeye ndiye gavana mpya wa Syria. Wao wakasema walikuwa ni watu wa Syria na kwamba hawamkubali mtu yoyote kama mtawala wao isipokuwa Mu’awiyah. Waliongeza pia kwamba kama angeendelea kwenda mbele zaidi angeuawa. Hapo, Sahl hakuingia Syria, na akarudi Madina.

Sahl alikuwa ni ndugu yake Uthman bin Hunaif. Yeye pia alikuwa ni sahaba wa Mtume (s.a.w.w.), na alikuwa amepigana katika vita vyake vyote, akijipatia sifa ndani yake kwa ujasiri wake.

5. Ubaidullah Ibn Abbas, Gavana Wa Yemen.

Ubaidullah alikuwa ni binamu wa kwanza wa Muhammad na Ali. Aliingia Yemen bila ya upinzani wowote na akachukua madaraka ya serikali. Yayla bin Umayya ambaye alikuwa gavana wa Uthman huko Yemen, alikuwa ameondoka kabla ya kufika kwake, na alikuwa amechukua hazina ya umma na kuondoka nayo.

6. Qathm Ibn Abbas, Gavana-Mteule Wa Makka.

Qathm alikuwa mdogo wake Ubaidullah. Anasemekana alikuwa amechukua kufanana kunakovutia sana na Mtume. Alikuwa bado yuko Madina wakati Makka ilipogeuka kuwa kituo cha upinzani kwa Ali. Yeye kwa hiyo, ilimbidi asubiri mpaka hali iliporudia kwenye kawaida huko Makka. Baada ya kifo cha Ali, aliondoka Arabia, akaenda Samarkand iliyoko Asia ya Kati, na akafa huko.

Miezi michache baada ya kupanda kwake kwenye mamlaka, ilimbidi Ali aondoke Madina kwenda Basra kukabiliana na changamoto ya waasi, na alimteua Sahl bin Hunaif Ansari kuwa gavana wa makao makuu katika kutokuwepo kwake yeye mwenyewe.

Baada ya vita ya Basra, Ali alimteua Abdallah ibn Abbas kama gavana mpya wa mji ule. Abdallah alikuwa ni “mwanafunzi wa kuchukua kazi” ya bwana wake, Ali, na alipata umaarufu mkubwa kwa elimu yake. Alikuwa ni mmoja wa mabingwa wa mwanzo kabisa katika tafsiri ya Qur’an Tukufu. Alikufa huko Taif akiwa na umri wa miaka 70.