read

Arabia Kabla Ya Uislamu

Katika kuandika historia ya Uislamu, ni kawaida kuanza na ukaguzi wa hali ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na ya kidini ya Arabia kabla tu ya tangazo la Muhammad (s.a.w.) la ujumbe wake kama Mtume wa Allah (s.w.t.)

Ndio mapatano ya pili ya wanahistoria (ya kwanza likiwa ni kutoa maelezo ya ki- jogografia ya eneo hilo). Nitazingatia mapatano haya, na nitachambua kwa ufupi, hali ya kijumla katika Arabia katika mwisho wa karne ya sita na mwanzo wa karne ya saba A.D.

Hali Ya Kisiasa Katika Arabia.

Sura inayoonekana sana ya maisha ya kisiasa ya Arabia kabla ya Uislamu ilikuwa ni kutokuwepo kabisa kwa mfumo wa kisiasa katika muundo wowote ule. Ukiiondoa Yemen iliyoko Kusini Magharibi, hakuna sehemu ya peninsula ya Arabia iliyokuwa na serikali kwa wakati wowote ule, na Waarabu kamwe hawakutambua mamlaka yoyote ile mbali na mamlaka ya machifu wao wa makabila yao. Haya mamlaka ya machifu wa kikabila hata hivyo, yaliegama, kwa namna nyingi, juu ya tabia na nafasi zao, na yalikuwa ya uungwana kuliko kisiasa.

Mwanafunzi wa kisasa wa historia anaona mshangao kwamba Waarabu wameishi, kizazi baada ya kizazi, karne baada ya karne, bila ya serikali ya aina yoyote ile. Kwa vile hapakuwa na serikali, hapakuwa na sheria na utulivu. Kanuni pekee ya nchi ilikuwa ni hali ya uhalifu. Kama inavyotokea, inapofanyika jinai, upande uliodhuriwa ulichukua hatua mikononi mwao, na ukajabiru kupitisha ‘hukumu’ kwa yule mwovu. Mtindo huu ulis- ababisha mara nyingi matendo ya ukatili wa kuogofya.

Kama Waarabu walifanya kiasi kidogo cha kujizuia, haikuwa ni kwa sababu ya wepesi wa hisia alizokuwa nazo juu ya maswali ya kweli na batili lakini ni kwa sababu ya kuhofia kuchochea visasi na mauaji ya kurithi kisasi. Mauaji ya kisasi cha kurithi yalimaliza vizazi vizima vya Waarabu. Kwa vile hakukuwepo na vitu kama polisi, mahakama au majaji, ulinzi pekee mtu alioweza kuupata kutokana na maadui zake, ulikuwa katika kabila lake mwenyewe.

Kabila lilikuwa na jukumu la kulinda watu wake hata kama walitenda maovu. Ukabila au ‘asabiyya’ (moyo wa kiukoo) ulichukua nafasi ya kwanza kabla ya maadili. Kabila lililoshindwa kulinda watu wake kutokana na maadui zao lilijihatarisha kwenye kebehi, kashfa na dharau. Maadili, kwa kweli hayakuingia kwenye picha mahali popote pale. Kwa vile Arabia haikuwa na serikali; na kwa vile waarabu walikuwa na utawala huria kwa silika yao, walifungana katika mapigano yasiyokwisha. Vita ilikuwa ni desturi ya kudumu ya jamii ya kiarabu.

Jangwa liliweza kuchukua idadi ndogo tu ya watu, na hali ya vita vya kikabila ilidumisha uthibiti mkali juu ya ongezeko la watu. Lakini Waarabu wenyewe hawakuiona vita katika mwanga huu. Kwao wao, vita vilikuwa burudani au kiasi mchezo wa hatari, au aina ya tamthiliya ya kikabila, iliyofanywa na wenye weledi (ubingwa), kwa mujibu wa mfumo wa kanuni za zamani na ushujaa, ambapo “watazamaji” walishangilia.

Amani ya kudumu haikuwa na mvuto kwao na vita vilitoa fursa ya kukwepa kazi ngumu na kutokubadilika kwa mwenendo wa maisha katika jangwa. Wao kwa hiyo walichochea msisimko wa mapambano ya silaha. Vita viliwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika kutupa mishale, ufundi wa kurusha panga na upandaji wa farasi, na pia, katika vita, wangeweza kujipatia sifa kwa ushujaa wao na wakati huohuo kuleta fahari na heshima kwa makabila yao. Kwa mara nyingi, Waarabu walipigana ili kupigana tu, ama iwepo au isiwepo sababu ya kuchochea vita.

Anasema G.E.Grunebaum:

“Katika karne ya kabla ya kuja Uislamu makabila yalitawanya nguvu zao zote katika vita vya kuviziana, wote dhidi ya wote.” (Classical Islam - A History 600-1258-1970)

Yale makabila ya wahamaji yalizunguka kwenye peninsula yote na kupora misafara na makazi madogomadogo. Misafara mingi na vijiji vilinunua kinga ya mashambulizi Haya kwa kulipa kiwango maalum cha fedha kwa watekanyara wa wahamaji.

Ni muhimu kuzingatia ule ukweli katika usiku wa kuzaliwa Uislamu hakukuwa na serikali katika ngazi yoyote katika Arabia, na ukweli huu unawezakuwa umeathiri kuinukia kwa Uislamu wenyewe. Ukosekanaji mzima wa serikali, hata katika hali ya kuanzishwa tu, ni kitu kisichokuwa cha kawaida kabisa kwamba kimeonwa na kutolewa maoni na mustashirik wengi, miongoni mwao ni:

D.S. Margoliouth:

“Arabia ingebakia ya kipagani angekuwapo mtu katika Makka ambaye angeweza kutoa pigo; ambaye angeweza kutenda. Lakini wengi wao, kama walivyokuwa wabaya wa Moham med, hapakuwa na mmoja wao aliyekuwa na ujasiri wa namna hii; na (kama ilivyoonekana) hapakuwepo na mahakimu kwa ujumla ambao kwao angeweza kushitakiwa. (Mohammed and the Rise of Islam, 1971)

Naye Maxime Rodinson Asema:

“Mauaji ya halaiki yalibeba adhabu kubwa kwa mujibu wa sheria zisizoandikwa za jangwani. Katika utendaji waarabu huru walikuwa hawakufungwa na kanuni ya sheria zake kwa msaada wa jeshi la polisi. Ulinzi pekee wa maisha ya mtu ni ile hakika iliyowekwa na mila na desturi, ambayo ingenunuliwa kwa gharama kubwa. Damu kwa damu na uhai kwa uhai. Kisasi cha kurithi, tha’r, kwa kiarabu, ni moja ya misingi ya jamii ya kibedui.” (Mohammed, 1971)

Asema Herbert J. Muller:

“Katika Arabia ya Mohammed hakukuwa na dola kulikuwa tu na makabila huru yaliyotangaa na miji. Huyu Mtume (s.a.w.) aliunda dola yake mwenyewe, na aliipa sheria tukufu iliyoandikwa na Allah (s.w.t.)”
(The Loom of History, 1958)

Watu wa Arabia walitokana na makundi mawili, wenye maskani na wahamiaji. Hijazi na Arabia ya Kusini ilitapakaa miji mingi midogo na mikubwa michache. Nchi yote iliyobakia illikuwa na watu waliotapakaa wakitokana na Mabedui. Walikuwa nyuma katika dhana ya uraia na siasa lakini pia walikuwa ni chanzo cha wasiwasi na hofu kwa wale wenye maskani. Waliishi kama maharamia wa jangwani, na walikuwa na sifa mbaya kwa ubinafsi wao usiozuilika na vurugu zao za upambanuzi wa kikabila.

Yale makabila maarufu zaidi yalitumia kiwango maalum cha mamlaka katika maeneo yao husika. Katika Makka kabila lenye nguvu lilikuwa la Quraishi, katika Yathrib, makabila yenye nguvu yalikuwa ni yale makabila ya Kiarabu ya Aus na Khazraji, na makabila ya kiyahudi ya Nadhir, Qaynuqa’a na Quraydha. Maquraishi wa Makka walijiona wenyewe ni bora kuliko Mabedui lakini hawa Mabedui walikuwa na dharau tu juu ya hawa watu wa mjini ambao kwao wao walikuwa ni “Taifa la wauza maduka tu”.

Waarabu wote walikuwa na sifa mbaya kwa namna fulani ya tabia kama vile majivuno, kiburi na majisifu, ulipizaji kisasi na kupenda kwingi uporaji. Kiburi chao kilihusika kwa namna fulani na kushindwa kwao kuanzisha dola yao wenyewe. Walikosa nidhamu ya kisiasa, na mpaka kuja kwa Uislamu, hawakutambua mamlaka yoyote kama ni yenye umuhimu mkubwa katika Arabia.

Walitambua mamlaka ya mtu aliyewaongoza kwenye uvamizi lakini angeweza kulaz- imisha utii wao ikiwa tu walikuwa na uhakika wa kupata mgao mzuri wa ngawira, na mam- laka yake yaliisha mara tu shughuli hiyo ilipokwisha.

Hali Ya Kiuchumi

Kiuchumi, Wayahudi ndio waliokuwa viongozi wa Arabia. Walikuwa ndio wenye ardhi nzuri yenye kulimika katika Hijazi, na walikuwa wakulima wazuri zaidi nchini humo. Walikuwa pia ndio wawekezaji wa vile viwanda vilivyokuwepo katika Arabia wakati huo, na walikamata ukiritimba wa utengenezaji wa zana za kivita.

Utumwa ulikuwa ni asisi ya kiuchumi ya Waarabu. Watumwa wa kiume na wa kike waliuzwa na kununuliwa kama wanyama, na waliunda tabaka la waliokandamizwa zaidi kati- ka jamii ya kiarabu.

Tabaka lenye nguvu zaidi, la waarabu, liliundwa na mabepari na wakopeshaji fedha. Viwango vya riba walivyotoza kwenye mikopo vilikuwa vikubwa mno, na viliundwa maalum kuwafanya matajiri zaidi na zaidi, na wale wakopaji kuwa masikini zaidi.

Vituo maarufu zaidi vya mjini katika Arabia vilikuwa Makka na Yathrib, vyote katika Hijazi. Wakazi wa Makka zaidi walikuwa ni wafanyabiashara, wachuuzi na wakopeshaji wa fedha.

Misafara yao ilisafiri wakati wa kiangazi kwenda Syria na wakati wa kipupwe kwenda Yemen. Walisafiri pia kwenda Bahrain upande wa Mashariki na Iraq upande wa Kaskazini Mashariki. Misafara ya biashara ilikuwa msingi wa uchumi wa Makka, na kuiendesha kwake kulihitaji ujuzi, uzoefu na uwezo.

R.V.C. Bodley Asema:

“Kuwasili na kuondoka kwa misafara kulikuwa ni matukio muhimu katika maisha ya watu wa Makka. Karibu kila mmoja ndani ya Makka alikuwa na namna ya kitega uchumi katika ile mali ya maelfu ya ngamia, mamia ya watu, farasi na punda walioondoka na ngozi za wanyama, zabibu kavu na minara ya fedha na kurudi na mafuta, manukato na bidhaa mbalimbali kutoka Syria, Misri na Fursi (Persia), na viungo na dhahabu kutoka upande wa Kusini.”(The Messenger, 1946, Uk. 31)

Huko Yathrib, Waarabu waliendesha maisha yao kwa kilimo na Wayahudi waliendesha maisha yao kama wafanyabiashara na wanaviwanda. Lakini Wayahudi hawakuwa wafanyabiashara tu na viwanda; miongoni mwao pia walikuwepo wakulima wengi, na wameileta ardhi nyingi mbovu kwenye kulimika. Kiuchumi, kijamii na kisiasa, Hijazi ilikuwa ndio sehemu mashuhuri zaidi katika Arabia mwanzoni mwa karne ya saba.

Francesco Gabrielli Anasema:

“Katika mkesha wa Uislamu, watu wenye kujishughulisha mno na walioendelea wa Arabia waliishi katika mji wa Maquraish. Wakati wa himaya za Arabu ya Kusini za Petra na Palmyra ulikuwa umepita kwa muda kiasi katika historia ya Arabia. Sasa hali ya baadae ilikuwa inaandaliwa hapo katika Hijazi.”
(The Arabs – A Compact History-1963)

Waarabu na Wayahudi wote walikula riba. Wengi miongoni mwao walikuwa wala riba wajuzi; waliishi kwa riba waliyotoza kwenye mikopo yao.

E.A.Belyaev Anaeleza:

“Riba ilitumika sana Makka, kwani ili kushiriki katika msafara wenye faida, watu wa Makka wengi waliokuwa na kipato cha wastani walikimbilia kwa wala riba; mbali na riba kubwa, angeweza kutegemea kupata faida baada ya kurudi salama kwa msafara. Wafanyabiashara matajiri zaidi walikuwa wachuuzi na wala riba.

Wakopeshaji fedha kwa kawaida walichukua dinari kwa dinari, dirham kwa dirham, kwa maneno mengine, asilimia mia moja ya riba. Katika Qur’an 3:125, Allah (s.w.t.) akiwaambia waumini, alisema: ‘Msile riba mara mbili maradufu.’ Hii ingeweza kumaanisha kwamba riba ya asilimia mia mbili au hata mia nne ilidaiwa.

Nyavu za riba ya Makka hazikuwakamata wakazi wenzao tu na wa makabila yao bali pia watu wa makabila ya Ki-Bedui ya Hijazi walioshugulika katika biashara ya Makka. Kama katika Athens ya zamani “njia kuu za kukandamiza uhuru wa watu zilikuwa ni pesa.”
(Arabs, Islamu and the Arab Caliphate in Early Middle Ages,1969)